Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uchina yakanusha kuingilia katika siasa za Uingereza baada ya tahadhari ya MI5
Uchina imekanusha kuingilia siasa za Uingereza baada ya Idara ya usalama ya Uingereza MI5 kutoa tahadhari kuwa nchi hiyo imepenya na kuingia katika bunge.
Huduma za usalama zilisema kuwa Bi Christine Ching Kui Lee "alianzisha mahusiano" kwa ajili ya chama cha kikomunisti na wabunge wa sasa na wale wanaotarajia kuwa wabunge nchini Uingereza.
Halafu alitoa misaada kwa wanasiasa , akiwemo mbunge wa chama cha Labour Barry Gadner, ambaye alipokea zaidi ya pauni 420,000 kutoka kwake.
Ubalozi wa Uchina mjini London uliishutumu MI5 kwa " uchochezi na vitisho" dhidi ya jamii ya Wachina wa Uingereza.
Katika taarifa iliyochapishwa kwenye wavuti wa ubalozi huo, msemaji alisema: "China kila mara inaheshimu kanuni ya kutoingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine.
"Hatuna haja na hatujawahi kutaka 'kununua ushawishi' katika bunge lolote la kigeni. Tunapinga kabisa njama ya uchochezi na vitisho dhidi ya jamii ya Wachina Uingereza."
Kulingana na tahadhari iliyotolewa na MI5, Bi Lee alidai kuhusika kwake na bunge kulikuwa ni kwa lengo la "kuwakilisha Wachina Waingereza na kuongeza ushirikishwaji wa watu wa aina mbali mbali".
Lakini MI5 ilisema kuwa shughuli zake "zimekuwa zikifanywa na idara ya United Front Work Department [ya CCP], huku udhamini ukitolewa na raia wa kigeni wanaoishi nchini Uchina na Hong Kong ".
UFWD inadai kutaka " kuanzisha mahusiano" na "watu wenye ushawishi " kuhakikisha siasa za Uingereza zinapendelea CCP na kuwakosoa wale wanaoelezea wazi wazi kuhusu chama, ikiwa ni pamoja na juu ya haki za binadamu.
Huduma za usalama MI5 zilisema kuwa Bi lee alikuwa na " mawasiliano ya mara kwa mara na wanasiasa binafsi wa vyama vya kisiasa tofauti kote nchini Uingereza ", ikiwa ni pamoja na chama kilichovunjwa kwa sasa cha kikundi cha -All Party Parliamentary Group kilichoitwa Wachina nchini Uingereza( Chinese in Britain)
MI5 ilionya kuwa Bi Lee "anaweza kutaka kuanzisha APPG [makundi ya wabunge] kwa ajili ya kuendeleaza ajenda za to CCP".
Unaweza pia kusoma:
Mbunge wa Conservative na kiongozi wa zamani wa chama Sir Iain Duncan Smith aliwasilisha tahadhari yake katika bunge la Uingereza Alhamisi, akithibitisha kuwa imetumwa na Spika kwa wabunge kwa njia ya barua pepe.
Alisema kuwa lilikuwa ni "jambo la hofu kubwa", alitoa wito kwa Bi Lee kurudishwa Uchina na akiitaka serikali kutoa taarifa kwa Bunge.
Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Priti Patel alisema "inatia hofu kubwa " kwamba mtu fulani "ambaye alifahamika kuhusika katika uingiliaji wa siasa za Uingereza kwa niaba ya chama cha kikomunisti cha Uchina aliwalenga wabunge ".
Lakini alisema Uingereza ina hatua "za kutambua uingiliaji wa kigeni".
Bw Gardiner alianza kupata misaada kutoka kwa kampuni ya sheria ya Lee, Christine Lee & Co, mwishoni mwa mwaka 2014.
Mtoto wa kiume wa Lee pia alifahamika kuwa alijitolea kwa ajili ya kumsaidia mbunge wa labour na baadaye aliajiriwa kama meneja wa shajara.
Bw Gardiner, ambaye alikuwa mjumbe wa waziri kivuli wakati Jeremy Corbyn alipokuwa kiongozi wa chama cha Labour , alisema kuwa " amekuwa akiwasiliana na huduma zetu za usalama kwa miaka mingi " kumhusu Bi Lee.
Bi Lee ''hakuwa na jukumu" katika kazi aliyoteuliwa kama watafiti wake na misaada yote iliripotiwa ipasavyo'', alisema.
Bw Gardiner baadaye alikiambia kituo cha habari cha Sky News: "Kwa mtizamo wangu, pesa zile zilikuwa pale kuboresha kazi ambayo niliweza kuifanya katika bunge, na kuboresha kazi ambayo niliweza kuifanya kwa maeneo bunge yangu-ililipwa kwa wale watafiti na ililipwa kwao moja kwa moja, hakuna sehemu ya pesa hiyo iliyokuwa kwa ajili faida yangu binafsi ."
Kiongozi wa Liberal Democrat Sir Ed Davey pia alipokea msaafa wa 5,000 alipokuwa waziri wa nishati - lakini alisema kuwa pesa hizo zilikubaliwa na shirika la eneo na ilikuwa "mara ya kwanza kupata sababu ya kuwa na hofu ".