Muhoozi Kainerugaba: Je, tunajua nini kuhusu tangazo la kustaafu la mtoto huyu wa Rais Museveni?

th
Muda wa kusoma: Dakika 4

Mkuu wa jeshi la Uganda mwenye umri wa miaka 47 na mtoto wa rais wa Uganda Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba Jumanne alitoa ujumbe kwenye mtandao wa Twitter uliowashangaza wengi kwamba anastaafu kutoka jeshi.

Katika tangazo hilo lake alisema amestaafu kutoka kwa jeshi la taifa baada ya zaidi ya miongo miwili .

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Hata hivyo saa kadhaa baada ya ufichuzi wake Twitter , Muhoozi Kainerugaba, alituma tena video wakati wa usiku akiwa na rafiki yake na mwanahabari mkongwe wa Uganda Andrew Mwenda.

Katika video hiyo, Mwenda aliyemtembelea anasema kwamba kustaafu kwa Muhoozi kunatarajiwa baada ya miaka 8 huku Muhoozi akijibu kwa nguvu, "haswa." Hata hivyo haijulini video hiyo ilirekodiwa lini .

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Hata hivyo jeshi la Uganda limesema kwamba Muhoozi hajastaafu kutoka jeshini.

"Ninachoweza kusema, ni kwamba bado hajastaafu.'' Felix Kulaigye Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Uganda alisema alipopigiwa simu .

Mpenzi wa Twitter

Kilichowafanya wengi kuchukulia kwa uzito ujumbe huo wa Muhoozi kupitia Twitter ni kwamba ukumbi huo ndio umekuwa uwanja wake wa kusema lolote analotaka .

Katika jumbe zake humo, ni kawaida yake kutoa kauli zake binafsi kuhusu masuala mbali mbali nje na ndani ya Uganda.

Kutoka masuala mazito ya ulimwengu kama vita vya Ukraine na operesheni za kidiplomasia ambazo amehusika nazo kati ya Uganda na Rwanda hadi mambo yanayochukuliwa kama ya mzaha ama ucheshi,Twitter imekuwa chaguo la Muhoozi anapotaka kusema lolote .

TH

Chanzo cha picha, Muhoozi Kainerugaba/TWITTER

Maelezo ya picha, Jenerali Muhoozi akiwa na rais wa Rwanda Paul Kagame

Sio sadfa kwamba baada ya kuutuma ujumbe wake kustaafu kupitia Twitter,video iliyokana hilo pia iliwasilishwa kupitia ukumbi huo huo wa mawasiliano ya kijamii.

Unaeweza pia kusoma:

Sheria ya UPDF

Wakati huo huo, nia yake ya kustaafu inasalia kuwa suala la idhini ya jeshi chini ya Sheria ya UPDF, 2005.

"Afisa anaweza kwa maandishi kuwasilisha ombi la kujiuzulu kwa tume yake kwenye bodi lakini hataruhusiwa, isipokuwa kama itakavyoamriwa vinginevyo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, kuachiliwa katika majukumu ya uteuzi wake hadi atakapopata taarifa kupitia maandishi ,kuidhinisha kujiuzulu kwake na bodi," kinasema kifungu cha 66 (1) cha Sheria hiyo.

Jenerali Muhoozi Kainerugaba ni nani?

Muhoozi Kainerugaba ni mtoto wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda na mama Janet Museveni, ambaye ni waziri wa elimu na michezo tangu mwaka 2016.

Ni mume wa Charlotte Nankunda Kutesa aliyemuoa mwaka 1999 na mtoto wa kwanza wa Rais Museveni. Alizaliwa tarehe 24 mwezi Aprili 1974 mjini Dar es Salaam Tanzania. Akapata elimu yake ya shahada ya sayansi ya siasa kutoka chuo kikuu cha Nottingham University nchini Uingereza.

Mwaka 1999 alijiunga na jeshi la Uganda UPDF akiwa afisa kadeti na kuhitimu shahada kutoka chuo cha mafuzo ya jeshi cha Royal Military Academy Sandhurst, mwaka 2000 ambacho hutumika kwa mafunzo ya wanajeshi wa uingereza .

Kainerugaba ni miongoni mwa wanajeshi wa Uganda walipanda vyeo harakahara. Lakini kufika ngazi za juu za jeshi amepitia pakubwa. Dalili zilianza kumuendea vyema baada ya kupandishwa cheo na kuwa kapteni wa jeshi Novemba 2001, mwaka uliofuata (2002) akahudhuria mafunzo ya kuwa kamanda wa kitengo cha Jeshi (Battalion) huko nchini Misri.

line

Safari yake ndani ya jeshi

Mwaka 2003 alipandishwa cheo cha kuwa Meja na kuteuliwa kuwa kamanda wa kitengo cha jeshi cha Motorised Infantry batallion, na mwanachama wa baraza kuu la ulinzi nchini Uganda.

