Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Shambulio la kikatili nchini Benin miaka 125 iliyopita lililobadilisha mtazamo wa Ulaya kuhusu Waafrika
Ulikuwa ya ukatili, uporaji, uharibifu na vifo.
"Benin ilizidiwa na janga ambalo linaweza kutumainiwa kuwa halitapona kamwe," mtaalam wa ethnolojia wa Ujerumani Eckart von Sydow aliandika miongo minne baadaye, akistaajabia "utajiri wa sanaa ya kipagani" iliyotolewa katika "Benin mpya" kutoka kwa tabula ras.
Jedwali hilo lilikuwa limeachwa bila kukamilika na msafara wa adhabu wa Uingereza mnamo Februari 1897, katika pambano kali lililodumu kwa siku 10.
Waingereza walishinda, wakavamia mji mkuu wa ufalme wa Benin, wakamtoa mfalme, na moto mkubwa ukateketeza mahali hapo.
Chanzo kilikuwa ni shambulio la kuvizia mwezi uliotangulia ambapo wapiganaji kutoka ufalme huo waliua kundi la mamia ya wanaume wakiongozwa na James Robert Phillips, kaimu balozi mkuu wa himaya ya Niger
Sababu ilikuwa ya kiuchumi.
Uharibifu wa Benin ulitokea katika kipindi kinachojulikana kama Kuing'ang'ania Afrika ambapo mataifa saba yenye nguvu ya Ulaya yalishindana kunyakua sehemu kubwa ya bara la Afrika iwezekanavyo. Mwaka 1870 asilimia 10 ya bara ilikuwa chini ya udhibiti wa Ulaya. Mnamo mwaka 1914, ilifikia asilimia 90.
Benin iliweza kudumisha uhuru wake na ukiritimba wa maliasili za thamani, kama vile mafuta ya mawese, pilipili, matumbawe ya buluu na pembe za ndovu, jambo ambalo liliwakera wakoloni wa Uingereza.
Lengo lake lilikuwa kuweka sehemu kubwa ya eneo la iliyo Nigeria ya sasa chini ya utawala wake.
Na katika harakati zao, waligawanya ufalme wa karne saba.
Karibu na mwisho wa karne ya 12 na mwanzoni mwa karne ya 13, oba Eweka I alianzisha Ibinu (ambayo baadaye ilitafsiriwa kama Benin na Wareno) kuwa jiji lake kuu.
Katika karne ya 16 na 17, Benin ilikuwa himaya ndogo-iliyotawala Igbo ya Magharibi, Yoruba ya Mashariki, na Itsekiri ya pwani, kati ya watu wengine-na nguvu kuu ya biashara katika pwani ya Nigeria.
Wasafiri wa Uropa waliandika kwa mshangao kuhusu ufalme huo uliofanikiwa.
Watu wa imani mbaya na wasiostaarabika
Biashara na Wazungu ilianza na Wareno mnamo 1472, na biashara ya Atlantiki ilipozidi kupanuka, iliendelea lakini tu na mashirika yaliyodhibitiwa na falme.
Pamoja na upanuzi wa biashara ya watumwa ya Atlantiki mwishoni mwa karne ya 17 na 18, falme nyingine za pwani zilianza kuchukua Benin, ambayo ilipata kupungua polepole kwa utawala wake wa eneo ambalo lilikuwa chini ya udhibiti wake.
Kuanzia katikati ya karne ya 19, uwepo wa Waingereza katika eneo hilo uliongezeka, kwa kisingizio cha kukomesha biashara ya utumwa.
Benin ilikataa wawakilishi wa Malkia Victoria kujadili mikataba na kupanua ulinzi juu ya ufalme huo.
Akiwa amechanganyikiwa, mgunduzi wa Uingereza Richard Burton, wakati huo akiwa Balozi wa Afrika Magharibi, mwaka wa 1862 alielezea kwa dharau Jiji la Benin kama "mahali pa ushenzi panaponuka kifo".
Uvumi wa dhabihu ya binadamu na biashara ya watumwa ulianza kuenea katika magazeti ya Ulaya.
Baada ya muda, ripoti za kupendeza za wageni wa Ureno na Uholanzi katika karne ya 15 na 16 zilibadilishwa na simulizi zahali ya kishenzi, zenye ghasia , ambapo watu wake walihitaji kuokolewa na kustaarabishwa chini ya utawala wa kikoloni au kuangamizwa kabisa.
Mshangao
Ushindi wa msafara wa adhabu ulivutia umakini wa ulimwengu.
Kwa miezi kadhaa, magazeti yalichapisha masimulizi ya kutisha ya mashahidi waliojionea yale ambayo wavamizi walikuwa wamepata katika "mahali pale pabaya."
