Ukraine inataka mkutano na Urusi katika kipindi cha saa 48 kujadili kuongezeka kwa wanajeshi

Ukraine imeitisha mkutano na Urusi na wajumbe wengine wa kikundi muhimu cha usalama cha Ulaya kuhusu kuongezeka kwa hali ya wasi wasi kwenye mipaka yake.

Wazir wa mambo ya nje wa nchi hiyo Dmytro Kuleba alisema kuwa Urusi ilipuuza maombi rasmi ya kufafanua kuonezeka kwa vikosi vyake kwenye mpaka baina ya nchi hizo mbill.

Alisema "hatua inayofuata" ni kuitisha mkutano katika kipindi cha saa 48 kwa ajili ya "uwazi " kuhusu mipango ya Urusi.

Russia inakanusha kuwa na mipango yoyote ya kuivamia Ukraine licha ya kuongeza wanajeshi wake 100,000 kwenye mipaka na Ukraine.

Lakini baadhi ya mataifa ya magharibi wametahadharisha kuwa Urusi inajiandaa kwa ajili ya hatua ya kijeshi, huku Marekani ikisema kuwa Urusi inaweza kuanza kupiga makombora ya anga "wakati wowote".

Unaweza pia kusoma:

Zaidi ya mataifa kumi na mawili yamewataka raia wake waondoke Ukraine, na baadhi yamewaondoa wafanyakazi wake wa ubalozi katika mji mkuu wa nchi hiyo. Shirika la Habari la CBS News liliripoti kuwa Marekani inaandaa kuondoa wafanyakazi wake wote kutoka mjini Kiev katika kipindi cha saa 48 likinukuu vyanzo.

Bw Kuleba alisema kwamba Ijumaa Ukraine, ilidai majibu kutoka kwa Urusi kuhusu malengo yao chini ya sheria za Vienna , makubaliano kuhusu masuala ya usalama ya wajumbe wa shirika la usalama na ushirikiano barani Ulaya (OSCE), ambayo yanaihusisha pia Urusi.

"Iwapo Urusi ni makini inapozungumzia kuhusu usalama katika eneo la OSCE , ni lazima itekeleze wajibu wake wa uwazi wa kijeshi, ili kuondoa hali ya wasi wasi na kuimarisha usalama kwa wote ," alisema.

Hata hivyo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ambaye anakosoa kwamba "wasi wasi " unaweza kusambaa kutokana na madai ya aina hiyo, alisema kuwa hajaona ushahidi wowote kwamba Urusi inapanga uvamizi katika siku zijazo.

Jumapili, alizungumza kwa karibu saa nzima kwa njia ya simu na rais wa Marekani Joe Biden. Ikulu ya White House ilisema kuwa Rais Biden alirejelea tena uungaji mkono wa Marekani kwa Ukraine, na kuongeza kwamba viongozi wote wawili wamekubaliana kuhusu "umuhimu wa kuendelea kutumia njia ya kidiplomasia na kuzuwia ukosefu wa usalama ".

Taarifa ya Ukraine ya wito ilisema kuwa rais wake alimshukuru rais wa Marekani kwa "msaada wake usioyumba " na kwamba, mwisho wa mazungumzo hayo Rais Zelensky alimkaribisha kiongozi wa Marekani kuja Ukraine. Hakuna kauli iliyotolewa kuhusu mwaliko huyo kutoka Ikulu White House.

Mazungumzo ya njia ya simu ya saa nzima baina ya Rais Biden na kiongozi wa Urusi Vladimir Putin siku moja kabla kabla yalishindwa kufikia mafanikio yoyote.

Washirika wa Magharibi awali walitangaza wazi kuhsuu moja ya madai ya Urusi-kwamba Ukraine isiwahi kuruhusiwa kujiunga na Muungano wa Nato-sio swala la kujadiliwa, wakisema kuwa milango ya muungano huo lazima ibakie kuwa wazi kwa ajili ya wajumbe wapya wanaotaka kujiunga.

Lakini balozi wa Ukraine mjini londo, Vadym Prystaiko, ameiambia BBC kwamba nchi yake huenda kikawa tayari kuachana na lengo lake la kujiunga na Nato ili kuzuwia vita, akisema kuwa Ukraine inaweza "kuwa tayari kubadili msimamo wake".

Alipoulizwa iwapo utawala wa Kiyv unaangalia uwezekano wa mipango ya kujiunga na uanachama wa Nato, licha ya kwamba hilo limeandikwa katika katiba ya Ukraine, alijibu : "Tunaliweka kwenye uzani-hususan wakati tunapotishwa kama hivyo, kusalitiwa na hilo, na kusukumwa katika ."

Katika jaribio la hivi karibuni la kutafuta suluhu la kidiplomasia Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amepanga kufanya mikutano na Rais Zelensky mjini Kyiv Jumatatu na Putin Jumanne mjini Moscow.

Kansela, ambaye alichukua uongozi wa Ujerumani baada kutoka kwa Angela Merkel mwenzi Disema, ameonya juu ya athari mbaya ya kiuchumi kwa Urusi iwapo itaanzisha uvamizi wowote , akiunga mkono taarifa za mataifa mengine ya magharibi na wajumbe wa muungano wa kijeshi wa Nato.

Merkel mwenzi Disema, ameonya juu ya athari mbaya ya kiuchumi kwa Urusi iwapo itaanzisha uvamizi wowote , akiunga mkono taarifa za mataifa mengine ya magharibi na wajumbe wa muungano wa kijeshi wa Nato.

Lakini maafisa wa Berlin wameelezea wasi wasi juu ya matarajio yoyote ya kudikiwa kwa mafanikio yoyote katika mazungumzo hayo.

Wakati huo huo, Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson anapanga kufanya mazungumzo mapya ya kidiplomasia kote kuondoa ''Urusi katika hali ya kukaribia'' vita.

Mjini Washington, mshauri wa Rais Biden wa usalam wa taifa Sullivan alisema uvamizi unaweza kuanza "siku yoyote kuanzia sasa".

Bw Sullivan alisema kuwa Marekani inafuatilia kwa uwezekano wa "dalili zisizo uongo" za operesheni za Moscow kama dalili za uvamizi kamili ili iweze kudai kwamba inajibu uchokozi wa Ukraine.

Urusi inasema hatua yake ya kuongeza wanajeshi wake kwenye mpaka na Ukraine unatokana na hofu yake, ndani ya eneo lake. Jumapili , afisa wa ngazi ya juu wa sera Yuri Ushakov alilielezea tahadhari ambazo zimekuwa zikitolewa na Marekani kama '' zilizotiwa chumvi kwa kiwango cha juu ".