Twitter: Kwa nini Elon Musk alioa mwanamke mmoja mara mbili?

Chanzo cha picha, Reuters
Elon Musk, mmoja wa watu tajiri zaidi duniani, mvumbuzi wa gari la umeme, mwenye ndoto ya kuhakikisha mwanadamu anaweza kuishi katika anga la mbali, sasa atakuwa mkuu wa mtandao wa Twitter.
Elon Musk atamiliki Twitter kwa kitita cha bilioni 44.
Bodi ya Twitter imeidhinisha hili.
Elon Musk, mwanzilishi mwenza wa Tesla na Space-X, ana utajiri wa zaidi ya bilioni 200.
Lakini maisha ya bilionea huyu sio ya kuvutia sana.
Je! unajua mambo yanayomkabili katika maisha yake?
1. Kuvutiwa na hadithi za kisayansi na umeme
Elon Musk alizaliwa Pretoria, Afrika Kusini. Tangu utotoni, alipendezwa na hadithi za kisayansi na umeme.
Kulingana na wengine, kivutio hiki kilionekana zaidi katika kampuni zao, SpaceX na Tesla. Katika umri wa miaka kumi na saba, Musk alikwenda Canada kusoma fizikia na uchumi. Mnamo mwaka 1992, aliingia chuo kikuu huko Marekani.
2. Aliacha chuo ndani ya siku mbili
Baada ya kujiunga na chuo kwa ajili ya kufanya PhD nchini Marekani, aliacha chuo ndani ya siku mbili na kuzindua gazeti la mtandaoni la Zip2.
Baadaye aliuza kampuni na kuanzisha PayPal. Mnamo mwaka 2002, akiwa na umri wa miaka 31, aliuza kampuni ya PayPal kwa eBay kwa bilioni 1.5.
3. Sio mwanzilishi wa kampuni ya Tesla
Ingawa Elon Musk na Tesla ni sawa leo, Musk hakuanzisha Tesla.
Hapo awali alikuwa mwenyekiti wa kampuni ya Tesla na mnamo mwaka 2008 akawa afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo. Musk alikuwa na pesa nyingi baada ya kuuza kampuni ya PayPal.
Waliwekeza pesa hizo kwa kampuni kama SpaceX na Tesla. Lakini mwanzoni, kampuni zote mbili zilishindwa. SpaceX ilipata ajali tatu mfululizo za roketi.
4. Elon Musk alimuoa mwanamke mmoja mara mbili
Elon Musk ameoa mara tatu, lakini mara mbili kwa mwanamke mmoja.
Ndoa ya kwanza ya Musk ilikuwa kwa Justin Wilson. Alikuwa mwandishi wa mambo yasiyo ya kweli.
Walifunga ndoa mwaka wa 2000 na kuachana mwaka wa 2008. Musk baadaye alimuoa Talulah Riley mwaka wa 2010. Lakini ndani ya miaka miwili, waliachana.
Lakini mwaka uliofuata, 2013, wawili hao walifunga ndoa tena ila mzunguko wa ndoa-talaka-ndoa haukuishia hapo.
Mnamo mwaka 2014, Musk aliwasilisha tena talaka na akajiondoa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mnamo mwaka 2016, Talulah Riley aliwasilisha talaka tena na wakatengana. Inasemekana kwamba mwigizaji Robert Downey Jr. aliongozwa na whimsy ya Elon Musk kwa uhusika wake katika filamu ya Iron Man.
Mnamo mwaka wa 2018, mwimbaji wa pop wa Canada Grimes (jina halisi Claire Butcher) na Musk walikutana.
5. Alitaja jina la mtoto na kuhakikisha hakuna mtu mwingine anayeweza kulitamka
Grimes na Musk wamekuwa wakichumbiana kwa miaka minne iliyopita.
Walipata mtoto wa kiume mnamo mwaka 2020. Jina lake ni X Æ A-12. Kulikuwa na hisia nyingi kwenye Twitter wakati wawili hao walipotangaza jina la mtoto. Kila mtu alikuwa akiuliza swali moja, jinsi ya kutamka jina hili haswa.

Chanzo cha picha, Elon Musk
Grimes baadaye alifafanua jina hilo kwenye Twitter.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
''Sasa Grimes na Musk wanaishi mbalimbali, Musk alisema katika mahojiano.
Akihojiwa na jarida la Page Six la New York alisema, ''Tunapendana, lakini hatuwezi kukaa pamoja kwa muda mrefu kwa sababu ya kazi zetu. Tumekaa mbali kwa muda mrefu, hivyo karibu tutengane.''
6.Gari la michezo lilitumwa kwenye anga ya mbali
Mnamo mwaka 2018, kampuni ya Musk ilizindua roketi nzito ya Falcon kwenye anga la mbali.
Iliruka kwa takriban sekunde 154, na kisha ikaachiliwa. Wakati sehemu zingine za roketi zilidondoka kutoka kwa mwili mkuu, tukio jipya lilionekana ulimwenguni.
Gari nyekundu ya michezo ya umeme. Gari hilo lilikuwa limepelekwa kwenye anga la mbali. Nyuma ya haya yote, bila shaka, alikuwa Musk.
Gari hilo pia lilikuwa la kapuni ya Tesla. Wimbo wa 'Space Odity' ulikuwa ukichezwa kwenye gari hili. Na utaimba kwenye anga la mbali milele.

Chanzo cha picha, SpaceX
Akizungumzia hilo, Musk alisema, ''Ni kweli kwamba hili lilikuwa tukio lisilo la kawaida. Lakini kuna furaha nyingi zinazoendelea katika maisha.''
7. Mhalifu wa ngono aliyeshtakiwa kwa kuokoa watoto walionaswa kwenye pango nchini Thailand.
Je, unakumbuka watoto hao ambao walikwama kwenye pango nchini Thailand mnamo 2018?
Mnamo Juni 23, watoto 12 na kocha wao mwenye umri wa miaka 25 waliingia kwenye pango la Tham Luang katika eneo la Chiang Rai kaskazini mwa Thailand baada ya kufanya mazoezi ya soka.
Lakini tangu wakati huo hakuna mtu aliyesikia sauti yake.
Wavulana hao walikuwa wamenaswa katika pango lililojaa maji kwa siku 18. Mpiga mbizi aliyekwenda kumuokoa pia aliuawa.

Chanzo cha picha, EPA
Baadaye watoto hao waliachiliwa wakiwa salama.
Mpiga mbizi wa Uingereza, Vernon Unsworth, alichangia jukumu muhimu katika kufikiwa kwa hatua hiyo.
Lakini Elon Musk alikuwa ametoa madai ya kutisha ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto dhidi ya mzamiaji huyo.
Alitoa madai hayo kwenye Twitter Musk na alikuwa amesema Vernon alibaka Watoto hao. Vernon pia alikuwa amewasilisha kesi ya kuchafuliwa sifa dhidi ya Musk. Alikuwa amedai fidia ya mamilioni ya dola.
Baadaye Musk aliufuta ujumbe wake kwenye mtandao wa Twitter na kumuomba msamaha Vernon.
Pia aliomba msamaha kwa Vernon mahakamani. Hata hivyo, baraza la majaji, hata hivyo, liliamua kwamba matamshi ya Musk hayakuchafua jina la Vernon Unsworth.












