Juan Jose Florian: 'Bomu lililokaribia kuniua lilikuwa zawadi ya maisha'

Juan Jose Florian

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Florian nusura auawe na bomu lililomlenga kufuatia kutoroka kwake kutoka Farc

Nyumba ya utotoni ya Juan Jose Florian ilikuwa sehemu ya eneo la msitu wa Colombia. Familia yake ilijipatia riziki kwa kulima mapapai, machungwa na parachichi. Lakini usiku eneo hilo lilikuwa la makundi haramu yenye silaha.

Wale waliyokaidi amri ya kutotoka nje iliyowekwa, walifungwa kamba usiku kucha au wanaokamatwa mara ya pili waliuawa. Maiti ilionekana kila siku katika msitu ulio karibu.

Hakukuwa na barabara wala televisheni ambazo watoto wangeweza kufuatilia timu za mpira wa miguu. Florian na kaka yake mkubwa Miller wangeweza kujificha na kutazama moto wa tracer uliowaka angani usiku, ukishangilia jeshi la Colombia katika mzozo wao na Farc - Kikosi cha Wanajeshi wa Mapinduzi ya Colombia - na vikundi vingine vya waasi.

"Wanajeshi walipokuwa huku, tungelicheza nje hadi usiku, watoto wa shule walikuwa salama dhidi ya usajili wa lazima wa makundi ya waasi," Florian anasema.

Wapiganaji wa kundi la Farc - lililobuniwa mwaka 1966 na kuvunjwa 2016, wakati mkataba wa kusitisha vita ulipotiwa saini- walikuwa wageni wa kawaidi katika boma la familia yao, wakitaka chakula , pesa na mengine mengi.

Florian in training, accompanied by his wife Angie

Chanzo cha picha, Getty Images

Florian na kaka yake Miller waliamua kuwa wanajeshi walipokuwa wakubwa. Miller alipokuwa na umri wa miaka 23, alisafiri hadi mji wa karibu, kuwasilisha hati zake kwenye kituo cha ukaguzi lakini aliambiwa kwamba alikuwa amechelewa kujiunga na utumishi wa kijeshi wa lazima. Hakulalamika.

Wiki kadhaa baadaye, kikundi cha askari wa Farc kilitembelea familia ya Florian katika eneo lao la pekee la msitu wakiwa na ujumbe. Familia ilikuwa imemtoa mtoto wa kiume kwa vikosi vya serikali, walisema, kwa hivyo walikuwa na deni la mwingine kwa vikosi vya mapinduzi

"Mama yangu alijaribu kujadiliana nao. Aliwarai sana. Wakati waliponichukua, alinibariki huku machozi yakimlenga," anasema Florian.

Hivyo ndivyo Florian - aliyekuwa na umri wa miaka 16 mwaka 1998 - alivyoingizwa kwenye mzozo uliyowaua watu 260,000 na kuwaacha wengine zaidi ya milioni sita bila makao na kuwa wakimbizi wa ndani kati ya mwaka 1954 na 2016.

Alikuwa mmoja wa zaidi ya watoto 18,000, asilimia 70 wakiwa chini ya miaka 15, walioajiriwa na Farc wakati wa miongo yao mitano ya mapambano ya silaha kama kundi kubwa la waasi nchini humo.

"Tulikabiliwa na shinikizo la kisaikolojia kwa masaa," Florian anasema. "Maadili waliyofundisha yalikuwa kinyume na ya mama yangu. Siku zote nilikuwa nikifikiria juu ya kutoroka kwangu. Nilitumia siku zangu kuangalia, kusikiliza, kupanga. Niliona jinsi watoro walivyopigwa risasi kwa sababu ya usaliti."

Lakini Florian alipinga mafundisho yao na, mwaka mmoja katika maisha yake kama mpiganaji wa msituni, alipata fursa yake ya kutoroka.

Florian na mke wake Angie wanaonyesha picha yake akiwa mwanajeshi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Florian na mke wake Angie wanaonyesha picha yake akiwa mwanajeshi

Kikosi chake cha 27, kilitumwa kushambulia kituo cha polisi. Jeshi lilituma helikopta kujibu mashambulizi..

"Walituona na kuanza kutupiga risasi," anasema. "Nilijificha chini ya majani ya mti. Wakati helikopta iliyokuwa juu yangu ikizunguka mti huo."

Wenzake walipotoroka, Florian alivamia nyuma ya shambani na kuwapata ghafla wakazi wake - mwanamume na mke wake.

"Kulikuwa na wafuasi wengi wa Farc katika sehemu hizo, na walipata fadhila ikiwa wangekabidhi waliotoroka, kwa hivyo nikasema, 'Atakayejaribu kufanya hivyo nitampiga risasi.

"Niliwaambia nataka nguo. Mwanamume huyo alinipatia suruali ya jeans na shati nyeupe.Nilimuamrishafanya yeye na mke wake walale sakafuni na, kwa kutumia mkono mmoja, nilibadilisha magwanda yangu ya kivita. Nilopomaliza nikatoka mbio nje ya nyumba.

