Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Nigeria: Nini kitafanyiwa wanawake 18 wa Mfalme Lamidi Olayiwola Adeyemi wa III aliyefariki?
Wakati wa uhai wake, Mfalme, Lamidi Olayiwola Adeyemi wa III alikuwa amewaoa wanawake kadhaa- Jumla ya wanawake 18 ndio wanaojulikana.
Kulingana na taarifa tofauti, wanaume wengi ambao wamefika katika kasri ya Mfalme Olayiwola kutoa rambi rambi zao, wamefika huko kutokana na wasi wasi waliokuwa nao kuwahusu Malkia wake.
Katika utamaduni wa kabila la Yorùbá, inaaminiwa kwamba hakuna mwanamke anayeruhusiwa kumuoa mwanamke ambaye mfalme alikuwa amemuoa, hususan mfalme maarufu kama Alaafin.
Idhaa ya BBC News Yoruba ilizungumza na wazee kubaini hatma ya wake hawa 18, ambao wengi wao bado wana umri mdogo, ambao Mfalme Alaafin amewaacha baada ya kifo chake.
Kulingana na Baba Araba wa ardhi ya Osogbo katika jimbo la Osun, Chifu Ifayemi Elebuibon, malkia hao watatakiwa kufanya kile kinachoitwa "opo", matambiko ya kitamaduni ambayo wajane hufanya katika mila za Yoruba wakati wanapofiwa na wame zao.
Hii inamaanisha kwamba malkia hao hawataonekana hadharani kwa kipindi fulani na hatahudhuria sherehe au haflla kwa kipindi fulani.
"Utakaswaji wa kiroho kabla ya kuweza kuolewa na mwanaume mwingine"
Elebuibon anasema mamalkia wako huru kuondoka kwenye kasri baada ya kufanyiwa matambiko yanayoitwa opo , lakini ni lazima watakaswe kabla yay a kuolewa na mwanaume mwingine.
Alielezea kwamba malkia hao watapitia utaratibu wa utakaswaji wa kiroho ili kuondolewa haki za Mfalme Alaafin kabla ya mwanaume mwingine kuwa na haki kwao.
Aliongeza kuwa wale miongoni mwao wanaoamua kuishi katika kasri watakuwa ni mali ya yeyote atakaye atakayekuwa mfalme mpya.
Pia akizungujmza mtawala Adimula wa Ila Orangun, Chifu Fagbenle Adedayo, alisema kuwa malikia wote wajane walioachwa na Mfalme wamepitia matambiko kabla ya kuolewa na mfalme na kwahiyo lazima wapitie mchakato sawa na huo kabla ya kuolewa na ten ana mwanaume mwingine.