2005: Vilevile alihudhuria mafunzo ya ngazi za juu za usimamizi wa kitengo cha jeshi katika chuo cha kaisenyi magharibi mwa Uganda.

2006: Alisimamia mafunzo na mipango ya kitengo kipya cha jeshi kwa jina 1 Command katika eneo la Barlege, kaunti ya Otuke , wilayani Lira kaskazini mwa Uganda.

th

Chanzo cha picha, Muhoozi Kainerugaba/Twitter

2008: Julai alikuwa mganda wa kwanza kufuzu mafunzo ya kushambulia kwa kutumia parachute katika jeshi la Uganda la UPDF baada a kumaliza mafunzo yake huko Marekani. Mwaka huo huo akapandishwa cheo na kuwa Luteni kanali na kuteuliwa kuwa kamanda wa kikosi maalumu chini ya UPDF.

2010: Akateuliwa kuwa kamanda wa Kikosi maalumu ambacho sasa kinajumuisha kikosi cha ulinzi wa rais ambacho awali kilitenganishwa.

2011: Septemba akapandishwa cheo na kuwa kanali kabla ya kuwa Brigedia Jenerali.

Kuandaliwa kurithi kiti cha urais cha baba yake Museveni

Kutokana na kupandishwa vyeo harakaraka, kukazuka maneno ya kwamba anaandaliwa kuja kuwa mrithi wa Museven aliyetawala Uganda kwa zaidi ya miaka 30.

Mwezi Juni 2013 alijitokeza na kupinga tetesi hizo na kusema: "Uganda sio nchi ya kifalme ambao uongozi unarithishwa kutoka kwa baba kwenda kwa mtoto. Hili linalosemwa ni [Muhoozi] ni mradi ni maneno tu yakutungwa na watu."

Alikuja kurejea hilo la kupinga kuandaliwa kumrithi baba yake mwaka 2016 alipoteuliwa kuwa meja jenerali. Katika sherehe za uapisho wake alisema mradi wa "Muhoozi haupoi na ni maneno tu".

Kumlinda baba yake 'Rais' na nguvu 'tata' za kimamlaka alizokuwa nazo

Ni Luteni wa pili kuhudumu katika kikosi cha kumlinda rais (PPU).

Januari 2017, Muhoozi aliteuliwa kuwa mshauri wa rais wa shughuli maalumu. Kupandishwa kwake cheo na kusogezwa Ikulu, kukaongeza maneno zaidi kwenye vyombo vya habari vya Uganda kwamba Kainerugaba ni kama andaaliwa kuwa rais ajaye wa Uganda kumrithi baba yake.

2020: Rais Museveni akamteua tena kuwa kamanda wa kikosi maalumu (SFC) kumrithi Meja jenerali James Birungi. Akiendelea kuwa mshauri mwandamizi wa rais kwenye shughuli maalumu.

2021: Kabla ya June 24, kuteuliwa kuwa Kamanda wa vikosi vya ardhini akichukua nafasi ya lutein jenerali Peter Elwelu ambaye aliteuliwa kuwa mkuu wa majeshi msaidizi.

2021: Desemba alimtaka baba yake Rais Museveni kumwachia huru Inspekta wa zamani wa Polisi Jenerali Kale Kayihura. Alitumia tu mtandao wake wa twitter kufikisha ujumbe huo na miezi miwili baadaye Inspekta mstaafu huyo aliachiwa huru.

Jenerali Kayihura alikuwa ndani akiruhumiwa kwa makosa matatu: kushindwa kulinda vifaa vya vita, kusaidia na kuchochea utekaji nyara na urejeshwaji wa wakimbizi wa Rwanda nchini Uganda. Alifikishwa mahakamani Agosti mwaka 2018.

Mtoto huyu wa Rais alichapisha ujumbe kwenye mtandao wake wa twitter kuonyesha kuunga mkono uvamizi wa Urusi nchini Ukraine akiandika: "Watu wengi (ambao sio wazungu) wanaunga mkono msimamo wa Urusi nchini Ukraine. Putin yuko sahihi! Wakati USSR ilipopeleka makombora ya nyuklia nchini Cuba mwaka 1962, mataifa ya magharibi yalikuwa tayari kuilipua dunia. Wakati huu Nato inafanya hivyo hivyo wanatarajia Urusi kufanya tofauti?"

line