Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Urusi na Ukraine: Mlipuko wakumba Kyiv huku Urusi ikiendeleza mashambulizi
Umoja wa Mataifa unasema wakimbizi milioni moja sasa wameikimbia Ukraine na kuelekea nchi jirani.
Moja kwa moja
Uvamizi wa Ukraine: Mji wa Mariupol umezingirwa
Meya wa Mauripol amesema wanajeshi wa Urusi ambao wamezunguka mji wa bandari wa kusini wametengeneza azingira sawa na uvamizi mbaya zaidi uliotekelezwa na Wanazi huko St Petersburg (iliyojulikana kama Leningrad) katika vita vya Pili vya Dunia.
Wanajaribu kutengeneza kuzuizi hapa, kama tu ilivyokuwa huko Leningrad," amesema Vadym Boichenko.
Meya wa mji amesema wanajeshi wa Urusi wamekata huduma ya umeme mjini humo, chakula, maji na mifumo ya utoaji joto.
Alisema "hawakuweza kupata njia ya kutuvunja moyo. Kwa hivyo sasa wanajaribu kutuzuia kukarabati umeme, maji na mfumo wa usambazaji wa joto".
Aidha mkaazi mmoja amesema, "hakujawa na mwanga, hakuna joto, na hakuna maji sasa kwa siku mbili kamili na hatuna chakula chochote," alisema Maxim, 27, msanidi wa IT ambaye alikuwa amejificha kwenye nyumba ya babu na babu yake Alhamisi asubuhi.
Vikosi vya Urusi viliharibu unganisho la treni ili wasiweze kuwahamisha raia, anaongeza.
Halijoto inatabiriwa kushuka hadi -2C (28 Fahrenheit) wikendi hii ijayo.
- Mzozo wa Ukraine: Urusi ina silaha ngapi za nyuklia?
- Fahamu mataifa 9 yenye uwezo mkubwa wa silaha hatari za nyuklia duniani
Mzozo wa Ukraine-Mazungumzo ya amani kati ya Urusi na Ukraine yanaendelea
Mshauri wa urais wa Ukraine Mykhaylo Podolyak ameandika kwenye Twittter yake kwamba yeye na maafisa wengine wameanza mazungumzo na wawakilishi wa Urusi nchini Belarus.
Amesema masuala muhimu yanayojadili:
- Usitishaji mapigano mara moja
- kuzingatia makubaliano yaliyofanywa na pande zinazopingana katika vita kuacha kupigana kwa muda fulani; makubaliano.
- Ukanda wa misaada ya kibinadamu kwa ajili ya kuwahamisha raia kutoka kwa vijiji na miji iliyoharibiwa au iliyopigwa kila mara
Ufaransa imeishikilia meli ya kifahari inayomilikiwa na tajiri wa Urusi
Mamlaka ya Ufaransa imeishikilia boti ya Igor Sechin, mtendaji mkuu wa kampuni ya nishati ya serikali ya Urusi ya Rosneft, kama sehemu ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya kutokana na uvamizi wa Ukraine.
Mawakala wa forodha walikamata meli hiyo baada ya kubaini Sechin kuwa mwanahisa mkuu wa kampuni inayomiliki, wizara ya fedha ya Ufaransa ilisema.
Yacht ilikuwa imewasili La Ciotat, Marseille, mnamo Januari kwa ajili ya matengenezo.
Lakini mamlaka ya Ufaransa ilisema imekuwa ikifanya "mipango ya kusafiri kwa meli haraka, bila kumaliza kazi iliyopangwa" ilipokaguliwa.
Ukraine yafungua simu ya dharura kwa Waafrika wanaokimbia vita
Serikali ya Ukraine imeanzisha simu ya dharura kwa Waafrika na raia wa Asia wanaokimbia uvamizi wa Urusi, kulingana na waziri wa mambo ya nje.
Hatua hii inakuja kufuatia madai yaliyoenea ya ubaguzi wa rangi yanayowakabili waafrika wanaojaribu kuondoka nchini humo.
Wanafunzi wengi kutoka Afrika nchini Ukraine wameshirikisha simulizi za wao kuzuiwa na afisa wa usalama wa Ukraine kuondoka nchini humo.
Katika ujumbe wake wa Twitter, Waziri wa Mambo ya nje Dmytro Kuleba alisema mamlaka "zinafanya kazi kwa bidii" kuhakikisha usalama na kupita kwa wanafunzi wa Kiafrika na Asia.
