Urusi na Ukraine: Nini kinachofahamika juu ya ubakaji katika vita vya Ukraine na unachunguzwa vipi?

Chanzo cha picha, Spencer Platt/Getty Images
Katika majimbo yaliyokombolewa na miji nchini Ukraine, wenyeji na waandishi wa Habari wanagundua Ushahidi wa ubakaji uliotekelezwa na wanajeshi wa Urusi. Ripoti kadhaa za ubakaji zinaendelea kuongezeka kila siku, lakini sio rahisi kuelewa kiwango halisi cha kile kinachotokea. Huku ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu wa Ukraine ilitangaza kufanya uchunguzi juu ya kisa kimoja tu cha ubakaji, mashirika ya kujitolea na ya haki za binadamu yamekwishaanza kukusanya ushahidi kutoka kwa waathiriwa.
Kuna matukio zaidi
Mwendesha mashitaka mkuu wa Ukraine Irina Venediktova alizungumzia kuwanza uchunguzi wa kisa kimoja cha ubakaji ambapo muathiriwa alizungumza na waandishi wa gazeti la Times. Chapisho hilo lilidai kwamba mwanamke mwenye umri wa miaka 33 kwa jina Natalya , mbazi wa mji wa Brovary karibu na Kiev, alifanyiwa ubakaji. Mwanamke huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa jeshi la Urusi lilimpiga risasi mume wake na kumbaka yeye huku mtaoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka minne akiwa kando yake. Natalya alifanikiwa kutoroka wakati wanajeshi wa Urusi walipokuwa wamelala usingizi.
Irina Venediktova anasema ofisi ya mwendesha mashitaka iliweza kumtambua mwanajeshi mmoja-alihukumiwa bila kuwepokwa tuhuma za kutekeleza uhalifu.
BBC ilizungumza na wanasaikolojia ambao walijitolea kutoa usaidizi wa kisaikolojia kwa wale walioathiriwa na vita. Kulingana nao, kuna visa vingi zaidi vya unyanyasaji wa kingono katika Ukraine kuliko vinavyojulikana.
Mtaalam Vasilisa Levchenko anasema kwamba manusura wa unyanyasaji wa kingono waliwasiliana naye. Kwa mfano mmoja wao alimwambia mwanasaikolojia kwamba msichana wake mdogo alikuwa amebakwa. Kulingana na mwanamke huyu, "baada ya kubakwa [binti] alikuwa anavuja damu." Jirani mwingine aliisaidia familia -wanawake wawili walimpeleka msichana hospitalini pamoja. Vasilisa Levchenko anasema kwamba mshichana hakuweza kuongea kwa siku kadhaa . Mwanasaikolojia hajui jinsi hatma ya mama na msichana wake ilivyokuwa.

Chanzo cha picha, SERGEI SUPINSKY/AFP via Getty Images
Mwanasaikolojia mwingine(ambayealiomba jina lake lisitajwe katika makala hii) aliithibitishia BBC kwamba watu kadhaa waliwasiliana naye kwa visa kadhaa vya ubakaji wakitaka usaidizi.
Kutokana na idadi kubwa ya jumbe zinazohusiana na ubakaji, wanaharakati wa haki za binadamu na wahudumu wa kujitolea sasa wanakusanya ushahidi wa visa hivyo nchini Ukraine.

