Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ukraine ilitoka vipi kuwa nchi ya tatu kwa nguvu za nyuklia duniani hadi hali yake ya sasa
Unaweza kuona jambo hili la ajabu, lakini wakati wa Vita Baridi, nchi ya tatu yenye nguvu kubwa za nyuklia duniani baada ya Marekani na Urusi ilikuwa Ukraine, si Uingereza, Ufaransa au China.
Kumalizika kwa Umoja wa Kisovieti (USSR) mnamo mwaka 1991, nchi mpya iliyojitegemea (Ukraine) ilirithi karibu silaha 3,000 za nyuklia ambazo Moscow ilikuwa imeacha kwenye eneo lake.
Lakini miongo mitatu baadaye, Ukraine sasa haina silaha za nyuklia.
Ukraine inapitia kipindi kigumu baada ya Urusi kuivamia Ukraine mnamo Februari 24 mwezi uliopita.
Tishio la vita vya nyuklia limeanza tena baada ya agizo la Vladimir Putin kwa nchi wanachama wa NATO kuendelea kuwa macho dhidi ya uingiliaji wowote unaoweza kufanywa na nchi wanachama wa NATO.
Lakini kilichotokea Ukraine katika miongo ya hivi karibuni ni kwamba imekuwa moja ya mataifa yenye nguvu kubwa za nyuklia, nchi ambayo jirani yake ana mshambulia.
Mbali na swali hili, maswali mengine mengi muhimu yanahitaji kujibiwa.
Je, uwepo wa silaha za nyuklia Ukraine kumezuia vita ya sasa?
Je, kuna hatari ya makabiliano ya nyuklia katika vita vya sasa?
Na je, ni kweli kwamba Ukraine ilikuwa ikijaribu kupata silaha za nyuklia, kama Urusi inavyodai?
Makubaliano ya Budapest
Mnamo mwaka 1991, Ukraine ilikubali kuondoa nyuklia katika eneo lake baada ya kuhakikisha usalama wake na kutambuliwa kama nchi huru.
Kufuatia kuanguka kwa Muungano wa Kisovieti, Marekani, Uingereza, Ukraine na Urusi zilitia saini Mkataba wa Maelewano wa Budapest.
Katika hati hiyo iliyotiwa saini katika mji mkuu wa Hungary mwaka 1994, Ukraine iliahidi kutia saini mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, (IAEA) na kukabidhi silaha za nyuklia zilizosalia kwa Moscow.
Vesanti Ferrero, Jr., wa Chuo Kikuu na Idara ya Mafunzo ya Asia ya Sao Paulo, aliiambia BBC: Kulikuwa na wasiwasi kwamba silaha hizi zinaweza kuhatarisha Ulaya.
Walichopata baada ya Ukraine kuachana na nyuklia, serikali za Urusi, Marekani na Uingereza ziliahidi kuheshimu uhuru, mamlaka na mipaka ya kijiografia ya Ukraine, na kujiepusha na uchokozi wowote dhidi ya Ukraine.
Wakati huo, serikali ya Ukraine ilikuwa inakabiliwa na matatizo mengi.
Nchi hiyo ilipata uhuru wake mwaka 1991 na imekuwa ikitafuta kutambuliwa kimataifa tangu enzi ya Usovieti.
Kufikia mwaka 1996, Ukraine ilikuwa imekabidhi silaha zote za nyuklia za enzi ya Soviet kwa Urusi.
Mkataba huo huo ulitiwa saini na Belarusi na Kazakhstan, chini ya masharti sawa na serikali ya Ukraine.
'Bila silaha na usalama'
Ukraine inaishutumu Urusi kwa kukiuka makubaliano hayo kwa mara ya kwanza mwaka 2014, ilipovamia na kuteka eneo la mashariki la Crimea, ambako Urusi ina kambi ya jeshi la wanamaji huko Sevastopol na jeshi la wanamaji la Bahari Nyeusi.
Kulingana na serikali ya Ukraine, Urusi ilikiuka mkataba huo mwaka huo huo kwa kuwalazimisha wanaotaka kujitenga kuasi, na kuwafadhili wanaotaka kujitenga katika majimbo ya mashariki ya Donetsk na Luhansk.
Zaidi ya watu 14,000 tayari wameuawa katika mzozo unaoendelea katika eneo hilo.
Wakati tishio la uvamizi wa Urusi katika eneo la Ukraine lilipoongezeka mapema 2022, Rais wa Ukrain Vladimir Zelensky kwa mara nyingine tena alitoa wito wa kutekelezwa kwa Mkataba wa Budapest.
Lakini hapakuwa na wakati wa kushauriana.
Mashambulizi ya Urusi yalianza mnamo Februari 24, yakilenga vituo vya kijeshi na vituo vya ulinzi kote nchini, na wanajeshi wa Urusi walianza kusonga mbele kutoka pande tofauti.
Kufuatia hotuba ya mwisho ya rais wa Ukraine kuhusu mkataba huo, Rais wa Urusi Vladimir Putin alitegemea maneno ya Zelensky kuhalalisha matendo yake.
Rais wa Urusi Vladimir Putin amedokeza katika hotuba yake kuwa Ukraine inajiondoa katika makubaliano hayo kufuatia nia yake ya kutengeneza silaha za nyuklia kwa msaada wa Marekani.
Kulingana na yeye, Ukraine ina nia ya kufanya uchokozi na hivyo kuongeza tishio kwa raia wa Urusi.
