Makahaba wanaume na wake za watu wanavyoongezeka Iran

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mamlaka nchini Iran imekuwa ikisema kuwa hakuna ukahaba nchini humo

"Ninaona aibu kwa kile ninachofanya, lakini nina chaguo gani?" anasema Neda, mtalaka wa huko Tehran.

Wakati wa mchana amekuwa akifanya kazi kama msusi wa nywele, lakini usiku anafanya kazi yake ya pili kama kahaba, akihisi kulazimishwa kuingia kwenye biashara hiyo ya kuuza mwili wake kwa ngono ili kupata mkate wake wa kila siku.

"Ninaishi katika nchi ambayo wanawake hawaheshimiwi, uchumi unayumba, na bei ya kila kitu inapanda karibu kila siku," anasema. "Nalea mtoto mwenywe bila baba. Lazima nimtunze mwanangu. Ukahaba hulipa vizuri, na sasa ninapanga kununua nyumba ndogo jijini. Huu ndio ukweli wa kusikitisha wa maisha yangu. Kwa kweli ninauza utu wangu."

Mwaka 2012, Iran ilitangaza mpango wa kitaifa wa kukabiliana na ukahaba. Hata hivyo, kwa mujibu wa ripoti zisizo rasmi za mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) na watafiti, idadi ya watu wanaofanya kazi katika sekta hiyo ya ukahaba imeongezeka.

Nchi hiyo ya kidini ya kihafidhina ya Iran kwa muda mrefu imekuwa ikikanusha kuwepo kwa wauza ngono au makahaba nchini humo. Badala yake, mamlaka zinaelezea ukahaba huko kama njama ya Magharibi iliyoundwa kuwapotosha vijana, au kuwatupia mzigo wa lawama wanawake kwa kuwapotosha wanaume wasio na maadili.

Takwimu zisizo rasmi pia zinaonyesha kuwa wafanyakazi wa ngono wa Iran wanapungua. Takwimu kutoka mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali zinaonyesha kuwa mwaka 2016 wasichana wenye umri wa miaka 12 walijihusisha na ukahaba.

Shirika la Aftab Society, shirika lisilo la kiserikali lililojitolea kuwasaidia wanawake wanaojihusisha na dawa za kulevya nchini Iran, lilisema mwaka 2019 kwamba kunaweza kuwa na makahaba 10,000 katika mji mkuu, takribani asilimia 35% kati yao ni wake za watu.

Kwa mujibu wa Amir Mahmoud Harrichi, profesa wa ustawi wa jamii katika Chuo Kikuu cha Tehran, idadi ya wafanyakazi wa wa ngono mjini Tehran inaweza kuwa mara mbili zaidi.

"Wanaume wanajua kuwa ukahaba ni kinyume cha sheria nchini Iran na na wanawake huadhibiwa pakubwa wakigundulika, kwa hivyo wanaitumia kwa faida yao," anasema mmoja wa makahaba wa muda, Mahnaz, mwanafunzi katika chuo kikuu huko Tehran.

"Imenitokea mara kadhaa kwamba nilifanya mapenzi na mtu lakini hakunilipa na sikuweza kwenda kwa mamlaka kushitaki."

Mahnaz anasema gharama ya maisha mjini Tehran ni kubwa sana na kwamba bila kufanya kazi nyingine hataweza kulipa bili zake.

'Ndoa za furaha'

Kufuatia Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran ya mwaka 1979, baadhi ya makahaba walinyongwa na utawala mpya na madanguro yao yalifungwa. Katika jitihada za kuhalalisha matumizi ya wanawake kwa ajili ya ngono, kile kinachojulikana kama 'zawaj al-mutaa au "ndoa ya furaha" - ambayo ni ya mkataba unaojumuisha muda wa ndoa hiyo na kiasi cha fidia ama fedha atakayopewa mke wa muda - kikawa kimeenea zaidi.

Utaratibu huo umeenea katika miji takatifu ya Mashhad na Qom, ambayo hutembelewa na mahujaji wa Shia kutoka duniani kote. Video kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha wanaume wa Iraq wanaotafuta ngono huko Mashhad, ambapo maafisa wanasema kuwa wanajihusisha na ndoa za muda tu.

Sasa, kuna huduma nyingi za mtandaoni zinazotoa huduma za 'ndoa ya mutaa' nchini Iran, ikiwa ni pamoja na Telegram na WhatsApp, na vikundi kama hivyo vinadai vina idhini ya serikali.

Gharama ya miasha imepanda Iran

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Gharama ya miasha imepanda Iran

Moja ya sababu inayofanya gharama za maisha kupanda nchini Iran na kuchochea vitendo vya ukahaba ni vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na Marekani juu ya mpango wa nyuklia wa Iran. Tangu mwaka jana, mfumuko wa bei nchini Iran umeongezeka kwa asilimia 48.6. Ukosefu wa ajira pia umeongezeka na kwa wengi ambao wana kazi, hawalipwi vizuri.

Kutokana na hali hii, pia kumekuwa na ongezeko la idadi ya wanaume wenye umri kati ya miaka 20 na 35 ambao wanafanya mapenzi na wanawake kwa kulipwa pesa.

Mmoja wa vijana hao ni Kamyar, mwenye umri wa miaka 28, ambaye alikuwa akiishi na wazazi wake hadi mwaka jana na hakuweza kulipia gharama zake bila msaada wa baba yake. Sasa anaweza kumudu kukodisha ghorofa katikati ya Tehran na anatarajia kuhamia nje ya nchi siku moja.

"Ninapata wateja wangu kupitia akaunti za mitandao ya kijamii," anasema. "Kwa kawaida wanawake hawa wako katika umri wa miaka 30 na 40. Wakati mmoja nilikuwa na mteja ambaye alikuwa na umri wa miaka 54. Wananitendea vizuri, wanalipa pesa nzuri na mar azote nalala majumbani kwao. Na kwa njia ya mdomo tu (kuzungumza), ninapata wateja wengi."

Kamyar ni mhandisi msomi lakini haoni mustakabali wake mwenyewe katika sekta hiyo ambayo daima aliipenda.

"Siku zote nilitaka kuwa mhandisi. Lakini mtaani hakuna kazi," anasema.

"Nilimpenda msichana mmoja, lakini hatukuweza kuoana kwa sababu sikuwa na kazi inayoelewa. Sijivunii kile ninachokifanya sasa. Kulala na watu usiowajua ili kupata pesa haikuwa kwenye ndoto yangu wakati nakua. Kwa kweli, naona aibu, lakini inanisaidia kulipa bili.