- Uvamizi Ukraine: Ghadhabu zazuka baada ya Waafrika kubaguliwa Ukraine
Wakazi wa Kyiv bado wamejificha katika handaki
Wakazi wa Kyiv wa rika zote - watu wazima na watoto - walielekea tena chini ya ardhi jana usiku wakati mji mkuu ukiendelea kulengwa.
Baadhi, kama inavyoonyeshwa hapa, walishuka hadi kwenye vituo vya metro ambavyo vinatumika kama makazi.
Kiasi cha watu 15,000 wanajihifadhi katika vituo hivyo, meya wa jiji hilo amekadiria.
BBC correspondents have said the blasts could be heard from two storeys underground in their bunker.
Baadhi walifanikiwa kulala huku wengine wakijaribu kuwaburudisha watoto wadogo.
Milipuko minne mikubwa ilisikika usiku kucha na kunaswa kwenye video na mashahidi, ingawa haijabainika malengo yalikuwa nini au kama kulikuwa na vifo.
Waandishi wa BBC wamesema milipuko hiyo inaweza kusikika kutoka ghorofa mbili chini ya ardhi katika chumba chao cha kulala.
Nato yalaumiwa kwa mauaji ya raia, Ukraine
Naibu waziri mkuu wa Ukraine amesema Nato inahusika kwa kiasi fulani na vifo vya raia nchini humo kwa kushindwa kuweka zuio la ndege kuruka nchini Ukraine.
Akizungumza na BBC Radio 4, Olha Stefanishyna alisema "ni unyama kujua kwamba idadi ya raia na watoto watauawa kwa kutochukua uamuzi huo".
"Damu za hawa raia - ikiwa ni pamoja na mama na baba wa watoto wawili ambao walizaliwa jana tu na leo tu wanapoteza wazazi wao kwa kupigwa makombora - lawama sio tu kwenye mikono ya Urusi."
Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine aliomba radhi kwa kutokuwa mwanadiplomasia katika chaguo lake la lugha, lakini alisema alikuwa akizungumza "akiwa ameketi kwenye makazi ya mabomu".
Wanachama wa Nato wamekataa kuanzisha eneo lisilo na ndege kwa vile wanahofia kuzidisha mzozo huo kwa kuweka vikosi vya Magharibi katika vita vya moja kwa moja na nguvu za anga za Urusi.
- Mzozo wa Ukraine: Urusi ina silaha ngapi za nyuklia?
- Fahamu mataifa 9 yenye uwezo mkubwa wa silaha hatari za nyuklia duniani
Madai ya hivi karibuni kutoka pande zote mbili dhidi ya waliokufa
Jeshi la Ukraine limekuwa likitoa taarifa mara kwa mara kuhusu uharibifu ambao umesababishwa na vikosi vya Urusi, ambavyo vinaendelea kushikilia miji muhimu, haswa kusini.
Tunapaswa kusisitiza kwamba BBC haiwezi kuthibitisha habari hii, lakini taarifa za hivi punde kutoka kwa Mkuu wa Jeshi zinasema kwamba takriban wanajeshi 9,000 wa Urusi wameuawa au kujeruhiwa.
Pia zinasema vikosi vya Ukraine vimeharibu:
- Mizinga 217
- Mifumo 90 ya silaha
- Helikopta 31
- Ndege nyingine 30
Huku Urusi ikitoa taarifa kwa mara ya kwanza jana na kusema kuwa idadi maalum ya wanajeshi wa Urusi waliokufa Ukraine ni 498 na karibu 1,600 wamejeruhiwa.
Aidha taarifa hiyo iisema imewauwa wanajeshi 2,870 wa Ukraine na "raia".
Inafaa kukumbuka kuwa mamia ya raia tayari wamekufa katika vita, na maonyo ya mzozo wa kibinadamu unazidi kuongezeka.
- Jinsi Kenya ilivyoikabili Urusi kupitia hotuba ya balozi wake Martin Kimani katika mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa
- Ukraine na Urusi: Bidhaa ambazo zitaguswa na jinsi Afrika itakavyoathirika
Wakazi wa Kherson 'wanahitaji chakula na misaada ya matibabu'
Mkazi mwingine wa Kherson amesema leo kwamba amefungua kituo cha kujitolea kusaidia watu kwa chakula, maji na dawa huku jiji hilo likiwa chini ya udhibiti wa Urusi.
Akizungumza na BBC, anasema chakula hakitoshi na kuna raia wengi waliojeruhiwa ambao wanahitaji kutolewa nje ya jiji kwa matibabu. Anasema Warusi "hawaruhusu Msalaba Mwekundu kuleta dawa na ambulensi kusaidia watu". "
Tayari nimepata uzoefu huu huko Donetsk mnamo 2014 na nilikuja hapa Kherson," anaongeza.