Alexander Lanuzka, profesa wa uhusiano wa kimataifa katika Chuo Kikuu cha Waterloo (Canada) na mtaalamu wa usalama wa nyuklia, alieleza: ''Matamshi ya Putin si sahihi kabisa. Marekani haina nia ya kuipatia Ukraine silaha za nyuklia au kuiona kuwa nchi yenye nguvu za nyuklia.
Zelensky alisema katika hotuba yake Februari 19 kwamba ''Ukraine ilipewa dhamana ya usalama baada ya kuachana na silaha za nyuklia iliyokuwa ikishika nafasi ya tatu duniani. Hatuna tena silaha hizo, lakini hatuna usalama.''
Tangu mwaka 2014, Ukraine imefanya majaribio matatu ya kushauriana na waliotia saini Mkataba wa Budapest, lakini haikufaulu. Leo, Ukraine itafanya hivyo kwa mara ya nne. Alisema ataifanya kwa mara ya mwisho.
'Mazungumzo ya kimapenzi tu na ambayo hayajakomaa.'
Hata kabla ya Mkataba wa Maelewano wa Budapest kuidhinishwa, wanachama wa wataalam wa kisiasa wa Ukraine na wataalam wa kisiasa wa kimataifa walizungumza juu ya uwezekano kwamba makubaliano hayo yamekiukwa na baadhi ya waliotia saini.
Volodymyr Tolubko, kamanda wa zamani wa kijeshi aliyechaguliwa katika bunge la Ukraine, alisema katika bunge 1992 kwamba wazo la Ukraine kuachana kabisa na nyuklia kwa ajili ya mabadilishano ya ahadi za usalama lilikuwa ni 'mazungumzo ya kimapenzi tu na ambayo hayajakomaa.'
Ilikuwa Kulingana na yeye, nchi inapaswa kuwa na angalau baadhi makombora ya nyuklia ya wakati wa Usovieti, ambayo yangeweza kutumika ''kuzuia uchokozi yoyote.''
Kwa uvamizi wa hivi punde wa Urusi, mjadala umeanza tena, huku maafisa wa serikali na wachambuzi wa masuala ya kisiasa wakisema kwamba ikiwa Ukraine ingekuwa na silaha za nyuklia, Ukraine ingesimamisha uvamizi wa Urusi.
Ferraro Jr. anaeleza kwamba kwa hakika baadhi ya mataifa yanaamini kwamba silaha za nyuklia zinaweza kuwa na matokeo katika kuzuia mashambulizi ya kigeni.
Katika uhusiano wa kimataifa, kuna dhana ya kuzuia nyuklia na ambayo watu wengi wanaamini.
Kulingana na yeye, nchi zinazomiliki silaha za nyuklia zina hatari ndogo, si kwa sababu zinaweza kutumia silaha za nyuklia, lakini kwa sababu zinatumia silaha za nyuklia kama dhamana na katika tukio la tishio la mashambulizi.
Watetezi wa kesi yake wamekuwa wakifanya kazi ili kufanya nakala halisi ya taarifa hii ipatikane mtandaoni.
Licha ya hayo yote, wataalamu wanaonya kuwa kuwepo kwa silaha za nyuklia kunamaanisha si tu hakikisho la amani na hali ya amani, bali pia mengi zaidi.
''Migogoro kati ya mataifa yenye nguvu za nyuklia daima ni hatari na yenye kutia wasiwasi, kama ilivyo kwa mzozo wa miaka mingi kati ya Pakistan na India,'' Ferraro Jr anasema.
Gharama za kisiasa na kifedha
Kwa Alexander Lanuzka, hoja zinazotolewa na wasomi wa Ukraine hazina maana kwa sababu baada ya Vita vya Kidunia vya pili, Kyiv haikuwahi kuwa na udhibiti wa silaha kwenye ardhi yake.
Mtafiti huyo alisema kuwa ''silaha hizi lazima zilikuwepo Ukraine, lakini Ukraine haikuwa na udhibiti wa vitendo juu yao.''
Ukrainia haikuwa na misimbo ya ufikiaji au maelezo mengine muhimu ya kuziendesha.
Andrew Footer, profesa wa siasa za kimataifa katika Chuo Kikuu cha Leicester (Uingereza), pia anasema kuwa na silaha nchini Ukraine kulimaanisha vitisho vya siku zijazo.
Ingawa Ukraine sasa ina sekta ya nishati ya nyuklia, kuibadilisha kuwa mpango wa silaha za nyuklia kutasababisha gharama kubwa za kisiasa na kifedha
Je, kuna hatari ya makabiliano ya nyuklia
Ijapokuwa Ukraine imeondokana na silaha za nyuklia, uvamizi wa Ukraine na majeshi ya Urusi umefufua hofu ya kutokea makabiliano ya nyuklia barani Ulaya.
Putin ameweka wazi katika hotuba zake kwamba iwapo mwanachama yeyote wa NATO, muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani na mataifa makubwa ya Ulaya, anaamua kuingilia kati mzozo huo, atajibu vikali.
Aidha, ameviweka vikosi vya nyuklia vya Urusi kwenye ''tahadhari maalum.''
Katika mazungumzo na maafisa wa kijeshi, rais wa Urusi alisema mataifa yenye nguvu duniani yamechukua ''hatua kali'' dhidi ya Urusi na kuweka ''vikwazo visivyo halali''.
Hata hivyo, kubadili hali ya tahadhari haimaanishi kuwa kuna nia ya kweli ya kuzitumia.