Sue Gray: Tafrija katika ofisi ya waziri mkuu wa Uingereza katika 'lockdown' zisingeruhusiwa

Sue Gray amelaumu "kushindwa kwa uongozi "kwa kuruhusu kufanyika kwa tafrija ifanyike katika ofisi za waziri mkuu wa Uingereza Downing Street wakati nchi ikiwa chini ya sheria kali za kukabiliana na maambuki ya Covid ''lockdown''

Katika matokeo ya uchunguzi uliosubiriwa kwa muda mrefu kuhusu tukio hilo, mhudumu wa ngazi ya juu wa umma anasema baadhi ya matukio "hayakupaswa kufanyika".

Bi Gray alichunguza mikusanyiko 16 tofauti ikiwa ni pamoja na matatu ambayo awali hayakujulikana awali.

Boris Johnson alisema kuwa alikubali yaliyomo katika uchunguzi huo kwa ukamilifu, katika taarifa aliyoitoa kwa Wabunge.

"Ninaomba msamaha kwa vitu ambavyo hatukuvifanya kwa usahihi na pia kwa ambavyo suala hili limeshugulikiwa, alisema, Waziri mkuu Johnson, huku akiahidi kufanya mabadiliko ya jinsi mambo yanavyoendeshwa katika Downing Street.

Katika matokeo ya uchunguzi wake, Sue Gray, anasema hofu za afya ya umma "haikufikiriwa " na pia jinsi tukio hilo lingeonekana kwa umma.

Ripoti yake inathibitisha kwamba polisi ya mji inachunguza matukio 12 kwa madai ya kukiuka sheria za Covid.

Matukio hay ani pamoa na tukio la tarehe 20 Mei 2020 "leta pombe yako mwenyewe" tukio lililofanyika katika Downing Street, ambalo waziri mkuu ameomba msamaha kwa kuhudhuria, na sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya Waziri mkuu ya tarehe 19 Juni 2020.

Polisi pia wanachunguza mkusanyiko wa tarehe 13 Novemba 2020 uliokuwa katika jingo la gorofa lililoko Downing Street , ingawa haijathibitishwa kuwa Bw johnson alikuwa katika tukio hili.

Taarifa ya Bi Gray ilisema ali "wekewa ukomo mkubwa" na uchunguzi wa polisi kuhusu ni kiasi gani anaweza kusema kuhusu mikusanyiko

Lakini alikosoa utamaduni katika Downing Street miongoni mwa wahudumu wa ngazi ya juu na wafanyakazi.

"Wakati mwingine inaonekana kuna fikra za kiwango cha chini kwa kile kinachoendelea kote nchini katika kuangalia usahihi wa baadhi ya mikusanyiko hii, hatari inayoweza kusababisha kwa afya ya umma na jinsi inavyoweza kuonekana kwa umma.

"Baadhi ya matukio yasingepaswa kuruhusiwa kufanyika. Matukio mengine hayangeruhusiwa kuandaliwa kama walivyofanya."

Aliongeza kuwa "unywaji wa pombe wa kupindukia haufai katika maeneo ya kazi wakati wowote",

Huenda kutakuwa na ripoti za tabia ya ulevu katika bustani ya ofisi ya waziri mkuu -Number 10 na wafanyakazi waliojaza mifuko chupa za mvinyo.

Hatua zinapaswa kuchukuliwa kuhakikisha idara za serikali zina sera "thabiti" juu ya unywaji wa pombe, ripoti imesema.

Unaweza pia kutazama:

Awali kiongozi wa chama cha Labour Sir Keir Starmer alisema Waziri Mkuu sasa lazima aache visingizio vyake "vya kusikitisha" na uwongo "wa kipuuzi".

Wakati Waziri Mkuu akipambana kuokoa wadhifa wake, alikiri bungeni "hasira" ya umma juu ya hafla ya Mei 2020 kwenye bustani ya Downing Street.

Alisema anajutia kitendo chake, na anaamini tukio hilo lilihusiana na kazi.

Alisema alitumia takriban dakika 25 kwenye hafla hiyo, ili aweze "kushukuru vikundi vya wafanyikazi" kwa bidii yao.

Lakini aliongeza: "Kwa kuzingatia athari ya tukio lenyewe bila shaka ningemrudisha kila mtu ndani.

"Ningepata njia nyingine ya kuwashukuru, na nilipaswa kutambua kwamba - hata kama ingesemwa kitaalamu ingekiuka mwongozo - kungekuwa na mamilioni na mamilioni ya watu ambao hawangeona hivyo. "

Wabunge wa upinzani walijitokeza kumtaka waziri mkuu ajiuzulu - au wabunge wake wamtoe kwa lazima - katika Maswali ya Waziri Mkuu yenye dhoruba.

Sir Keir Starmer alisema: "Hali ndio hiyo. Baada ya miezi kadhaa ya udanganyifu na udanganyifu, tamasha la kusikitisha la mtu ambaye ameishiwa njiani limefika ukingoni.

"Utetezi wake...kwamba hakutambua kuwa alikuwa kwenye tafrija ni ujinga kiasi kwamba unakera umma wa Uingereza.

"Hatimaye amelazimika kukiri kile ambacho kila mtu alijua, kwamba wakati nchi nzima ilikuwa imefungwa alikuwa akiandaa karamu za pombe Downing Street. Je, sasa atafanya jambo la heshima na kujiuzulu?"