Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Urusi na Ukraine: Je bomu la Cluster lenye milipuko ya kutapakaa ni silaha ya aina gani na Je Urusi inalitumia
Urusi imeshutumiwa kwa kutumia mabomu ya Cluster nchini Ukraine-na Mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC)imefungua uchunguzi juu ya uwezekani wa uhalifu wa kivita . Tuliziangalia video za mitandao ya Habari ya kijamii na taarifa nyingine huru kupata taarifa zinazozingira moja ya shambulio.
Tarehe 28 Februari Andriy (sio jina lake halisi) alikuwa akioga katika jengo la gorofa katika Kharkiv wakati aliposikia mlipuko wenye sauti kubwa nje.
"libidi ni nijikaushe, nikiwab nimelala , nimelalakwenye sakavu yenye unyevunyevu katika nyumba iliyokuwa inatikisika na kusikia sauti ya kupasuka kwa vioo."
Madirisha katika nyumba hii ya gorofa yalipasuka na alipoangalia nje, watu kadhaa walikuwa wamelala chini kwenye sakafu. Ilikuwa ni wazi walau mmoja wao alikuwa amekufa.Walikuwa wanasubiri kupata maji kwenye bomba la maji ambako pia mwenye alikuwa amesimama dakika chake kabla kupata maji.
Baadaye Meya wa Kharkiv alithibitisha kuwa watu wanne waliuawa.
BBC imetahmini picha na kuzungumza na mashuhuda na wataalamu ili kubaini zaidi kuhusu shambulio hili- moja tu kati ya mashambulio katika mzozo wa hivi karibuni ambapo ilidaiwa kuwa silaha za cluster zilitumiwa kwenye maeneo ya makazi ya raia.
Taarifa za tukio zilitumwa kwa mara ya kwanza kwenye mtandao wa Twitter majira ya saa saba mchana kwa saa za Eneo. Video ilionyesha vilipuzi na moshi mweusi uliokuwa ukipaa angani.
Video nyingine, ilitumwa muda mfupi baadaye, ikionyesha hali baada ya tukio, huku watu miili ikiwa ambayo ilionekana kutokuwa na uhai imelala sakafuni.
Kwa kutambua vitu kama -bomba la maji na duka la fundi wa viatu-tunaweza kuthibitisha kuwa tukio lilifanyika eneo la kaskazini mwa Kharkiv. TKulikuwa na ripoti za mashambulio ya anga ya ndege za Urusi siku hiyo.
KIELELEZO CHA ENEO LA SHAMBULIO:
Tumekuwa tukituma picha zaidi, zilizopigwa siuku ile na kwa wakati sawa n awa tukio linalodaiwa kutoka mtaa ulio mbali zaidi nae neo hilo wa unaofahamika kama 23 Serpnya Lane. (Jina la mtaa linamaanisha tarehe 23 Agosti 1943, wakati mji ulipokombolewa kutoka mikononi mwavikosi vya Nazi vya Ujerumani.)
Muda ulioonyeshwa ni saa 06:46, picha ya video ilichukuliwa kutoka ndani ya gari lililolokuwa likiendeshwa kuelekea kwenye eneo la tukio. Lilipokuwa likigeuka kueleke mtaa wa 23 Serpnya Lane, kulikuwa na milipuko ya haraka, na mtu mmoja akaanguka ardhini.
Mabomu ya Cluster ni mabomu gani?
Tulionyesha video hii fupi kwa wataalamu wane wa silaha , akiwemo Sam Cranny-Evans, mtafiti na mchambuzi katika taasisi ya Royal United Services Institute, taasiis ya utafiti wa masuala ya ulinzi.
Anasema picha ya gari inaonyesha zaidi shambulio la bomu la cluster kwani inaonyesha "milipuko midogo midogo mingi katika eneo dogo".
Silaha za Cluster ni Maroketi au makombora ambayo hulipua eidadi kubwa ya vilipuzi vidogo vidogo. Kwa kawaida hufyatuliwa kutoka ardhini, na kadri yanapofika katika eneo yalipolengwa , hufunguka na kutawanya vilipuzi vyake vyote.
JINSI MABOMU YA CLUSTER YANAVYOFANYA KAZI:
Mtaalamu wa ujasusi wa silaha Pete Norton anaafiki kwamba ushahidi "unaohusishwa na matumizi ya silaha ndogo ndogo" - vilipuzi vingi katika silaha ya cluster. Norton anasema kwamba milipuko katika ni "milipuko midogo midogo".
Pia tumewaonyesha wa taalamu wa picha za video shambulio hilo, picha za tukio hilo hilo zilizochukuliwa kutoka eneo tofauti. Wanasema mkusanyiko wa maroketi na mabomu ya cluster vinaonekana kutumiwa katika shambulio hilo.
Matumizi ya silaha za cluster yamekuwa yakikosolewa na makundi ya kutetea haki za binadamu na baadhi ya serikali. Wakati mabomu madogo madogo yalipofyatuliwa husambaa katika eneo kubwa, na kuwa na uwezekano mkubwa wa kuwadhuru watu wengi.
Pia kuna hatari inayoweza kutokea baada ya shambulio. Kulingana na Bw Cranny-Evans, kifyatuzi cha roketi kinaweza kutuma hadi mabomu 7,000 ya cluster na kwa kawaida takriban 2% yake hayalipuki. Vilipuzi hivi ambavyo havijalipuka vinaweza kuwauwa au kuwakata viungo raia muda mrefu baada ya kumalizika kwa , n ani ghali kuvipata vilipoanguka na kuviondoa.
Zaidi yan chi 100 ni sehemu ya mkataba wa kimataifa unaozuwia utengenezaji au matumizi ya silaha hizi, lakini urusi na Ukraine hazijasaini mkataba huo na zote zinamiliki silaha za cluster. Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alikanusha matumizi ya silaha hizi Jumanne
Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
- MOJA KWA MOJAUrusi na Ukraine: Mlipuko wakumba Kyiv huku Urusi ikiendeleza mashambulizi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Eneo linalolengwa
Urusi imekuwa ikishutumiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuwalenga raia kwa makusudi kwa mashambulio, lakini katika tukio lililotokea kwenye bomba la maji, wapelelezi kutoka Amnesty International wanaamini kinadharia kwamba kulikuwa na nia ya kushambulia makao makuu ya kampuni inayoitwa XADO yaliyopo karibu na eneo lililoshambuliwa. Jengo hilo liko katika mtaa mmoja ambao Andriy alishuhudia shambulio.
XADO ni kampuni ya kemikali ambayo pia inafahamika kwa kutengeneza silaha. Lakini hakuna Ushahidi kwamba utengenezaji wowote wa silaha unafanyika katika jingo la makao makuu, ambalo lipo katika eneo la makazi ya watu.
Hata kama XADO ilikuwa inalengwa, wataalamu wanafikiria mabomu ya cluster hayangepaswa kutumiwa.
"Iwapo eneo lililokuwa linalengwa lilichukuliwa kama eneo muhimu kwamba lilihitaji shambulio la kombora, unapaswa kutumia shambulio la kombora la masafa lenye kifyatuzi cha hali ya juu ," anasema Bw Cranny-Evans.
"Silaha ya cluster inasababisha uharibifu mbaya kimwili na kiwewe kisaikolojia , lakini haina ufanisi mkubwa kama watu wako ndani ya jengo.
Iwapo unataka kuangamiza jengo unahitaji vilipuzi vingi vya hali ya juu, sio milipuko midogo midogo ."
BBC imewasiliana na ubalozi wa Urusi mjini London kupata kauli yake.