"Nadhani katika miaka michache tutakuwa na Ukraine tofauti kabisa na itakuwa Ukraine huru kabisa, sio chini ya Urusi."
- Urusi na Ukraine: Hujui kinachokuja - Joe Biden amwambia Putin
- Jeshi la Urusi: Hatumtishi mtu, tunalinda mipaka yetu
Ufaransa yataka raia wake kuondoka Urusi
Serikali ya Ufaransa imewataka raia wake kuondoka nchini Urusi kutokana na mzozo unaoongezeka ikiwa uwepo wao huko sio "muhimu".
Nchi zingine zimetoa ushauri sawa wa kusafiri.
Ofisi ya mambo ya nje ya Uingereza "imeshauri dhidi ya safari zote za Urusi kwa sababu ya ugumu wa kuondoka nchini na kile inachoelezea kama kuongezeka kwa hali kuwa mbaya ya uchumi wa Urusi.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani inashauri vivyo hivyo.
Inataja mambo mengi ikiwa ni pamoja na "maofisa wa usalama wa Urusi kuweza kuwanyanyasa.
- Mzozo wa Ukraine: 'Putin amenihakikishia hakutakuwa na mzozo' - Macron
- Mzozo wa Ukraine: Marekani yashutumu Urusi kwa kupanga visingizio bandia vya uvamizi
Rais wa Msumbiji amewafukuza mawaziri sita
Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi amewafuta kazi mawaziri sita akiwemo waziri wa fedha.
Tangazo hilo lilitolewa katika taarifa ambayo haikutoa sababu zozote za kufukuzwa kazi kwa mawaziri hao wala kutoa dalili za lini nafasi hizo zitapewa watu wengine.
Haya ni mabadiliko ya pili makubwa ya baraza la mawaziri katika miezi ya hivi karibuni.
Wengine waliofutwa kazi ni pamoja na waziri wa rasilimali za madini na nishati, bahari, maji na uvuvi na kazi za umma, nyumba na rasilimali za maji.
Wachunguzi wa masuala ya kisiasa nchini walisema hawakushangazwa na kufukuzwa kazi kwa watumishi hao.
Mnamo Novemba, Rais Nyusi aliwaachisha kazi waziri wa ulinzi na mambo ya ndani na kueka wengine.
- Mzozo wa Msumbiji: Rais Samia azuru Kaskazini mwa Msumbiji-eneo lenye wapiganaji wa kijihadi
Jinsi mataifa ya Afrika yalivyopigia kura mjadala wa UN kuhusu Ukraine
Takriban nchi 17 za Afrika hazikupiga kura katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kushutumu uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.
Walijumuisha Afrika Kusini, Algeria, Uganda, Burundi, Senegal, Sudan Kusini, Mali na Msumbiji.
Nyingine zilikuwa Sudan, Namibia, Angola, Zimbabwe, Equatorial Guinea, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Madagascar, Tanzania na DRC.
Eritrea ndiyo nchi pekee ya Afrika iliyopiga kura kupinga azimio hilo.
Uganda ilisema ilijiepusha na kura ya kuunga mkono "kutopendelea upande wowote" kama mwenyekiti anayekuja wa Vuguvugu la Zisizofungamana na Siasa (Nam).
Nam ni kongamano linaloundwa na nchi 120 zinazoendelea ili kudai uhuru wao kutoka kwa madai yanayoshindana ya mataifa hayo mawili makubwa.
Katika ujumbe wa Twitter, mwakilishi wa kudumu wa Uganda katika Umoja wa Mataifa, Adonia Ayebare, alisema nchi hiyo "itaendelea kuwa na jukumu la kujenga katika kudumisha amani na usalama kikanda na kimataifa".
- Mzozo wa Ukraine na Afrika: Athari kwa mafuta,wanafunzi na mkate
- Mzozo wa Ukraine: Tunayofahamu mpaka sasa kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine
- Mzozo wa Ukraine: 'Tulitendewa kama wanyama' – Waafrika wanaokimbia Ukraine
Ujasusi wa Uingereza: Kasi ya uvamizi wa Urusi yapungua
Maendeleo kidogo yamefanywa katika siku tatu zilizopita na msafara mrefu wa vikosi vya Urusi vinavyokaribia Kyiv, kulingana na tathmini ya kijasusi ya jeshi la Uingereza.
Sehemu kuu ya kijeshi, ambayo inakaribia mji mkuu kutoka kaskazini mwake, "imebakia na zaidi ya kilomita 30 kutoka katikati mwa jiji ikiwa imecheleweshwa na upinzani mkali wa Ukraine, kuharibika kwa magari na msongamano".
