Omar Weeks: Licha ya kuhudumia kifungo chini ya Taliban, bado anataka kurudi Afghanistan

Jibril Umar

Chanzo cha picha, JIBREEL OMAR

Maelezo ya picha, Gabriel Omar aka Timothy Weeks

Timothy Weeks (ambaye jina lake la Kiislamu ni Jibril Omar), ambaye aliishi katika kifungo cha Taliban kwa miaka mitatu na nusu na kubadili dini kuwa Muislamu, sasa anataka kwenda Afghanistan kwa mara nyingine tena.

Jibril Omar (Timothy Weeks) alitekwa nyara na Taliban mnamo Agosti 2016 kutoka lango kuu la Chuo Kikuu cha Marekani huko Kabul. Na baada ya kuwa katika kizuizi cha Taliban kwa miaka mitatu na nusu, aliachiliwa mwaka 2019 akibadilishwa na makamanda watatu mashuhuri wa Taliban, akiwemo Haqqani, chini ya Mkataba wa Doha.

Alikuwa mwalimu wa Kiingereza katika Chuo Kikuu cha Marekaji mjini Kabul. Alipewa jukumu la kuunda mtaala wa kufundisha Kiingereza kwa maafisa wa polisi wa Afghanistan.

Jibril Omar (Timothy Weeks) aliwasili Afghanistan mnamo Julai 2016 na alikuwa bado hajaanza kazi ya kuandaa mtaala, kwamba mnamo Agosti 9 mwezi uliofuata Taliban, pamoja na mmoja wa washirika wake, Kevin King, walitekwa nyara kwenye lango la chuo kikuu.

Ili kuwapata wote wawili, Jeshi la Merika lilifanya operesheni kadhaa katika sehemu tofauti za Afghanistan. Katika tukio moja au mawili, ilitokea kwamba makamanda wa jeshi la Merika hata walifika mahali ambapo wote wawili waliwuwa wakizuiwa.

Operesheni ya uokoaji ya Jeshi la Marekani

Malengo yalikuwa ni pamoja na kufikia boma katika mji wa Ghazni nchini Afghanistan, ambapo wanajeshi wa Taliban na Marekani walipambana wakati wa shughuli za uokoaji.

Picha ya Timothy Weeks akiwa na Kevin King chini ya Kizuizi cha Taliban

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Picha ya Timothy Weeks akiwa na Kevin King chini ya Kizuizi cha Taliban

Hata hivyo, majeshi ya Marekani yalishindwa kuwaokoa mateka hao, kwani kila mara mateka hao walihamishiwa sehemu nyingine siku chache kabla ya operesheni hiyo.

Kabla hatujaingia kuhusu jinsi Timothy Weeks aligeuka kuwa muislamu wakati wa utumwa wa Taliban, ni muhimu kujua kwamba baada ya miaka mingi ya mateso katika utumwa wa Taliban, kuachiliwa kwa mazungumzo magumu ni kwa nini Timothy Weeks, au Gabriel Omar, anataka kwenda Afghanistan tena?

'Kurudi Afghanistan ndio kusudi la maisha'

Katika mahojiano maalum yaliyofanywa na BBC, Gabriel Omar (Timothy Weeks) anasimulia maisha yake kabla na baada ya miaka hiyo mitatu na nusu, akisema kwamba maisha yake yalianza kubadilika alipotekwa na Taliban.

Anasimulia kuwa "Siku moja nikiwa nje ya nyumba niliyokuwa nimefungwa, nilisikia sauti za watoto wakicheza, wakirukaruka na kucheka. Mimi kama mwalimu, nilikuwa na wasiwasi kuhusu mustakabali wa watoto hao, kwamba watoto hawa maskini walikuwa na nini matarajio ya maisha bora yajayo?

Na wakati huo huo, niliamua kwamba ikiwa maisha yangu yataokolewa na niwe huru , nitarudi Afghanistan tena na kufanya chochote niwezacho kwa watoto hawa."

Aliendelea, "Kwa kuwa sasa niko huru, nakusudia kushirikiana na serikali ya Taliban nchini Afghanistan kuwasomesha watoto hawa hasa wasichana na wanawake. Nimejitambulisha na wasichana na wanawake." Nimejitolea kuelimisha na ninaamini kuwa ninaweza kufanya mengi nchini Afghanistan kwa kuanzisha shirika la kutoa misaada."

Alisema kuwa "Sijutii tena kutekwa nyara na Taliban, kwa sababu kama isingetokea nisingejua ukweli wa Uislamu. Sasa naipenda Afghanistan, utamaduni wake na watu wake na ninataka kufanya kazi kwao."

