Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Chelsea: Roman Abramovich anasema ana mpango wa kuiuza klabu hiyo
Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich anasema anapanga kuiuza klabu hiyo.
Katika taarifa kwenye tovuti ya klabu hiyo ya ligi ya Premier, mfanyabiashara Abramovich alisema ni "uamuzi mgumu sana kufanya", ambao "unamuumiza".
Hatua hiyo inafuatia siku za uvumi kwamba klabu hiyo itauzwa.
Bilionea Hansjorg Wyss aliliambia gazeti la Uswizi la Blick kwamba Abramovich alitaka "kuiuza Chelsea kwa haraka" baada ya tishio la vikwazo kuibuliwa Bungeni.
Abramovich alitoa "usimamizi na utunzaji" wa Chelsea kwa wadhamini wake kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Mapema Jumatano, bilionea Hansjorg Wyss aliliambia gazeti la Uswizi la Blick kwamba alikuwa amepewa nafasi ya kununua klabu hiyo ya London Magharibi.
Abramovich, 55, anadaiwa kuwa na uhusiano mkubwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin, jambo ambalo amelikanusha.
Katika taarifa yake, Abramovich aliongeza: "Siku zote nimekuwa nikichukua maamuzi kwa nia njema ya klabu.
"Kwa hali ilivyo sasa nimechukua uamuzi wa kuiuza klabu hii, kwasababu naamini hili ni kwa manufaa ya klabu, mashabiki, wafanyakazi, wadhamini na washirika wa klabu.
"Uuzaji wa klabu hautaharakishwa lakini utafuata utaratibu unaostahili. Sitaomba kulipwa mkopo wowote."
Abramovich aliinunua Chelsea mwaka wa 2003 na anasema " sio kwasababu ye biashara wala fedha, lakini kwasababu ana mapenzi na mchezo wa kandanda pamoja na klabu hiyo"
"Nimeiagiza timu yangu kuanzisha shirika la hisani ambapo mapato yote yanayotokana na mauzo yatatolewa. Shirika hilo litakuwa kwa manufaa ya wahasiriwa wote wa vita nchini Ukraine."