Taarifa ya wizara ya ulinzi pia inaongeza kuwa miji ya Kharkiv, Chernihiv na Mariupol bado iko chini ya udhibiti wa Ukraine.
Kuhusu takwimu za majeruhi wa Urusi, Uingereza inatabiri kwamba idadi halisi ni "juu zaidi" kuliko 498 ya waliouawa na 1,597 waliojeruhiwa waliotangazwa hadi sasa na Moscow.
- Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
- Mzozo wa Ukraine: Ni vikwazo gani vilivyowekwa dhidi ya Urusi?
Mzozo wa Ukraine: Tunachokijua mpaka sasa
Kile tunachokikatika jua siku ya nane ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Katika Kyiv:
Milipuko minne mikubwa katika saa chache zilizopita imenaswa kwenye video na mashahidi, lakini haijulikani malengo yake yalikuwa nini na kama kulikuwa na majeruhi.
Waandishi wa BBC wanasema milipuko hiyo ilisikika kutoka ghorofa mbili chini ya ardhi katika chumba cha kulala.
Afisa wa ulinzi wa Marekani anasema msafara mkubwa wa magari ya kijeshi ya Urusi karibu na Kyiv "umekwama" kutokana na mafuta na uhaba wa chakula.
Kusini:
Vikosi vya Urusi vimeudhibiti mji muhimu wa bandari wa Kherson, kwa mujibu wa maafisa wa eneo hilo.
Ni jiji la kwanza kuu la Ukraine kuchukuliwa tangu uvamizi huo uanze Katika mji wa bandari wa Mariupol, mamia ya watu wanahofiwa kufariki kufuatia saa kadhaa za mashambulizi ya makombora, naibu meya wa jiji hilo anasema.
Jeshi la Ukraine linadai kuwa jiji hilo bado liko mikononi mwa Ukraine.
Katika kaskazini mashariki: Pia kumekuwa na mashambulizi makubwa ya makombora katika mji wa pili kwa ukubwa katika nchi hiyo, Kharkhiv.
Katika maendeleo mengine:
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitoa video ya usiku wa manane, akisifu ujasiri wa raia katika kutetea nchi yao.
Zaidi ya watu milioni moja sasa wameikimbia Ukraine tangu kuanza kwa uvamizi huo, Umoja wa Mataifa unasema, huku idadi hiyo ikiongezeka kwa kasi.
Uchunguzi kuhusu uwezekano wa uhalifu wa kivita nchini Ukraine umezinduliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mjini The Hague
Urusi kwa mara ya kwanza imekiri kuhusika na mauaji makubwa ya kijeshi wakati wa shambulio lake dhidi ya Ukraine, ambapo wanajeshi 498 waliuawa na wengine 1,597 kujeruhiwa.
- Mzozo wa Ukraine: Siku ya saba ya uvamizi wa Urusi kwenye ramani
- Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
Urusi na Belarus zimepigwa marufuku kushiriki mashindano ya Olimpiki ya Walemavu 2022
Wanariadha kutoka Urusi na Belarus hawataruhusiwa kushiriki katika Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya baridi ya 2022 huko Beijing, Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki ya Walemavu imesema.
- Michuano ya Olimpiki kwa walemavu ni leo Rio de Janeiro
Zelensky: "Tumewazuia"
Rais wa Ukraine ametoa ujumbe mpya wa video kwa raia wake siku ya Jumatano usiku, akiwataka kuendelea na mapambano dhidi ya wavamizi wa Urusi.
Video hiyo, iliyotumwa kwenye mtandao wa Facebook, ina maelezo: "Kila mvamizi anapaswa kujua kuwa: atapokea karipio kali kutoka kwa Waukraine.
"Sisi ni taifa ambalo lilivunja mipango ya adui katika wiki moja," rais huyo aliyechaguliwa kidemokrasia alisema kutoka eneo lisilojulikana.
"Lakini tuliwazuia."
Alisema wanajeshi wa Urusi waliokamatwa "hawajui ni kwa nini wako hapa", na kwamba askari hao ambao ni adui "wanakimbia kurudi Urusi".
Aliongeza kusema kuwa wanajeshi hao ni "watoto waliochanganyikiwa", ambao "wanatumiwa" na viongozi wao huko Moscow.
Zelensky pia aliwashukuru raia katika miji ya Konotop, Bashtanka, Energodar na Melitopol, ambao alisema walikuwa wamefunga barabara kwa wanajeshi wa Urusi.
