Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je, Marekani, Urusi na China wanaelekea kwenye vita vya anga za mbali?
Mnamo mwaka 1982, Umoja wa Uovyeti ulizindua satelaiti ya kijasusi iliyoitwa Kosmos-1408 kwenda anga za mbali. Baada ya miaka miwili ya kwenda anga za mbali, ikawa haina maana na tangu wakati huo ilikuwa ikiendelea kuzunguka katika obiti yake.
Hatimaye, mnamo Novemba 2021, Urusi iliiharibu kwa kurusha kombora la kuzuia satelaiti. Karibu vipande 1,500 vyake vilienea angani.
Hapo awali, Amerika ilifanya hivi mnamo 2008 na Uchina mnamo 2007.
Hatua hiyo ya Urusi ilikosolewa vikali kwa sababu vipande vya satelaiti hiyo vingeweza kugonga chombo kingine na kusababisha ajali kubwa angani.
Kwa hivyo wakati huu ulimwenguni kote, hatupaswi tu kuuliza juu ya nani anapaswa kufanya nini, nini haipaswi kufanywa katika anga za mbali, ni sheria gani zinapaswa kufanywa kuhusu hili. Swali letu ni je, anga za mbali zitakuwa uwanja mpya wa migogoro?
Taka katika anga za mbali
Inasemekana kwamba watu huona anga za mbali kuwa mahali pasipo na chochote lakini sivyo. Kulingana na data hadi Aprili 2021, zaidi ya satelaiti 7,300 zinazunguka kwa kasi kubwa katika anga ya kilomita mia chache juu ya Dunia.
"Zote zinazunguka kwa kasi ya maili 17,000 kwa saa kwenda kila upande. Ni kama uwanja mkubwa wa michezo wenye wachezaji wanaokimbia huku na huko," McDall alisema.
Ili kusalia katika obiti yake, satelaiti hiyo inabidi iruke kwa kasi hiyo, yaani, kila satelaiti, ikiwa ni pamoja na Kituo cha Kimataifa cha Anga cha mbali, hufanya takribani mizunguko 16 ya Dunia kwa siku.
Lakini idadi kubwa kama hiyo ya satelaiti inafanya nini angani?
McDwell anaeleza zaidi, "Satelaiti hutumiwa sana katika mawasiliano, kama vile matangazo ya televisheni, simu na Intaneti na kwa utabiri wa hali ya hewa. Ni rahisi kuona mahali ilipo Dunia kwa kutumia satelaiti, hivyo inasaidia katika kugundua mabadiliko ya hali ya hewa."
Hiyo ni ni kusema sehemu kubwa ya mahitaji yetu duniani yanahusiana na satelaiti hizi. Hapo awali, satelaiti nyingi zilirushwa na serikali, kwani wakati wa Vita Baridi, satelaiti nyingi zilitoka kwa serikali ya Marekani au Usovieti.
Lakini baada ya muda makampuni ya kibinafsi yanakuja katika sekta hii kwa matumizi ya kibiashara. Swali ni kwamba ikiwa idadi kubwa ya satelaiti zinazunguka angani, basi kwa nini hazigongani. Je, kuna udhibiti wowote kwa haya pia?
McDwall anasema, "Kanuni kuhusiana na hizi ni za kawaida sana. Matumizi ya masafa ya redio, lakini kuna sheria kali sana ili mawimbi unayotuma yasiingilie. Lakini unaweza kufanya chochote unachotaka kwenye obiti yako. Anga za mbali sio barabara ambapo magari ni sharia kwa kwenda upande mmoja kwa mwendo sawa. Unapaswa kudhani kuwa angali za mbali ni sehemu kubwa na hautamgonga yeyote. Hili linakuwa shida kubwa."
Wasiwasi mkubwa
Anga za mbali sasa inazidi kuwa mahali penye msongamano na juhudi za kuepusha hali ya mgongano pia zinaongezeka. Taka nyingi hufuatiliwa, lakini wakati Urusi ilipoharibu setilaiti yake mwaka wa 2021, taka iliyotoa haikufuatiliwa na baadhi ya sehemu ya taka ilikuwa karibu na obiti ya Kituo cha Kimataifa cha Anga za mbali.
"Kila baada ya dakika 93, udhibiti wa safari ulikuwa ukituma ujumbe wa redio kwa kituo cha anga kuwa uko karibu kupitia takataka tena, jaribu kuwa salama. Jambo la msingi ni kwamba lazima upate data sahihi la hali hiyo ya taka," McDwall alisema. Anwani kamili haijulikani, kwa hivyo ni ngumu sana kuizuia."
Ikiwa uharibifu wa moja ya satelaiti za nchi unaweza kusababisha hatari kubwa kama hiyo, basi inaweza kukadiriwa kwamba ikiwa jaribio lilifanywa la kusababisha uharibifu kwa makusudi, basi uharibifu ungekuwa mkubwa kiasi gani.
Kwa hivyo inawezekana kwamba mvutano kati ya nchi mbili hautaishia ardhini na kufikia anga za mbali.
Kuhusiana na hili, McDwell anasema, "Tangu wanadamu wameingia angani, kumekuwa na uwepo wa jeshi. Lakini hawarushi silaha, bali wanarusha satelaiti za kijasusi au mawasiliano kusaidia jeshi duniani. Lakini jeshi la Marekani na nchi nyingine zinaongelea migogoro katika anga za juu.Jeshi la ardhini kwa kiasi kikubwa linategemea satelaiti na ikitokea mzozo hapa duniani basi jambo hilo linaweza kufika angani pia.Ugumu ni kwamba hili likitokea litaleta takataka kubwa na matumizi ya anga za mbali yatakuwa magumu sana."
