Jenerali Muhoozi Kainerugaba wa Uganda ni nani?

Luteni Jenerali Kainerugaba Muhoozi anadaiwa kupikwa ili amrithi baba yake Yoweri Museveni uraisi wa Uganda
Maelezo ya picha, Luteni Jenerali Kainerugaba Muhoozi anadaiwa kupikwa ili amrithi baba yake Yoweri Museveni uraisi wa Uganda

Muhoozi Kainerugaba ni mtoto wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda na mama Janet Museven, ambaye ni waziri wa elimu na michezo tangu mwaka 2016.

Ni mume wa Charlotte Nankunda Kutesa aliyemuoa mwaka 1999 na mtoto wa kwanza wa Rais Museven. Alizaliwa tarehe 24 mwezi Aprili 1974 mjini Dar es Salaam Tanzania. Akapata elimu yake ya shahada ya sayansi ya siasa kutoka chou kikuu cha Nottingham University nchini Uingereza.

Mwaka 1999 alijiunga na jeshi la Uganda UPDF akiwa afisa kadeti na kuhitimu shahada kutoka chuo cha mafuzo ya jeshi cha Royal Military Academy Sandhurst, mwaka 2000 ambacho hutumika kwa mafunzo ya wanajeshi wa uingereza .

Vyeo Jeshini

Kainerugaba ni miongoni mwa wanajeshi wa Uganda walipanda vyeo harakahara. Lakini kufika ngazi za juu za jeshi amepitia pakubwa. Dalili zilianza kumuendea vyema baada ya kupandishwa cheo na kuwa kapteni wa jeshi Novemba 2001, mwaka uliofuata (2002) akahudhuria mafunzo ya kuwa kamanda wa kitengo cha Jeshi (Battalion) huko nchini Misri.

Mwaka 2003 alipandishwa cheo cha kuwa Meja na kuteuliwa kuwa kamanda wa kitengo cha jeshi cha Motorised Infantry batallion, na mwanachama wa baraza kuu la ulinzi nchini Uganda.

2005: Vilevile alihudhuria mafunzo ya ngazi za juu za usimamizi wa kitengo cha jeshi katika chou cha kaisenyi magharibi mwa Uganda.

2006: Alisimamia mafunzo na mipango ya kitengo kipya cha jeshi kwa jina 1 Command katika eneo la Barlege, kaunti ya Otuke , wilayani Lira kaskazini mwa Uganda.

2008, Julai alikuwa mganda wa kwanza kufuzu mafunzo ya kushambulia kwa kutumia parachute katika jeshi la Uganda la UPDF baada a kumaliza mafunzo yake huko Marekani. Mwaka huo huo akapandishwa cheo na kuwa Luteni kanali na kuteuliwa kuwa kamanda wa kikosi maalumu chini ya UPDF.

2010: Akateuliwa kuwa kamanda wa Kikosi maalumu ambacho sasa kinajumuisha kikosi cha ulinzi wa rais ambacho awali kilitenganishwa.

Rais Kagame na jenerali kainerugaba

Chanzo cha picha, Twitter/Kainerugaba

Maelezo ya picha, Rais Kagame na jenerali kainerugaba

2011, Septemba akapandishwa cheo na kuwa kanali kabla ya kuwa Brigedia Jenerali.

Kuandaliwa kurithi kiti cha urais cha baba yake Museveni

Kutokana na kupandishwa vyeo harakaraka, kukazuka maneno ya kwamba anaandaliwa kuja kuwa mrithi wa Museven aliyetawala Uganda kwa zaidi ya miaka 30.

Mwezi Juni 2013 alijitokeza na kupinga tetesi hizo na kusema: "Uganda sio nchi ya kifalme ambao uongozi unarithishwa kutoka kwa baba kwenda kwa mtoto. Hili linalosemwa ni [Muhoozi] ni mradi ni maneno tu yakutungwa na watu."

Alikuja kurejea hilo la kupinga kuandaliwa kumrithi baba yake mwaka 2016 alipoteuliwa kuwa meja jenerali. Katika sherehe za uapisho wake alisema mradi wa "Muhoozi haupoi na ni maneno tu".

Kumlinda baba yake 'Rais' na nguvu 'tata' za kimamlaka alizokuwa nazo

Ni Luteni wa pili kuhudumu katika kikosi cha kumlinda rais (PPU).

Januari 2017, Muhoozi aliteuliwa kuwa mshauri wa rais wa shughuli maalumu. Kupandishwa kwake cheo na kusogezwa Ikulu, kukaongeza maneno zaidi kwenye vyombo vya habari vya Uganda kwamba Kainerugaba ni kama andaaliwa kuwa rais ajaye wa Uganda kumrithi baba yake.

2020: Rais Museveni akamteua tena kuwa kamanda wa kikosi maalumu (SFC) kumrithi Meja jenerali James Birungi. Akiendelea kuwa mshauri mwandamizi wa rais kwenye shughuli maalumu.

2021: Kabla ya June 24, kuteuliwa kuwa Kamanda wa vikosi vya ardhini akichukua nafasi ya lutein jenerali Peter Elwelu ambaye aliteuliwa kuwa mkuu wa majeshi msaidizi.

Luteni Jenerali Kainerugaba Muhoozi anadaiwa kupikwa ili amrithi baba yake Yoweri Museveni uraisi wa Uganda

2021: Desemba alimtaka baba yake Rais Museveni kumwachia huru Inspekta wa zamani wa Polisi Jenerali Kale Kayihura. Alitumia tu mtandao wake wa twitter kufikisha ujumbe huo na miezi miwili baadaye Inspekta mstaafu huyo aliachiwa huru.

Jenerali Kayihura alikuwa ndani akiruhumiwa kwa makosa matatu: kushindwa kulinda vifaa vya vita, kusaidia na kuchochea utekaji nyara na urejeshwaji wa wakimbizi wa Rwanda nchini Uganda. Alifikishwa mahakamani Agosti mwaka 2018.

Mtoto huyu wa Rais alichapishwa ujumbe kwenye mtandao wake wa twitter kuonyesha kuunga mkono uvamizi wa Urusi nchini Ukraine akiandika: "Watu wengi (ambao sio wazungu) wanaunga mkono msimamo wa Urusi nchini Ukraine. Putin yuko sahihi! Wakati USSR ilipopeleka makombora ya nyuklia nchini Cuba mwaka 1962, mataifa ya magharibi yalikuwa tayari kuilipua dunia. Wakati huu Nato inafanya hivyo hivyo wanatarajia Urusi kufanya tofauti?"

Ni mtaratibu na mpenda michezo

Jenerali Muhoozi ni mpenda michezo tangu akiwa shule akionekana kushiriki katika shughuli mbalimbali za michezo ukiwemo wa kikapu.

Mbali na kuwa mtu anayeweza kusikiliza na kujichanganya na watu wa makundi mbalimbali ikiwemo wanamichezo, wanasiasa na wasanii, mtoto huyu wa rais amekuwa pia akiandika machapisho mbalimbali.

Ameandika kitabu kilichoitwa 'Battles of the Ugandan Resistance: A Tradition of Maneuver'. Lakini pia amekuwa akiandika Makala mbalimbali kwenye magazeti na majarida.

Pamoja na hayo kikosi maalumu cha SFC kilichokuwa chini yake, kilishutumiwa kwa vitendo vingi vya unyanyasaji na utesaji wa watu hasa wanaokosoa na kupinga mamlaka za nchi hiyo. Hapa zilikuwa zikitajwa nguvu zake kama 'chachu'.