Fahamu mkakati wa vita vya siku zijazo vya mataifa yenye nguvu zaidi duniani, nchi za Magharibi ziko tayari?

Jaribio la

Chanzo cha picha, GIANCARLO CASEM / US AIR FORCE

Maelezo ya picha, Jaribio la ndege ya BH Stratofortress ya makombora ya hypersonic California

Mwaka uliopita tulishuhudia mabadiliko makubwa katika sera ya ulinzi na usalama ya Uingereza. Bajeti kwa ajili ya teknolojia ya digitali , intelijensia bandia na teknolojia ya mtandao iliongezwa.

Bajeti kwa ajili ya silaha za kawaida na vikosi vya kawaida ilipungua.

Yote hayo yalikuja wkati vikosi vya Urusi vinakusanyika kwenye mpaka wa Ukraine, Urusi pia ilitoa wito wa kuondolewa kwa vikosi vya NATO katika mataifa wanachama wa NATO , na Uchina imepaza sauti yake kuhusu kukamatwa tena kwa Taiwan-ikiwezekana kwa nguvu.

Mizozo midogo ya kikanda pia imejitokeza katika baadhi ya maeneo ya dunia.

Ethiopia iko katika mzozo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe , huku zaidi ya watu sita wakiuawa katika mzozo wa kujitenga wa Ukraine, uasi unatokota katika Syria na wanamgambo wa Kiislamu wanafanya mashambulio katika baadhi ya maeneo ya Afrika.

Lakini je vita vipya baina ya mataifa yenye nguvu zaidi vitakuwaje?, na je mataifa ya magharibi yataweza kuhimili changamoto za kivita zijazo?

Dalili za vita vijavyo tayari zipo. Viashiria vingi vya vita vikuu baina yan chi za magharibi na, kwa mfano Urusi au Uchina , vinaandaliwa na vikosi vinapelekwa kwenye maeneo ya vita.

Novemba 8, Urusi ilifanya jaribio la ufyatuaji wa roketi katika anga za mbali, na kuangamiza mojawapo ya setilaiti zake.

Katika msimu wa kiangazi, Uchina ilifanya jaribio la kombora lake la kisasa zaidi la aina ya supersonic missile, linalosafiri kwa kasi ya haraka ya mara kadhaa kuliko kasi ya sauti. Mashambulio ya kimtandao, uharibufu na uvamizi, unatokea kila siku, haya ni mambo hayahesabiki kama vita halisi lakini yanaendelea kufanyika.

Chini ya utawala wa marais wa zamani wa Marekani Clinton na Obama, Michelle Flournoy alikuwa mkuu wa idara ya Mkakati kitengocha ulinzi. Anaamini kwamba kwa miongo miwili iliyopita huku matafa ya magharibi yakielekeza juhudi zao zote katika mashariki ya kati, mahasimu wao waliweza kupata mafanikio makubwa ya kijeshi.

Alisema: '' Sisi hufanya mabadiliko ya mkakati, huku tukiwa katika jukwaa moja linaloitwa Marekani, Uingereza na washirika wetu- kabla ya kufanya kazi kwa miaka ishirini katika mapambano dhidi ya ugaidi, vita vya Iraq na Afghanstan na sasa.

Tuanafahamu kuwa tunakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa mataifa yenye nguvu zaidi. Bila shaka alikuwa akimaanisha Urusi na Uchina. Na tathmini ya serikali ya Uingereza pia ilitaja tisho kubwa na mahasimu wa muhula mrefu wa mkakati.

SpaceX Utopia, chombo ambacho hubeba setilaiti bandia kwa ajili ya US Air Force, kikipaa kutoka ngome ya Kennedy Air Force Base katika Florida.

Chanzo cha picha, PERSONNEL WITH THE 175TH CYBERSPACE OPERATIONS GRO

Maelezo ya picha, SpaceX Utopia, chombo ambacho hubeba setilaiti bandia kwa ajili ya US Air Force, kikipaa kutoka ngome ya Kennedy Air Force Base katika Florida.

Michelle alisema : '' Huku tunaelekeza juhudi zetu kaika Mashariki ya kati, kilichopo katika mataifa mengine makubwa ni kuendelea kwa msururu wa uwekezaji katika teknolojia mpya za kijeshi.

Mwingi kati ya uwekezaji umejikita katika mashambulio ya uharibifu wa kimtandao kwa lengo la kuichafulia sifa jamii ya nchi za Magharibi , kushawishi uchaguzi na kuiba taarifa za siri.

Zote hizi ni aina shuguli za kivita, ambazo hazihesabiki katika vita a nyingi zinaweza kukanwa na mtekelezaji kwa urahisi.

Hatari kubwa sana ya kijeshi hapa ni kuongezeka kwa uhasama. Kama mawasiliano ya setilaiti yako hayako vyema na makamanda wako wa mipango wako chini ya ardhi na hawajui ni nini kinachoendelea, itakuwa vigumu sana kwao kuamua kuhusu hatua inayofuata.

Kigezo kimoja kitakachokuwa na nafasi kubwa sana katika vita vya siku na akili bandia.

Hii inaweza kupunguza muda wa kujibu mashambulio na kuharakisha maamuzi ya makamanda wa vita, na hivyo kuwawezesha kupokea taarifa kwa kasi zaidi.

Unaweza pia kusoma:

Tisho la Urusi na Uchina

Kutokana na hili, Marekani imeweza kulichukulia hili kama moja wapo ya faida yake dhidi ya mahasimu wake, na Michel Fleur anaamini kuwa faida hii itaondoa tatizo la kupunguza vikosi va magharibi wakati Uchina ikiongeza uwepo wake wa kijeshi.

Lakini kuna eneo moja ambapo nchi za Magharibi liko nyuma sana ya Urusi na uchina. Eneo hili ni la teknolojia ya makombora ya kasi na hatari ya hypersonic missiles - makombora haya yanaweza kulipua mara tano zaidi ya kasi ya sauti na kubeba silaha za kawaida na za nyuklia kwa pamoja.