Na pia ni jambo la kutia wasiwasi kwamba athari za mkazo katika anga zinaweza kuathiri mamilioni ya maisha. Na hili sio suala la siku zijazo, tayari limeanza.
Kiasi gani cha mvutano kilicho katika obiti ya anga za mbali
Alexandra Stickings, Kiongozi wa Mikakati ya Anga katika Ushauri wa Fraser-Nash, anasema kuwa nchi zinaweza kuwa na sababu nyingi za kudhuru misheni za kila mmoja angani.
Anasema, "Nadhani inahusiana na kwa nini anga inatumika na ni habari gani inapokelewa kutoka angani kwa kazi inayoendelea duniani. Ukiweza kuzuia habari kumfikia adui, basi utakuwa na uwezo. "
Stickings anaonyesha kuwa kuna njia nyingi za kuharibu misheni za anga. Kulingana na yeye, "Kuna makombora ya kuzuia satelaiti ambayo yanaweza kuharibu satelaiti, kusababisha msongamano wa GPS na hata kufanya kitambuzi cha macho cha satelaiti kutoweza kutumika kwa muda. Usumbufu huo unaweza kuzuia taarifa kutufikia."
Tishio la Urusi
"Watu wanadhani kwamba anga za mbali ni kama msitu ambao hakuna sheria, lakini ukweli ni kwamba popote mtu anakwenda, sheria itaenda naye."
Bado hakuna mfumo wa kisheria uliotengenezwa wa anga hiyo. Lakini baada ya jaribio la silaha za nyuklia zinazozozaniwa katika anga ya juu ya Amerika, makubaliano ya anga ya juu yalifanyika mnamo 1967.
Mitchell analinganisha hili na sheria iliyotungwa nchini Uingereza miaka 800 iliyopita, akisema, "Tunauchukulia mkataba huu kuwa ilani ya Sheria ya Anga, hauzungumzii sheria bali maadili tuliyo nayo kama taifa na wanadamu." Lakini kile tunachopaswa kufanya na tusichopaswa kufanya katika anga za mbali. Msingi unapaswa kuwa kwamba kila mtu anaweza kutumia anga kwa usawa na inapaswa kutumika kwa kazi ya amani.
Hakuna kitu ambacho kimesemwa juu ya kazi yoyote, lakini kuna jambo moja ambalo ni marufuku kabisa. Kuhusu jambo hilo, Michel alisema, "Inasema kwamba silaha za maangamizi makubwa na silaha za nyuklia haziwezi kuwekwa karibu na obiti au mahali popote kwenye anga. Hili lilikubaliwa baada ya enzi ya Vita Baridi. Leo, ikiwa tunazungumzia sheria za anga, basi Mkataba huu ndio msingi wake Lakini inatarajiwa kuwa nchi zitazuia tabia zao.
Hiyo ni, kipaumbele cha nchi iwe kwamba shughuli za anga zisigeuke kuwa migogoro, lakini hii inafanyika kwa sababu kuharibiwa satelaiti ya Urusi imekuwa suala kubwa.
Matarajio ya baadaye
Katika gazeti la The Economist, Mhariri wa masuala ya ulinzi Shashank Joshi anaandika juu ya masuala yanayohusiana na ulinzi na usalama. Anasema kuwa mashambulizi yanayohusiana na teknolojia ya kidijitali Duniani yanaashiria kile tunachoweza kuona katika anga ya mtandao na anga katika nyakati zijazo.
Alisema, "Katika nyakati chache zilizopita tumeona mashambulizi ya kila kitu kuhusiana na maisha ya binadamu. Mizizi ya vita itakuwa daima duniani, iwe chini ya mtandao au anga. Hakuna eneo litakalokuwa huru kutokana na athari za vita hadi hatua zichukuliwe kuwazuia.
Hoja ya Shashank inaweza kueleweka kwa mfano, Urusi inashutumiwa kwa kuhamisha vifaa vya kijeshi ili kujiandaa na mashambulizi kwenye mpaka wa Ukraine. Hili ni jambo ambalo linaweza kuthibitishwa na picha za satelaiti. Lakini Shashank anasema kuwa tuhuma zinazuka kuwa Urusi inazuia picha hizo kuingia kwenye rada.
Alisema, "Kuna satelaiti ya rada inaitwa Sentinel One. Ilitumika kupiga picha za rada za vituo vya kijeshi vya Urusi karibu na Ukraine. Inaaminika kuwa picha hizo haziwezi kupigwa, kwa hivyo Urusi inaingilia satelaiti hiyo ili kuzizuia."
Vita kama hivyo vinaweza kuharibu zaidi kuliko vita vinavyoonekana katika filamu za kisayansi. Kadiri nchi inavyokuwa na vifaa vingi, ndivyo inavyosemekana kuwa hatarini zaidi. Katika suala hili, China na Amerika ziko karibu katika kiwango sawa. Lakini Shashank anasema kuwa itakuwa makosa kudhani kwamba nchi yenye vyombo vingi vya anga katika obiti pia ndiyo yenye nguvu zaidi angani.
Kwa hivyo tunarudi kwenye swali letu. Je anga itakuwa msingi mpya wa migogoro?
Tunajua kwamba mamia ya kilomita juu ya Dunia, maelfu ya satelaiti zinazunguka. Zinaunganisha watu wengi duniani na kuwa chanzo cha habari zinazohitajika ili kukuza uchumi wa dunia. Lakini barabara kuu hii ya anga imekuwa na msongamano mkubwa sasa. Sasa satelaiti za zamani zimekuwa tishio, kutokana na hatari ya mgongano wa satelaiti umeongezeka kwa kiasi kikubwa.
Bado kuna wakati wa kufikiria na kuchukua hatua, anasema mwanasayansi wa nyota Johnathan McDavall katika Kituo cha Harvard-Smithsonian cha Astrofizikia.