Aliongeza kuwa hivi karibuni amezungumza na viongozi wa Norway, Israel, Kazakhstan, Qatar, Canada, Poland na Baraza la Ulaya.
- Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
Multichoice yatangaza kusitisha kurusha matangazo ya chaneli ya Russia Today (RT)
Kampuni ya utangazaji ya satelaiti ya Afrika Kusini Multichoice imetangaza kuacha kutangaza chaneli ya habari inayomilikiwa na serikali ya Russia Today (RT) kwenye jukwaa lake la DSTV hadi itakapotangazwa tena.
Katika taarifa, Multichoice ilitaja vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Ulaya dhidi ya Urusi ndivyo ambavyo "vimesababisha msambazaji wa kimataifa wa idhaa hiyo kusitisha urushaji wa matangazo hayo kwa wasambazaji wote, ikiwa ni pamoja na Multichoice".
Huduma ya Multichoice ya DSTV inarusha matangazo bara zima.
Inafuatia uamuzi wa Umoja wa Ulaya siku ya Jumatano kusimamisha usambazaji wa matangazo ya kituo cha Russia Today na Sputnik kote katika jumuiya hiyo, ikizitaja njia hizo kama upotoshaji wa habari.
Lakini uamuzi huo wa Multichoice umeshutumiwa na chama cha Wapigania Uhuru wa Kiuchumi yaani Economic Freedom Fighters (EFF) cha Afrika Kusini, ambacho kilisema huko ni kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari na haki za watumiaji.
"Multichoice imechagua ni vyombo vipi vya habari ambavyo watumiaji wanapaswa kutazama na kuamuru ni maudhui gani lazima yatazamwe kulingana na uaminifu wao katika mzozo tata huko Uropa," chama kilisema kwenye taarifa.
Wakati huo huo, ubalozi wa Urusi nchini Uganda ulisema shirika la utangazaji la nchi hiyo, UBC, litarusha matangazo ya Urusi Leo kila siku kwa saa moja asubuhi na usiku sana.
Idhaa ya Russia Today (RT) inajielezea kama yenye kujitegemea inayofadhiliwa na Shirikisho la Urusi.
- Urusi na Ukraine: Ni zipi hatari za shambulio la kinyuklia?
- Chelsea: Roman Abramovich anasema ana mpango wa kuiuza klabu hiyo
Tazama jinsi raia wa Ukraine walivyofanikiwa kuwazuia wanajeshi wa Urusi
Huku tukiingia katika siku ya nane ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine , raia nchini humo wanaendelea kuwazuia wanajeshi wanaovamia maeneo yao.
BBC News imethibitisha kanda hizi za video.
Katika mji wa Kusini wa Enerhodar, raia walikongamana nje ya kituo cha umeme ili kuyazuia majeshi ya Urusi .
''Hatutawaruhusu kuingia katika kituo kikubwa cha umeme barani Ulaya'', alisema mtu ambaye haonekani katika kamera.
Soma zaidi:
Watu milioni moja wameikimbia Ukraine , UN yasema
Watu milioni moja wameikimbia Ukraine , UN imesema
Umoja wa Mataifa unasema wakimbizi milioni moja sasa wameikimbia Ukraine na kuelekea nchi jirani.
Hatua hiyo imefanyika ndani ya siku saba pekee. Uvamizi wa Urusi ulianza Alhamisi iliyopita.
Kama mwandishi wa BBC Lewis Goodall anavyaelezea: "Mgogoro wa wakimbizi wa 2015 ulihusisha wakimbizi milioni 1.3. Hiyo inakaribia kuipiku idadi ya wanaotoka Ukraine katika wiki moja."
Katika taarifa yake kwenye Twitter, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Wakimbizi Filippo Grandi aliomba "kusitishwa kwa vita , ili msaada wa kibinadamu uweze kutolewa" kwa mamilioni ya raia waliosalia nchini humo.
Shirika hilo limetabiri mzozo huo utawaacha takriban watu milioni 12 wakiwa wakimbizi wa ndani na kuhitaji msaada.
Ramani hii inaelezea zaidi kule ambako raia wa Ukrain wanatorokea.
Pia unaweza kusoma:
- Ukraine na Urusi: Je Vacuum au thermobaric ni bomu la aina gani?
- 'Watatushambulia hadi tubaki majivu'
- Urusi na Ukraine: Hujui kinachokuja - Joe Biden amwambia Putin
Natumai Hujambo. Hii leo siku ya Alhamisi tutaendelea kukupatia taarifa tofauti kutoka maeneo mbalimbali duniani ikiwemo Ukraine.