Je hamu ya kushiriki tendo la ndoa huisha mtu anapozeeka?

Claudia na Luis walikutana wachanga sana. Walijua mara moja kwamba waliumbwa kwa ajili ya kila mmoja wao. Mwanzo wa mlipuko wa mapenzi, hawakuweza kuacha kufikiriana mara kwa mara walitaka kukaribiana, walihitaji kufanya mapenzi mara kwa mara.

Wamekuwa katika maisha pamoja. Ingawa kumekuwa na matatizo ya kiafya, kimsingi wanatunzwa na kujituza vyema . Wao hutumia muda fulani katika kituo cha kulelea watoto karibu na Eneo jirani, hutembea pamoja na kusaidiana kazi za nyumbani.

Mara kwa mara, wao huwatunza wajukuu wao. Na bado wanaendelea kuvutiana! Sasa kwa namna tofauti, wakifurahia mapenzi yao na walivyo. Ni upendo wa hali ya juu kuwa na mtu unayempenda na kufurahia.

Ujinsia na usherati ni vipengele tofauti na vilivyojumuishwa katika tendo la ngono la binadamu. Katika kipindi chote cha maisha , imefunzwa na kuainishwa kuhusu raha ya maisha ya kila siku, ya mwili, ya kufurahiana, miongoni mwa wapendanao.

Wazee wana mahitaji sawa ya kutaka kupata raha na ustawi kama watoto, vijana na watu wazima, lakini ijapokuwa wana tabia ya kutofunikwa vizuri, haswa kwa wale wanaoishi kitaasisi, mapenzi yao hayaishi kwasababu ya umri.

Kusalia na hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa katika kipindi cha uzeeni kunapaswa kuwa haki ya kibinadamu na kiashiria muhimu cha ubora wa maisha

Njia ambayo kila mtu anahisi na kujieleza kama mwanamke au kama mwanamume ni ukweli wa kibayolojia ambao hudumu maisha yote, ndivyo walivyo kijinsia.

Raha haipungui kwasababu ya umri

Wazee wengi husalia kushirikia katika tendo la ndoa hatua inayoashiria kwamba , hamu ya tendo hilo na raha yake haipungui mtu anapozeeka.

IJapokuwa umri pekee haupaswi kuwa sababu ya kubadili viwango vya tendo la ndoa ambavyo vimefurahiwa katika kipindi chote cha maisha , inawezekana kwamba, mazoea inapofaa , kwa mapungufu fulani ya kimwili na madhara ya magonjwa au dawa yanapaswa kuzingatiwa.

Mabadiliko haya yatazungumziwa kwa uchache na hisia zinazohusiana na mhemko huathirika kidogo wakati mtu anaposhiriki tendo la ndoa. Mawazo, msisimko wa hisia, na visaidizi vingine vya kimazingira vinaweza kuongeza uwezo wa kupata raha.

Miongoni mwa wanaume, vipengele vinavyohusiana na kusisimka ndivyo vinavyoshauriwa zaidi, kupitia krimu za juu hadi viungo vya uume. Miongoni mwa wanawake, vipengele vinavyohusiana na ulainishi na vichochezi vya hisia kama vile manukato na nguo za ndani.

Hata hivyo, ni lazima kuzingatia kwamba kuna watu wazima ambao wanachagua kutoshiriki katika shughuli za ngono, na hilo pia ni jambo la kawaida.

Athari ya kuwa mjane

Maswala ya kisaikolojia na kijamii yanayoathiri jinsia kadri umri unavyosonga ni muhimu sana. Katika tamaduni nyingi, ngono inahusishwa na vijana na watu wazee wanaweza kuhisi kuhitaji kidogo, hali ambayo inaweza kuathiri vibaya utendaji wao wa tendo la ngono.

Kwa mfano, kuwa mjane kuna athari nyingi kwa afya ya kihisia na ya ngono, kwani watu ambao wamekuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu wa maisha yao wanaweza kutojua jinsi ya kudhibiti hisia zao za kimapenzi za muda mrefu.

Cha mno ni kwamba upendo wa raha hudumishwa katika maisha yote. Hatupaswi kusahau kwamba, sisi sote wakati mmoja tutakuwa wazee na kwamba tutahitaji kile ambacho tunataka: kama vile starehe, heshima, faragha na huduma ya makini ya mtu, bila kuingiliwa..