Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mzozo wa Ukraine: Kutoka Chuo mpaka jeshini - Kutana na wanajeshi 'makinda' ya Ukraine
Wiki wiki moja iliyopita nilikutana na kundi la vijana wanaojitolea huko Kyiv kupigana kwa ajili ya kuilinda Ukraine.
Wengi wao ni vijana ambao si muda mrefu wametoka kumaliza shule. Waliniambia kwamba baada ya mafunzo ya msingi ya siku tatu wangekuwa mstari wa mbele - kupambana.
Maksym Lutsyk, mwanafunzi wa biolojia mwenye umri wa miaka 19, aliniambia kuwa hakuwa na tabu kujaribu kuwa mwanajeshi katika kipindi cha chini ya wiki moja cha mafunzo. Haikuwa ngumu kutokana na miaka mitano yake ya kuwa Skauti, mbali na mafunzo mengine lakini alijifunza pia mafunzo ya silaha.
Alikuwa na umri wa miaka 10 wakati vita vya muda mrefu vya Ukraine na waasi vilivyofadhiliwa na Moscow vilipoanza mwaka 2014.
Maksym alijiunga na rafiki yake Dmytro Kisilenko, 18, aliyekuwa akisoma masomo ya uchumi katika chuo kikuu kimoja.
Vijana hao walikuwa sehemu ya kundi lolote la vijana wadogo ambao walisema wao sio wadogo tena. Baadhi yao walionekana watoto wadogo waliokuja kwenye sherehe za siku zao za kuzaliwa za miaka 12. Wachache walibeba mifuko ya kulalia. Mmoja alikuwa na kitanda cha yoga. Wakati wanasubiri basi ambalo lilikuwa linawapeleka kwenye kituo cha mafunzo, walionekana kama marafiki waliokuwa njiani kuelekea kwenye tamasha - sio mafunzo ya bunduki. Kila mmoja alikuwa ameshika bunduki aina ya Kalashnikov.
Niko na Dmytro na Maksym na vijana wengine wanaojitolea. Mwishoni mwa wiki hii nilikwenda kuwaona kwenye machapisho yao kwenye kituo chao mashariki wa mji, ambapo walipewa sare, silaha na helmeti.
Dmytro aliniambia: "Nimeizoa bunduki yangu. Nilijifunza jinsi ya kupiga risasi na jinsi ya kufanya vitania, pia mambo mengine mengi ambayo yatakuwa muhimu sana katika mapambano dhidi ya Warusi." Alicheka, kana kwamba aliona vigumu kufikiria kile alichokuwa akitafakari.
Unaweza kusoma pia:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Kwa upande wake Maksym anasema: "Najiona jasiri zaidi kuliko nilivyokuwa hapo awali, kwa sababu tunapata ujuzi wa kutosha wa mbinu, katika sanaa ya kijeshi, mbinu na jinsi ya kufanya kitu kwenye uwanja wa vita." Akitania, anataka kuona bendera ya Kiukreni ikiruka kutoka Kremlin.
Swali kwenye akili ya kila mtu hapa ni je vita inakuja Kyiv?
"Inawezekana kabisa," alisema Dmytro. "Tunapaswa kuwazuia hapa, kwa sababu wakifika Kyiv vita hii inaweza kuwa imekwisha."
Wanatoka katika mji mmoja ulioko karibu na mpaka wa Urusi, ambao unashambuliwa. Familia zao bado zipo. Niliwauliza wavulana hao kile wazazi wao wanafikiria nini kuhusu uamuzi wao huo. Maksym alitania kwamba mama yake alimwambia abaki nyumbani na ajitolee kumpikia. Alikuwa amewaficha anakokwenda kwa sababu hakutaka kuwatia wasiwasi.
Wazazi wa Dmytro walijua kile alichokuwa akifanya. Kabla alimpigia simu baba yake kumwambia kuwa ameamua kujiunga na jeshi la ulinzi. Baba yake alimwambia asijaribu sana kutaka kuwa shujaa.
Dmytro alisema wazazi wake wanajivunia kile anachofanya. Alionekana mwenye furaha. Nilimuuliza ikiwa alihisi hofu ya kile kilichokuwa mbele.
"Sio sana, lakini ni asili ya binadamu kuwa na hofu, na bila shaka ndani ya nafsi yangu ninahisi hofu kidogo, kwani hakuna mtu anayetaka kufa, hata kama ni kwa ajili ya nchi yako. Kwa hivyo kifo sio chaguo kwetu."
Dmytro na Maksym walizungumzia juu ya ndoto zao kwa siku zijazo, furaha na marafiki, kumaliza masomo yao, kazi na hatimaye familia. Wazazi wao lazima wawe wanaomba kwamba mipango ya watoto wao, nguvu na hata maisha yao yasikatishwe na hali halisi ya kikatili ya vita, kama ilivyo kwa maombi ya wazazi wengine wengi wa vijana ambao wamejiunga kupambana katika vita hivyo vya Ulaya.