Wafahamu Wahispania waliovuka bahari ya Pasifiki kupitia njia ya wanaume watatu wenye hekima

Ilikuwa ni nyota iliyowasadikiza kwamba hatimaye wamepata kile walichokuwa wamekitafuta mara nyingi sana.

Lilikuwa eneo la Ophir, ambapo, kulingana na Biblia, ndio sehemu kubwa ya mawe ya thamani, fedha, pembe za ndovu, msandali na tani za dhahabu zilitoka ambazo Mfalme Sulemani (974-937 BC) aliweza kutimiza ahadi ya Mungu. kwa Daudi: ya kujenga hekalu la kuweka sanduku la Agano.

Katika kufuatia hilo, wanaume 150 walisafiri kwa meli mbili, moja yao iitwayo "Los reyes," kutoka bandari ya Callao nchini Peru.

Ilikuwa Novemba 19, 1567, na msafara huo ulijitosa kusini mwa hahari ya Pasifiki, eneo ambalo halikuwa limegunduliwa.

Walianza kukadiria kwamba baada ya kusafiri karibu maili 2,000 wangefika mahali wanakoenda, lakini ni hadi waliposafiri zaidi ya umbali huo mara tatu ndipo, Jumamosi, Februari 7 ya mwaka mpya, ndipo waliona mahali pazuri.

Walikuwa wamesafiri siku 81, lakini wangesubiri nyingine mbili kwa sababu hawakupata mahali pa kutia nanga hadi siku Jumatatu.

"Kisiwa kilizungukwa na kina kirefu na ungeweza kuingia tu kupitia mlango wa bahari. Kulingana na [Kapteni Álvaro de] Mendaña, wakati huo nyota ilionekana ambayo ilionyesha njia ya kusonga mbele," msomi na mwanafilolojia Juan aliiambia BBC.

Je, ni uthibitisho gani bora zaidi kwamba walikuwa wamefika kwenye kisiwa cha Mfalme Sulemani na Mamajusi kuliko kuona nyota yenye kung'aa kama ile iliyowaongoza Melchior, Gaspari na Baltasar kwenye safari yao kwenda Bethlehemu?

Kwenye pwani nyingine

Ingawa haiko eneo sahihi, Ophir ya kibiblia inaonekana mara kadhaa katika kitabu kitakatifu.

Kwa hiyo kwa Wazungu hakukuwa na shaka kwamba ilikuwepo, na kwa kila uchunguzi mpya tumaini la kuipata lilizaliwa upya.

Baada ya kukosa Afrika, ndoto hiyo ilihamia magharibi, na kugundua kuwa kuna walimwengu wengine upande huo.

"Christopher Columbus alidhani aliipata kwenye Hispaniola, na mengine yote yalikuwa kufuata baada ya Columbus," anasema Gil.

Magharibi zaidi

Lakini kufikia katikati ya karne ya 16 uvumi ulikuwa pia ukienea kwamba katika Pasifiki, karibu na ufuo wa Milki ya Inca ya kale, kulikuwa na visiwa vyenye utajiri mwingi, ambavyo ilikisiwa kuwa vile vya Kibiblia vya Mfalme Sulemani.

Hii ilichanganywa na nadharia ya Pedro Sarmiento de Gamboa (1532-1592), askari na baharia wa Uhispania, ambaye aliamini kuwa jamii hii iliyoendelea sana na tajiri haikuwa asili ya Peru lakini ilitoka nchi iliyokuwa magharibi ambayo wavumbuzi hawakuweza kuipata kwa sababu walikuwa wamefuata upepo na mawimbio yaliyokuwa mbali sana kaskazini.

Mawazo yake yalimshawishi Don Lope García de Castro, ambaye aliunga mkono wazo la safari ya uchunguzi, lakini alitaka mpwa wake, Álvaro de Mendaña de Neira, 25, kuiongoza, huku Sarmiento akiwa wa pili katika uongozi .

Hivi ndivyo msafara ulivyoanza, ambao ulienda kutafuta kile kilichopotea kwa muda mrefu katika bahari ambayo haijawahi kuvukwa.

Na kisiwa walichofika kiliitwa Santa Isabel de la Estrella, jina la muongoza safari na nyota ambayo iliwaongoza.

Licha ya ishara nzuri, kukaa kwenye kisiwa hicho ilikuwa ngumu sana hivi kwamba miezi mitatu baadaye, baada ya kutengeneza meli, wafanyakazi walipiga kura ya kurudi Peru.

