Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Imran Khan aondolewa kama Waziri Mkuu wa Pakistan kufuatia kura ya kutokuwa na imani naye
Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan ameondolewa madarakani baada ya kupoteza kura ya kutokuwa na imani na uongozi wake.
Uamuzi wa kura hiyo ulifikiwa baada ya wabunge wa upinzani kuwasilisha hoja ya kutokuwa na umani naye, kufuatia siku kadhaa ya malumbano.
Kura ya kutokuwa na Imani dhidi ya Bw. Khan iliwasilishwa bungeni wiki iliyopita lakini iliipinga kwa kuvunja bunge.
Kura hiyo ya Jumapili ilifanyika baada ya Mahakama ya Juu zaidi nchini humo kutoa uamuzi uliounga mkono vyama vya upinzani na kusema kwamba hatua ya Bw. Khan ilikuka katiba.
Khan sasa ni Waziri Mkuu wa kwanza wa Pakistan kuondolewa madarakani kupitia kura ya kutokuwa na imani.
Bunge la Pakistan litakutana Jumatatu kumpigia kura kiongozi mpya wa nchi hiyo. Kiongozi atakayechaguliwa atashikilia uongozi hadi Oktoba 2023, wakati uchaguzi mkuu mwingineutakapofanyika.
Ayaz Sadiq, ambaye anasimamia bunge la kitaifa amesema karatasi za uteuzi wa wagombeaji zinapaswa kuwasilishwa kufikia saa tano usiku saa za nyumbani sawa na (06:00 GMT) siku wa Jumapili.
Vyama vya upinzani vilipata kura 174 katika bumge pa wajumbe 342 kuunga mkono hoja ya kutokuwa na Imani ,spika wa bunge wa bunge na kuifanya kushinda hoja hiyo kwa wingi wa kura.
Katika ujumbe wa kupitia mtandao wa Twitter, kiongozi wa upinzani Shehbaz Sharif alisema Pakistan na bunge lake "hatimaye limekombolewa dhidi ya mzozo mkubwaf ".
Bw. Sharif aliongeza: "Hongera kwa taifa la Pakistan kwa mapambazuko mapya."
'Njama ya Kimataifa'
Bwana Khan akikuwa amesema hataitambua serikali ya upinzani,akidai- bila ya kuwa na Ushahidi - kwamba kulikuwa na njama inayoongozwa na Marekani kumuondoa madarakani kwa sababu ya kusimama na Washington kuhusiana na masuala dhidi ya Urusi na China.
Amerudia kusema mara kadhaa kuwa vyama vya upinzani vya Pakistan vinafanya kazi na mataifa ya kigeni
Marekani imesema madai hayo "hayana msingi wowote", na kwamba Bw. Khan hajawahi kutoa Ushahidi wowote.
Alizuru Moscow kukutana na Rais Vladimir Putin wakati Urusi ikianzisha uvamizi wa Ukraine na hapo awali amekosoa kile ambacho utawala wa Bush ulikiita vita dhidi ya ugaidi.
Dakika chache kabla ya kura kuanza, spika wa bunge la Pakistani - mshirika wa Bw Khan - alitangaza kujiuzulu. Wanachama wa chama cha Bw Khan (PTI) waliondoka kwenye jumba hilo, wakisisitiza kuwa alikuwa mwathirika wa njama ya kimataifa.
Khan alivyoingia madarakani
Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya kriketi ya Pakistani alichaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka wa 2018, na kuahidi kupambana na ufisadi na kurekebisha uchumi.
Lakini ahadi hizo hazijafikiwa baada ya nchi kukumbwa na mzozo wa kifedha.
Mwishoni mwa mwezi Machi mfululizo wa uasi ulimnyima uliathiri uongozi wake na kumwacha akipigania tushawishi wake wa kisiasa.
Mwandishi wa BBC Secunder Kermani anasema Bw Khan anachukuliwa kuwa aliingia madarakani kwa usaidizi wa jeshi la Pakistan, lakini sasa wachunguzi wa mambo wanasema wametofautiana.
Seneta wa PTI Faisal Javed Khan alisema Bw Khan alitoka nje ya makao yake ya waziri mkuu "kwa neema na hakupiga magoti".
Seneta huyo aliendelea kusema kuwa waziri mkuu huyo wa zamani "ameliinua taifa zima".
Ni nini kilitokea wikendi iliyopita?
Kura hiyo ilipaswa kupigwa bungeni, lakini naibu spika Qasim Suri - mwanachama wa chama cha kisiasa cha Bw Khan - alizuia hoja hiyo, akisema ilionyesha "uingiliaji wa kigeni". Bw Suri pia alisema kuwa ni kinyume cha katiba, inayotaka uaminifu kwa serikali.
Serikali ya Bw Khan ilivunja bunge na kutaka uchaguzi ufanyike kwa haraka. Hili liliwakera wanachama kadhaa wa upinzani, huku baadhi wakimtuhumu waziri mkuu huyo kwa uhaini kwa kuzuia kura hiyo.