Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Chanjo ya Covid: Je una maswali yapi kuhusu chanjo za Covid?
Zaidi ya nusu ya wakazi wa dunia wamepokea walau dozi moja ya chanjo dhidi ya virusi vya corona. Hata hivyyo chanjo zilizotolewa zimekuwa zikizingirwa maswali mbali mbali kuzihusu.
Katika taarifa hii kitengo cha BBC Reality Check kinajibu baadhi ya maswali yanayoulizwa kuhusu chanjo:
Femi kutoka Nigeria anasema: "Sababu iliyonifanya nisiamini au nisite kuipata chanjo ya Covid-19 ni kwasababu ya namna chanjo ilivyotengenezwa kwa haraka ."
Jibu ni kwamba chanjo dhidi ya Covid zimekuwa zikitengenezwa kwa kasi kubwa sio kwasababu zimevuka hatua au kuharakishwa kwa utafiti kuzihusu, bali kwasababu wanasayansi na wenye makampuni kutoka maeneo yote ya dunia yalishirikishana kazi zao kwa ajili ya ufanisi wa chanjo hizo.
Chanjo za Covid zimekuwa zikifanyiwa majaribio ya kina kwa ajili ya usalama-kwanza katika majaribio ya maelfu ya watu ili kubaini athari yoyote ya kawaida na pia kupitia ufuatiliaji makini wakati chanjo zilipotolewa kwa mamilioni ya watu katika umma kwa ujumla, kuwawezesha wanasayansi kubaini athari ambazo hujitokeza kwa nadra zaidi. Lakini hata sasa, bado zinaendelea kufanyiwa utafiti na kufuatiliwa.
Lakini vipi kuhusu swali kwamba kuhusu iwapo watu ambao wamechanjwa bila matatizo yoyote, wanaweza kupata matatizo miezi au miaka baadaye ?
Wanasayansi waliochunguza chanjo za covid na mfumo wa kinga mwilini wanasema hili huenda lisitokee kabisa-tunafahamu vya kutosha kuhusu jinsi mwili wa binadamu unavyofanya kazi na tuna uzoefu wa kutosha kutokana na chanjo za kufahamu kuwa athari mbaya yoyote itajitokeza katika miezi miwili ya kwanza. Kwahiyo tumekuwa na muda wa kutosha wa athari hizo kuweza kujitokeza.
Sukria, kutoka Thailand alisema: "Wengi wa wale waliopata chanjo bado walipata maambukizi ya virusi vya corona, baadhi waliugua na baadhi walifariki. Kwahiyo kwanini vitu kama hivyo vinatokea kwa waliochanjwa ."
Jibu ni kwamba hakuna chanjo inayoweza kukupatia ulinzi wa 100% dhidi ya kuumwa.
Lakini muhimu, iwapo utapata dalili, zinauwezekano mkubwa kuwa ni ndogo sana. Chanjo bado zinatoa ulinzi mkubwa dhidi ya kuugua sana na kuishia kulazwa hospitalini, hata kwa aina mpya zaidi za virusi.
Ingawa bado unaweza kupata virusi, unakuwa na uwezekano wa chini wa maambukizi. Na iwapo utapata Covid baada ya kuchanjwa, pia una uwezekano wa chini wa kumuambukiza mtu mwingine na hivyo kuwalinda watu wanaokuzunguka dhidi ya maambukizi.
Kuhusu chanjo na ujauzito
Eda, kutoka Uturuki ambaye aligundua kuwa ana ujauzito alisema: "Nilitaka kujipatia muda fulani[ Kabla ya kupata chanjo] ili kuangalia athari za chanjo ya Covid-19. Lakini nilipatikana na Covid-19, Nimegundua kuwa nina ujauzito wa wiki tano pia. Nilikuwa na wasi wasi sana kwa mtoto wangu mchanga, iwapo angeathiriwa ."
Ukweli ni kwamba wakati wa ujauzito, inaeleweka kabisa kwamba watu huwa waangalifu zaidi. Lakini data hadi sasa zinatupa hakikishi. Mamilioni wamechanjwa na hatujaona athari zozote za kutia wasi wasi zinazohusiana na ujauzito au uzazi bado.
Tafiti kubwa zimebaini kuwa wanawake wajawazito waliochanjwea hawawezi kuwa na uwezekano wa kupata matatztizo-ikiwa ni pamoja na uaviaji mimba-kuliko ambao hawajachanjwa.
Hatahivyo kuna hatari zinazoongezeka kwa watu wenye ujauzito iwapo watapata maambukizi ya Covid. Wale wanaopata virusi, husasan wale wenye ujauzito mkubwa, wana uwezekano mkubwa wa kuugua sana au kujifungua watoto kabla ya muda au watoto au kufariki kwa vijusi baada ya wiki ya 20 ya ujauzito.
Baadhi ya watu wana wasiwasi kwamba kupata chanjo kunaweza kuathiri uzazi wao siku zijazo-lakini hakuna ushahidi wa ushahidi au msingi wa kisayansi wa kusaidia kumini hili kuwa jambo la kweli.
Tunafahamu kuwa kuna athari za nadra sana za chanjo za Covid.
Hatari za muda mrefu za matatizo ya kiafya na kifo ni za kawaida zaidi kutokana na covid kuliko zinavyotokana na chanjo, hata miongoni mwa vijana wadogo.
Hilo ni muhimu kulifahamu, ili uweze kupima hatari hizo na faida wakati unapofanya uamuzi wa iwapo unataka kupata chanjo
Lakini kuna tofauti kubwa katika viwango uchanjaji wa chanjo za Covid-18 kote dunaini. Chini asilimia 10 ya watu katika nchi zenye kipato cha chini ndio waliochanjwa.
Usambazaji wa chanjo bado ni tatizo kubwa katika nchi nyingi. Lakini hata chanjo zinapokuwepo, wengi wana hofu ya kuchanjwa, kulingana taarifa ya Disemba 2021, ya taasisi ya- Our World in Data.