Alihudumia kifungo cha mikak mitatu jela

Chanzo cha picha, JIBREEL OMAR

Maelezo ya picha, Alihudumia kifungo cha mikak mitatu jela

Kifungo cha cha miaka mitatu na nusu

Kipindi hiki cha miaka mitatu na nusu kwenye kifungo cha Taliban kilikuwa kigumu sana kwa Jibril Omar (Timothy Weeks). Wanasema kwamba mara nyingi walifungwa minyororo ili wasiweze kukimbia. Taliban walikuwa wakiwasumbua kwa uharibifu wowote uliofanywa na jeshi la Marekani, haswa wakati wapiganaji wa Taliban walikuwa wakiwatesa kila zinapotokea habari za kifo cha wapiganaji wa Taliban kutoka sehemu yoyote.

Ambapo Kevin King, ambaye alitekwa nyara pamoja naye, alikuwa amefungwa kwenye mwisho wa minyororo badala ya kufungwa kabisa kwa sababu alikuwa mzee na mgonjwa.

Jibril Omar (Timothy Weeks) anaeleza kuwa akiwa katika kifungo cha Taliban, pia alilazimika kuosha sakafu na kufua nguo za Taliban kwa maji baridi, ikiwa hazikusafishwa vizuri, wangepigwa.

Jibril Omar (Timothy Weeks) anasimulia operesheni iliyofanywa na wanajeshi wa Marekani kwa ajili ya kuachiliwa kwake akiwa kifungoni, "Wakati Navy SEALs walipoingia kwenye boma la nyumba tulimofungwa wakati wa mapigano na Taliban. Tulithubutu kuwauliza Taliban ni nani washambuliaji hawa lakini hawakusema ukweli , walisema washambuliaji hao walikuwa ni ISIS.

Timothy Weeks na wanawe wa kike

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Timothy Weeks na wanawe wa kike

Kuhusu muda wa kukaa gerezani, anasema kuwa "gereza la Kaid toh hai, kulikuwa na hali ngumu sana. Kuna wakati nilipigwa na kuteswa sana hivi kwamba hakukuwa na matumaini ya kuona siku iliyofuata."

Katika miaka miwili ya kwanza ya kifungo chake, maisha ya Jibreel yalikuwa magumu sana, huku mateso ya Taliban na chakula kikiwa kidogo sana kuweza kuishi.

Alibadili dini na kuwa Muislamu akiwa gerezani nchini Afghanistan

Jibril Omar anasema kwamba wakati wa kukaa kwake kifungoni, wakati mateso kutoka kwa Taliban yalipopungua, na hali ikaanza kuimarika, ndipo akapendezwa na kusoma.

"Nilipowauliza Taliban baadhi ya vitabu, walileta vitabu vilivyochapishwa kutoka Urdu Bazaar Karachi na tafseer ambayo ni tafsiriya Quran kwa Kiingereza."

"Baada ya kusoma vitabu hivi na Quran, taratibu nilianza kuvutiwa na Uislamu. Hatimaye tarehe 5 Mei, 2018, nilibadili dini na kuanza kutumia Wudhu na Namaz."

Anasema, "Wakati Taliban walipojua kuhusu kubadili dini kwangu, badala ya kufurahi, walianza kunitishia kuniua."

Omar Weeks akiwa na waziri wa mkuu wa Australia

Chanzo cha picha, JIbrael Omar

Maelezo ya picha, Omar Weeks akiwa na waziri wa mkuu wa Australia

'Niliitwa mbwa huko Australia, nikatemewa mate'

"Mara nyingi ninahisi kwamba vita dhidi ya ugaidi vinaonekana kama vita dhidi ya Uislamu," anasema Jibril Omar.

"Sielewi hili katika muktadha wa Afghanistan, lakini kama Muislamu mamboleo. Ninaelewa hili kwa misingi ya mateso niliyofanyiwa katika nchi yangu ya Australia, ambako nilitemewa mate mitaani, niliteswa hata kuitwa mbwa. "

Anasema kuwa kwa bahati mbaya ulimwengu wa magharibi unakumbwa na chuki dhidi ya Uislamu.

Jibril Omar anasema kwamba aliporudi nyumbani baada ya kifungo cha miaka mitatu na nusu gerezani, na wanafamilia wake wakagundua kwamba ninamuunga mkono 'adui' wangu, serikali ya Taliban nchini Afghanistan, ilikuwa vigumu sana kukubali jambo hilo.

Kitabu kuhusu Afghanistan

Kuhusu nia yake ya siku za usoni, Gabriel Omar alisema kuwa ameanza kufanyia kazi kitabu chake. "Kupitia kitabu hiki, nitaweza kutimiza wajibu wangu wa kuiambia dunia kuhusu Afghanistan."

Ametia saini mkataba na mchapishaji maarufu duniani 'HarperCollins' ili kuchapisha kitabu hiki, na kitabu hicho kinatarajiwa kukamilika mapema mwaka ujao. Anasema, "Kwa sasa, wakimbizi duniani kote wanakabiliwa na matatizo mengi kama wafungwa. Natumaini kwamba katika siku zijazo watapewa sehemu yao ya haki."