"Msafara huo ulipoingia jijini, walipata kwamba lilistahili jina 'Jiji la Damu,'" Gazeti la The New York Times iliripoti.
"Wahasiriwa wengi au makuhani wachawi, walipatikana wamesulubiwa (...). Nyumba zilikuwa na damu ya wale ambao walikuwa wamekatwa vichwa hivi karibuni katika sherehe za kidini."
Kila kitu kilikubaliana na maoni ambayo yalikuwa yameshikiliwa kwa muda fulani kuhusu ufalme uliotoweka wa Benin.
Lakini uporaji huo ulipofika Ulaya, wasi wasi uliibuka.
Binadamu
Mwanzoni, baadhi ya wasomi, wakijaribu kuelewa jinsi mafundi wa Kiafrika wangeweza kutengeneza kazi hizo za sanaa, walipendekeza nadharia potofu.
Wengine walidai kwamba walifanya hivyo kwa kutiwa moyo na nchi za kigeni, labda kwa kujifunza kutoka kwa wageni kutoka Ulaya.
Lakini hatua kwa hatua walikuwa wakichukua kile kilichomaanisha kiwango cha mafanikio ya kisanii ya kile kilichochukuliwa kuwa utamaduni wa dhabihu uliojaa damu.
Mwanaanthropolojia wa Austria Felix von Luschan labda ndiye aliyeiweka kwa nguvu zaidi.
Katika makala ya 1898 aliandika kwamba kazi hizi za sanaa, ambazo kwa hakika zilitengenezwa na Waafrika na ambao mtindo wao ulikuwa "wa Kiafrika kabisa, dhahiri na wa kipekee", zilikuwa ushahidi wa "sanaa kuu na kubwa ya asili".
Alisema hilo lilikuwa na "umuhimu wa kimaadili" kwani lilionyesha uwongo wa "dharau iliyoenea kwa waru weusi, haswa katika zile zinazoitwa duru za 'ukoloni'".
Mwaka uliofuata, alipozungumza katika Kongamano la Kimataifa la Kijiografia mjini Berlin, alitumia vitu vya sanaa vya Benin kama sehemu ya hoja yake kukanusha dhana potofu nyingi kuhusu Waafrika.
Na pia kama ombi kwa ubinadamu wake kutambuliwa: wanadamu ambao wangeweza kufikia ukamilifu huo katika sanaa hawakustahili kuchukuliwa kuwa nusu nyani.
Usasa
Mbali na kutikisa dhana ya Waafrika, uporaji kutoka Benin ulifanya sanaa ya Kiafrika ionekane kwa Wazungu, ambao wamekuwa wakikusanya kila aina ya vitu vya sanaa lakini hawakuthamini kuwa mambo ya kisanii.
Miaka michache baadaye, "ugunduzi" huu wa sanaa za bara lililoshindwa ungeongoza utamaduni kwenye njia ambazo hazijapitwa.
Baada ya kujikomboa kutoka kwa sheria ngumu za zamani, wasanii wa plastiki walifurahia wigo mpana wa majaribio.
Kuchunguza upeo mpya, wengi walivutiwa na aina za ubunifu za kitamaduni na za ajabu wa sanamu na vinyago vya Kiafrika.
Vitu vilivyoibwa
Hakuna lolote kati ya haya lililokuwa katika mipango ya wale ambao miaka 125 iliyopita waliamua kuondoa Ufalme wa Benin.
Ingekuwa miaka mingi kabla ya Uingereza, na Ulaya, kuanza kujisikia aibu kwa matendo yao katika bara la Afrika.
Na miaka zaidi kabla ya makumbusho ya ulimwengu ambayo huhifadhi kile ambacho milki ziliondoa zilizingatia uwezekano wa kuirejesha.
"Uporaji huo ulikuwa aina ya mkakati wa kijeshi," Dan Hicks, profesa wa elimu ya kale katika Chuo Kikuu cha Oxford, aliiambia BBC.
"Ililenga kunyang'anywa mamlaka, kuchukua vitu kutoka kwa wafalme, uharibifu wa dini ya jadi, kuchukua vitu vya kidini. Na kwamba kunyang'anywa kwa kitamaduni kutaendelea hadi vitu vinavyodaiwa virejeshwe."
Baadhi ya taasisi za Ulaya zimeanza kufanya hivyo, na Ufaransa, Ubelgiji na Ujerumani zimetangaza kufanya hivyo pia.
Unaweza pia kusoma:
Huko Ulaya na Marekani kuna vitu zaidi ya milioni 100 vilivyochukuliwa kutoka Afrika, vingi vikiwa kwenye maghala, vikifichwa kwa miaka 100 iliyopita.