"Nilipata vizuizi vya kijeshi barabaranina hapo nikarusha silaha zangu na kuinua mikono kuelekea kwao. Niliwaambiaafisa mmoja kwamba nilikuwa mpiganaji lakini nataka kujisalimisha. Nilimwambia sijala chakula kwa siku kadhaa. Walinipatia chakula nikawasimulia kisa changu. Waliniuliza kaka yangu alikuwa kwenye kikosi gani. Kwa bahati nzuri kaka yangu alikuwa ameripoti kuandikishwa kwangu kwa lazima, na walithibitisha kuwa mimi ndiye niliyedai kutekwa."

Florian aliwekwa chini ya ulinzi wa kijeshi katika mji mkuu wa Bogota.

"Niliogopa kwenda mitaani endapo wangenikuta," anasema. "Ilikuwa ya kutisha. Nilikuwa mdogo sana na nilikuwa na adui mkubwa na mwenye nguvu."

Kwetunyumbani, mama yake alilazimika kukimbia shamba na watoto wake wengine, ambao aliwapeleka shule ya bweni kwa usalama wao.

Florian alipofikisha miaka 18 mwaka 2000 alijiunga na jeshi la Colombia. Baada ya mafunzo yake alitumia miaka 12 kupambana na kampeni dhidi ya magenge ya dawa za kulevya na walanguzi wa mafuta.

Kaka yake Miller aliendelea na kazi yake ya kijeshi, lakini alijeruhiwa katika majibizano ya risasi na Farc katika mji wa El Dorado, Meta, takriban kilomita 350 kusini-mashariki mwa Bogota.

Florian alisafiri nyumbani kwenda kumuona. Mama yao alikuwa ameuza shamba na kukata kulipa kodi ya lazima inayotozwa na Farc. Walimsaka hadi makazi yake mapya. Mnamo Julai 12 mwaka 2012 wapiganaji hao waliwavamia

Florian training at home

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Florian alikuwa bingwa wa mbio za baiskeli za para-baiskeli wa Colombia mnamo 2021

Florian anasema:"Nakumbuka kuona maandishi karibu na mlango. Nilijongea kuona kilichoandikwa, nilipochuchumaa na kunyoosha mikono yangu. Kitu ninachokumbuka ni kulala chini nikipiga kelele. Mikono yangu yote miwili ilikuwa imetoweka.

"Mguu wangu wa kulia ulikuwa umekatwa juu ya goti.Nilikuwa nimechomeka vibaya sana kila mahali. Jicho langu la kulia lilikuwa limetoweka, Nilikuw ana matatizo ya kusikia upande wa sikio la kulia. Kaka yangu alikuwa akinikumbatia, nami nilikuwa nikilia kwa sauti, 'Niue. Nipige risasi. Siwezi kuishi hivi.'

Florian alizinduka baada ya siku 12 baada ya kukosa fahamu. Miezi ya upasuaji na kupandikizwa kwa ngozi. Hisia zake zililemewa na mfadhaiko, maono na mawazo ya kujiua.

"Nilitamani kujitoa uhai kwa kujirusha kupitia dirishani au kutoka kwenye ngazi,"anasema. "Lakini nikajiuliza, 'Je nikishindwa, na na hali yangu ikiishia kuwa mbaya zaidi?' Niliamua kujifunza kutembea ili niweze kujirusha mbele ya gari.

Baada ya miezi kadhaa katika uangalizi wa karibu, na maneno mengi ya huruma, alipata bahati ya kuhamishiwa kwa Kikosi cha Kibinafsi cha Jose Maria Hernandez, kikosi maalum katika Jeshi la Colombia kwa wale waliopata kiwewe kutokana na vita.

"Nilichoka kuonewa huruna, lakini nilijipata nikitabasamu kutokana na upendo nilioneshwa na jinsi nilivyotaniwa na wenzangu," Florian anasema. "Maafisa wengine walikuwa wakiniita 'Robo Kuku. Waligusa mashina yangu, wakanicheka. Tulitishiana kwa kupigana ngumi, lakini hakuna aliyekuwa na ngumi! Nilifufuka na kufarijika kuwa miongoni mwao."

Juan Jose Florian

Chanzo cha picha, Getty Images

Kama sehemu ya matibabu yake, Florian alianza matibabu ya maji. Vikao vya kikundi hvikageuka kuwa vya ushindani.

Aligundua kuwa angeweza kushikilia pumzi yake chini ya maji kwa muda mrefu zaidi kuliko wenzake, na kuwashinda katika uogeleaji wa bwawa. Alianza kujiwekea wakati na kuboresha nyakati zake.

Katika mchezo huo alipatana na raia waliojeruhiwa katika ajali ya barabarani au kuathiriwa na ugonjwa, wakishindana na ligi ya Bogota ya uogeleaji wa walemavu. Florian alianza kuwakilisha timu ya jeshi katikamchezo wa uogeleaji.

Florian alishinda medali yake ya kwanza nchini Marekani katika hafla iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Minnesota mwaka wa 2013.

Alishinda medali yake ya mwisho katika michezo ya kitaifa mwaka wa 2015. Mwaka uliofuata, alipewa pensheni kutoka kwa jeshi na kuanza kusomea shahada ya saikolojia ya chuo kikuu. Hakuwa na uwezo tena wa kushindana katika timu ya kijeshi ya kuogelea, lakini aliamua kufuata matamanio mengine ya michezo.