Ingawa walifika wakiwa na hadithi za eneo la kigeni ambalo hadi wakati huo halikuwa linajulikana kwa watu wa nchi yao, hawakuleta utajiri uliotamaniwa, kwa hivyo Mendaña alisifiwa kidogo kwa kile kilichochukuliwa kuwa safari iliyofeli.

Lakini hilo halikupunguza hamu ya kurudia safari hiyo, ila tu aliporudi, Gil anasema, "alikuta nafasi ya mjomba wake ilikuwa imechukuliwa na Makamu Don Francisco de Toledo, ambaye alikuwa hawelewani.

Ilichukua karibu miaka 30 kabla ya kurudi.

Janga

"Kufikia wakati huo, Mendaña alikuwa mzee na hangeweza kujilazimisha kwa wanaume wake," asema Gil, ambaye alihariri kitabu "In demand of the King Solomon", kitabu ambacho kina masimulizi ya safari tatu zilizofanywa visiwani wakati huo.

Zaidi ya kumbukumbu, ambayo inazungumzia kwa kina safari, mwendo, kasi na ajali mengine ripoti ya kile kilichotokea.

Sauti kuu ni ya Pedro Fernández de Quirós, ambaye alikuwa rubani katika msafara wa pili wa Mendaña, 1595-1596, ambaye dhamira yake ilikuwa ni kuanzisha koloni katika visiwa vya Solomon, hivyo meli hizo nne zilibeba wanaume, wanawake na watoto 378 ( akiwemo mke wa Mendaña na wanafamilia wengine).

Hatimaye, ugonjwa wa homa ulichukua maisha ya Mendaña, na amri ya meli ikaanguka kwa Quirós. Lakini si kwa muda mrefu.

"Wakazi wa kisiwa hicho, ambao walikuwa wajasiri sana, walikuwa wakiwapa Wahispania mengi ya kufanya. Hapo awali walifurahi sana kuwaona Wahispania, lakini walipogundua wanataka kubaki walipinga wazo hilo."

Quirós, licha ya kila kitu, alitaka kukabaki, "lakini ilionekana kuwa haiwezekani kwa watu wake, kwa hiyo wakamfungia ndani ya chumba chake na kuchukua meli kurudi Acapulco."

"Meli zingine zilikwenda Nueva Guinea na Manila, chini ya amri ya mke wa Mendaña, Isabel Barreto, ambaye alikuwa amerithi jina la mapema mkuu wa safari ya baharini, ambaye mapema alikuwa na serikali ya nchi alizoziteka) " .

Miaka 9 baadaye ...

Mnamo 1605 Quirós alifanikiwa kupata mfalme wa Uhispania kufadhili msafara mwingine, wakati huu kwa madhumuni ya kutafuta na kuteka Terra Australis , bara ambalo kulingana na mwanafalsafa wa Ugiriki Aristotle, linapaswa kuwepo kwa sababu Dunia ilipaswa kuwa na usawa.

Katika safari hii aliandamana na mwandishi mwingine wa ripoti zilizojumuishwa "In demand of the island of King Solomon": Diego de Prado, ambaye, kama bara waliloenda kutafuta, anapingana na toleo la Quirós.

"Wao ni mahusiano mawili tofauti sana: Prado ni mwazi na mwenye furaha zaidi. Kwa mara ya kwanza, unaweza kusikia Wahispania na watu wa kiasili wakicheka kwa sauti kubwa , kitu cha ajabu kwa sababu kwa ujumla katika mahusiano ya Kihispania, machache sana husemwa kuhusu hisia. "Gil anasema.

"Anasema kwamba baada ya chifu wa watu wa asili wa Nueva kuona jinsi Wahispania walivyoua nguruwe, alijaribu kuwaiga, lakini badala ya kupiga risasi, alichofanya ni kelele: boom! Na watu wote wa asili wakaanza kucheka.

"Katika tukio jingine, Wahispania walikuwa wakijiandaa kwa sababu walidhani wenyeji wa eneo hilo wangewavamia ghafla waliona ndege fulani wakinyanyuka na hawakuweza kujizuia kucheka walipoona kundi la ndege limewatisha".

Ingawa wazo lilikuwa kusafiri kusini, katika kutafuta bara hilo la kusini, "Quirós alipofikia digrii ishirini ya latitudo ya kusini, alikata tamaa."

"Alikuwa mtu wa ajabu sana; huwezi kuona kwa nini hakuendelea na msafara alioahidi. Na katika hadithi yake, Diego de Prado anasema kwamba wakati huo: 'Kusini unaweza kuona mawingu matatu makubwa sana, mawili kati ya mawingu yalikuwa meupe na moja leusi."

"Bila shaka," Gil anasisitiza, "Watu Watatu Wenye Hekima: wawili weupe na mmoja mweusi."