Chanzo cha picha, Chris McGrath/Getty Images
"Ninafikiria tunazungumzia idadi kubwa ya visa vya unyanyasaji ," anasema Kateryna Busol, wakili wa Ukraine kuhusu sheria ya kimataifa katika taasisi ya Uingereza ya Chatham House , ambaye awali alifanya kazi katika kesi za unyanyasaji wa kingono katika maeneo yaliyojitangazia kujitenga ya DPR and LNR.
Hali ni tata kutokana na ukweli kwamba baadhi ya maeneo bado yako chini ya udhibiti wa Urusi, na wahudumu wa kijiyolea na mawakli hawawezi kukusanya Ushahidi wa waathiriwa, anasema Busol. " Lakini la muhimu zaidi , hivi ni visa ambavyo ni vigumu , kwa waathiriwa kuzungumza kuhusu unyanyasaji. Kwa sasa hatuna idadi kamili," anasema mtaalamu.
"Inanikumbusha kuhusu msichana tuliyesoma naye darasa moja''
Shirika la kutetea haki za binadamu - Human Rights Watch lilipata ripoti kadhaa za ubakaji, lakini lilijumuisha kisa kimoja tu katika ripoti yake juu ya vita.
"Watu wengine watatu walituambia juu ya kisa kimoja cha ubakaji wanachokijua. Lakini hatukukijumuisha katika ripoti. Tunatakiwa kuwa waangalifu san ana kuzungumzia tu taarirfa sahihi tulizonazo. Hatuwezi kusema ni v ubakaji umekithiri kwa kiwango gani ."katika vita hivi," anasema Rachel Denber,mwandishi mwenza wa ripoti.
HRW linaelezea hadithi ya mkazi wa kijiji katika jimbo la Kharkiv. Olga (sio jina lake halisi), na binti yake mdogo, mtu mwingine wa famialia na wakazi wengine makumi kadhaa wa eneo, waliojificha katika chumba cha chini ya ardhi cha shule yae neo hilo wakati Warusi walipoingia katika kijiji hicho.
Olga aliwambia wanaharakati kuwa tarehe Machi 13, mwanajeshi wa Urusi alivamia katika shule walimokuwa wamejificha na kumwambia amfuate..alimchukua mwanamke katika darasa katika gorofa ya pili, na kumuwekea mtutu wa bunduki na kumuamrisha avue nguo.
HRW inaandika kuwa mwanajeshi huyo alimbaka mwanamke huyo mara kadhaa, huku akiendelea kumtishia kwa bunduki, na kufyatua risasi juu.
"Alisema nilimkumbusha msichana aliyesoma naye shule katika darasa moja ," Olga alinukuliwa akiiambia HRW.
Olga anadai kwamba mwanajeshi huyo alimpiga usoni kwa kitabu na kumuachia jeraha kwenye shingo yake na shavu ambapo alimkata kwa kisu - picha inayothibitisha maneno haya iko mikononi mwa HRW.
Rachel Denber aliiambia BBC kuwa Olga aliweza kuondoka kijijini, akafika Kharkiv na kupata usaidizi wa matibabu.
Wizara ya Ukraine ya ulinzi inalilaumu jeshi la Urusi kwa kisa kingine cha ubakaji. Inadai kwamba katika mji wa Mariupol wanajeshi kadhaa walimbaka mwanamke mbele yam toto wake mdogo wa kiume. Mwanamke huyo alikufa baadaye. Baadaye, mhudumu wa kujitolea Yulia Smirnova aliandika kuwa mvulana aliyejeruhiwa alipelekwa hospitalini-alikuwa katika mshituko mkubwa. Mhudumu aliweza kuwapata ndugu za mama yake aliyeuawa wanaoishi katika eneo la Prague - ambao walielezea kuwa wako tayari kumlea mtoto huyo.
Kufedheheshwa zaidi
Mtyaalamu wa saikolojia Katerina Busol anakumbuka tukio la kushitusha zaidi kwake lilikuwa ni ushahidi wa wanawake ambao walinyanyaswa kingono mbele ya familia na Watoto wao: " Hii ni fedheha ya kiwango cha juu zaidi . Hauna thamani kama mtu, kama mwanamke, au kama mwanafamilia.
Hauna maana yoyote "Tuko hapa kukuangamiza kwa kila njia yoyote iwezekanavyo, ikiwa ni pamoja na aina hiyo ya unaynyasaji. Hadi februari 2022, sikuwa nimekutana na visa vya aina hii katika mzozo baina ya Urusi na Ukraine."
Balozi wa Uingereza katika Ukraine Melinda Simmons pia alizungumzia juu ya ubakaji "Ni silaha ya vita. Ingawa bado hatujajua kikamilifu matumizi yake katika Ukraine, ni wazi kwamba ilikuwa ni sehemu ya silaha ya Warusi ," alisema balozi.

Chanzo cha picha, Nichole Sobecki/AFP via Getty Images
Katika sheria ya kimataifa, unaynyasaji wa kingono ulianza kuchukuliwa kama aina ya mauaji ya kimbari (genocide), kutokana na uamuzi wa mahakama ya kimataifa ya mauaji ya Rwanda (ICTR) -ni pale ambapo ubakaji ulitambuliwa kama silaha ya vita na mara kwa mara ulifanyika huku umati wa watu ukushuhudia- kwa pamoja wakazi na na jeshi.
Waziri wa habari war ais wa Urusi - Dmitry Peskov alizitaja taarifa kuhusu ubakaji uliotekelezwa na wanajeshi wa Urusi katika eneo la Ukraine uongo, bila hata kuelezea kwamba ripoti hiyo inapaswa kuangaliwa au kuchunguzwa.
Uchunguzi wa visa vya uhalifu wa kivita, ukiwemo ubakaji, unaweza kufanywa na Mahakam aya uhalifu ya kimataifa, ambapo Ukraine sasa ina matumaini makubwa ya kuendeshwa kwa kesi juu ya visa hivyo . Mahakama hatahivyo, huchunguza tu visa ambavyo vinaweza kuwatia hatiani wat una kubaini uwezo wao wa kibinafsi wa kutekeleza uhalifu unaotajwa.
Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine:Mengi zaidi
- MOJA KWA MOJA: Wanajeshi wa Urusi wanaotumia parachuti waishambua Kharkiv
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine













