Urusi na Ukraine: Ni kwanini vita vijavyo vya Donbas mashariki mwa Ukraine vinatarajiwa kuwa vya umwagaji damu na vya maamuzi?

Watu katika mashariki mwa Ukraine wanafahamu kuwa Warusi wanakaribia kuwavamia kwa mashambulizi hapa. Hata mbwa mitaani wanaonekana kujua fika, na wanaweza kusikika wakibweka kila mara kombora zito linapoaunga umbali nae neo hili.

Maelfu kwa maelfu ya watu tayari wamekwishatorokea katika maeneo yenye hali ya usalama kiasi ya magharibi mwa Ukraine. Kwa mara nyingine tena msururu mrefu wa magari ya Urusi umenaswa na picha za setilaiti -mara hii ukielekea eneo la masharariki.

Katika Donbas kumeshuhudiwa dalili za Ukraine ikileta zana zaidi za kijeshi, ikiwa ni pamoja na vifaru na mifumo ya ulinzi ya makombora ya masafa marefu ya anga. Lakini sio kwa kiwango cha Urusi.

Ukraine inaweza kuwa inatumia mbinu zaidi katika kuwapeleka wanajeshi wake Donbas au ina wanajeshi wachache. Haijafahamika.

Wengi wanaamini katika awamu ijayo ya vita katika mashariki inaweza kuamua matokeo ya mzozo huu. Wengi pia wanatarajia watu wengi watakufa katika vita awamu ijayo ya vita.

Kwa ombi letu, jeshi la Ukraine lilituonyesha moja ya maeneo ya makombora yao ambayo tayari yanashambulia maeneo ya Urusi. Njia pekee ya kufika pale ilikuwa ni kusafiri kwa vifaru vya kijeshi kupitia kwenye mashamba. Sehemu kubwa ya vita hapa vitapiganwa kwenye uwanja wa wazi. Vikosi vya Ukraine pia vitatumia fursa yao ya eneo lililochimbwa tayari katika maeneo ya ulinzi.

Kulikuwa na mifumo zaidi ya ulinzi wa mashambulio ya anga katika maeneo ya makombora, ikiwemo mifumo ya ulinzi ya kukabiliana na makombora ya masafa mafupi iliyotolewa na nchi za Magharibi. Ilikuwa nje ya masanduku yake na tayari kufyatua, iwapo ndege zisizo na rubani za Urusi au jeti zitashambulia maeneo yake .

Silaha za aina hiyo zimekuwa na athari muhimu katika vita hivi-huku urusi inaweza kuwa na uwezo wa kivita angani, bado haina udhibiti wa anga.

Makombora ya Ukraine hadi sasa yanawezesha kuwa na ufanisi. Hatukuweza kuona maeneo marefu ya makombora, lakini badala yake tuliona kikosi kidogo cha kikosi kinachoweza kuhama hama wakati inapobidi kufanya hivyo. Huku Warusi wakiwa na jeshi kubwa, vikosi vya Ukraine vinategemea zaidi maandalizi meme ya ulinzi na uwezo wake wa kuhama kutoka eneo moja kuelekea jingine.

Volodymyr,ambaye ni askari wa Ukraine, aliiambia BBC kwamba walilazimika kubadili maeneo yao ili kuepuka kulengwa.

"Kama tukikaa katika eneo moja kwa zaidi ya siku kadhaa, basi tunakuwa walengwa" alisema. Pia alielezea utofauti mwingine muhimu; makombora ya Ukraine yalikuwa ayanalenga maeneo ya kijeshi - makombora ya Urusi- huku Urusi ilikuwa ikilenga miji na majiji.

"Wanapiga katika miji yetu wasababu wanataka watu wakanganyikiwe na kuwa na hofu. Wanataka watu wetu wakate tamaa," alisema.

Urusi itahangaika kusonga mbele katika maeno muhimu huku Ukraine ikiendelea kuwa na kuwa na mifumo ya ulinzi dhidi ya mashambulizi ya anga na makombora. Pande zote mbili hadi sasa, zina idadi inayolingana ya wanajeshi katika kanda - ya takriban wanajeshi kati ya 30,000 hadi 40,000.

Lakini maafisa wa magharibi wanasema Urusi inalenga kuongeza idadi hiyo mara dufu au hata kuimarisha uwezo wake katika jimbo hilo. Baadhi wanakadiria kuwa Urusi imepoteza 20% ya uwezo wake tangu kuanza kwa vita hivi.

Ukraine pia imeimarisha mapambano ya vikosi vake katika kanda hiyo. Wamekuwa wakipigana na vikosi vilivyojitenga vinavyoungwa mkono na Urusi hapa kwa zaidi ya miaka minane iliyopita. Wamejizatiti vyema, wakitumia maeneo yao ya ulinzi waliyoyaandaa kwa miaka iliyopita. Baadhi ya wanajeshi wanaweza kuonekana wamechoka, lakini ari yao inaonekana iko juu.

Ukrainepia inapewa ujasusi wa wakati halisi juu ya kusonga mbele kwa jeshi la Urusi na washirika wake wa Magharibi. Hawawezi kuzungumzia kwa kina, lakini kwa pamoja maafisa wa Ukraine na wa magharibi wameithibitishia BBC .

Urusi bado ina faida ya idadi -maelfu ya wanajeshi zaidi wanaendelea kupelekwa vitani baada ya kushindwa katika uvamizi wake karibu na mji mkuu wa Ukraine Kyiv. Urusi pia kwa sasa inapigana katika maeno machache ya vita.

Ukraine pia ina tatizo jingine la kushugulikia- kudhibiti adui ndani yake. Katika mji wa Kramatorsk tulikwenda kwa kusindikizwa na doria ya polisi kuwatafuta wahujumu wa Warusi.

Kuna hisia zaidi za kuunga Urusi Donbas kuliko maeneo mengine ya Ukraine. Polisi walisimama na kuwasaka wapiti njia, wakitafuta Ushahidi kuwa wanaweza kuwa wasaliti wa Urusi. Walisaka simu za mkononi. Walikuwa na wasi wasi juu ya watu wanaopeleka taarifa na picha za maeneo ya ulinzi ya Waukraine.

Mkuu wa polisi wa eneo, Kanali Alexander Malish, aliiambia BBC watu wamefungwa na kuwasilishwa kwa huduma za ujasusi mara nyingi.

"Sielewi ni nini kilicho vichwani mwao... labda ni propaganda ya Urusi? Ninadhani kwamba baada ya vita watu wa Ukraine waangalia ni nini cha kufanya kuwahusu watu ambao wamekuwa wakisaidia vikosi vinavyovamia nchi ." Kanali Malish alisema ni sehemu ya vita vya Urusi.

Miji kadhaa ya mashariki mwa Ukraine imekuwa ikilengwa na mashambulio ya ndege ya Urusi, makombora na mashambulio ya bunduki.

BBC ilishuhudia kwa mbali ibada za wafu za raia wa Ukraine walioawa hivi karibuni.

Alexander Tislenko alikuwa na umri wa miaka 34 alipouawa katika eneo la mapigano, akipigana upande wa kikosi maalum cha Ukraine. Anayoyajua mama Tatiana kuhusu kifo chake, ni kwamba eneo alikokuwa lililengwa na maroketi makubwa ya Warusi, kabla aliambiwa aliuawa katika mapigano.

Tatiana alishikilia picha ya Alexander juu ya jeneza lake, ambalo lilikua limefunikwa kwa bendera ya Ukraine. Hakusita kulia. Alexander alikuwa ndiye mtoto wake pekee.

Baadaye , Tatiana aliiambia BBC : " Kijana wetu alikuwa amejitolea maisha yake kwa ardhi ya nyumbani ya Ukraine. Najivunia sana mtoto wangu, lakini ni hasara kubwa. Ni hasara kubwa ambayo siwezi kuisahau maishani mwangu. Namlaani rais wa Urusi Vladimir Putin."

Kwa kipindi cha wiki zijazo hapa mashariki mwa Ukraine kutakuw ana akina mama wengi watakaoomboleza katika nchi zote mbili Urusi na Ukraine. Awamu hii ya vita itakuwa ngumu kwa pande zote mbili. Zote zitakuwa na uwezekano mkubwa wa kuwapoteza watu.

Unaweza pia kusoma