Richard Moore: Kwanini mkuu wa ujausi Uingereza anasema "China, Iran na Urusi ni tisho kwa usalama wake''

MI6 headquarters in London

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Makao ya shirika la ujasusi la Uingereza MI6 mjini London

Mkuu wa shirika la ujasusi la Uingereza MI6 anasema Uchina na Urusi ni tisho kwa Uingereza na kwamba kutwaliwa kwa Kabul na Taliban ilikuwa ni "kushindwa kwa ujasusi ".

Richard Moore, ambaye ni mkuu wa shirika ujasusi la Uingereza MI6, ambalo linafahamika pia kama 'C', ameiambia BBC Radio 4 kwamba deni la Uchina na mtandao wa data vina uwezekano wa kuwa tisho kwa uhuru wa nchi hiyo na usalama wake. Na hatua za ulinzi zimechukuliwa kutokana na hilo.

Katika hotuba yake ya uzinduzi katika Taasisi ya kimataifa ya masomo ya stratejia - International Institute for Strategic Studies (IISS) Jumanne baada ya kuchukua wadhifa huo Oktoba mwaka jana, Bw Moore alikuwa akielezea masuala yanayoikabili idara ya ujasusi ya MI6 katika enzi hii ya digitali. Alisema kuwa uamuzi wa kuzungumza wazi kuhusu kazi ni muhimu katika demokrasia ya dunia ya leo.

Alielezea uwezo wa Uchina wa kupata mikopo na data za nchi nyingine kama tisho la amani ya dunia. Alielezea hatua ya Uchina ya kusema kuwa ina "uwezo wa kupata taarifa(data) kutoka maeneo yote ya ''dunia" na kwamba inawaingiza kwenye mtego watu kwa kuwapatia pesa za mkopo. Uchina inajaribu kushawishi nchi kupitia sera zake za uchumi na nadhani wakati mwingine watu hunaswa kwenye mtego huo," alisema.

Alizungumzia kuhusu Muungano wa Marekani, lakini akasema kwamba kubakia na kiasi fulani cha uhuru ni muhimu kwa Uchina. Utapoteza baadaye udhibiti wa data hizi "Uingereza inaelewa fikra kuhusu hili na tunachukua hatua za kulinda hili ," alisema.

Akiikosoa Urusi, Bw Moore alisema, ni muhimu kwa mataifa ya magharibi kuzungumza kwa kauli moja dhidi ya hatua za taifa kama vile Urusi kuipa sumu Salisbury na uungaji mkono wa kisiasa unaowayumbisha Wabalkan.

Mkuu huyo wa shirika la ujasusi la Uingereza MI6, ambaye alikuwa akizungumza kuhusu mada mbali mbali katika mahojiano alizungumzia kuhusu uvamizi wa Taliban nchini Afghanistan ambapo alikiri pia kwamba makadirio yake kuhusu kasi ya kusonga mbele kwa Taliban hayakuwa sahihi, lakini kutwaliwa kwa Kabul hakukuufanya ujasusi ushindwe.

"Hakukuwa na mtu hata mmoja aliyebashiri kukamatwa haraka kwa aina ile kwa Kabul,"alisema.

"Hatakama tulimpatia kazi kila mjumbe wa kikundi cha Ashura cha Taliban kama wapelelezi wa siri, tusingebashiri kutekwa mara moja kwa Kabul, kwasababu Taliban hawakujua hilo ," alisema.

Kulingana na mkuu wa ujasusi wa Uingereza, shirika lake MI6, litatakiwa kujiondoa ''kivulini'' ili kufanya kazi zake za siri vyema.

Richard Moore, anasema kwamba kujumuisha akili bandia, na teknolojia ya kidigitali kumebadilisha pakubwa jinsi ya upatikanaji wa ujasusi.

Data za kibayometriki na teknolojia ya utambuzi wa sura imefanya kazi ya majasusi kuwa ngumu huku watu wakifichautambulisho wao na kujilinda.

Richard Moore

Chanzo cha picha, Foreign and Commonwealth Office

Maelezo ya picha, Katika enzi yateknolojia ya digitali, upatikanaji wa ujasusi wa binadamu sio suala tu la MI6.

Septemba mwaka jana, ilifichuliwa kuwa kuna mafunzo ya MI6 kwenye makao makuu mjini London Septemba mwaka jana, ambapo kifaa kipya kilianzishwa cha kulinda usalama wa majasusi wa Uingereza na siri.

Richard Moore, ambaye amekuwa katika MI6 kwa miaka 34 , aliiambia hadhira kwamba zaidi ya kuwa wazi kwa MI6, kutakuwa na haja ya kushirikiana na sekta binafsi kupata teknolojia mpya. Anasema teknolojia ya habari za kinadhari na kivitendo pamoja na ya kibaiolojia kwa pamoja vitabadili sekta zote.

Unaweza pia kusoma:

Maendeleo katika teknolojia yatavutia watu waovu kama vile majasusi wa taifa na makundi ya ugaidi ya kimataifa. Alisema kuwa anapata mshahara wake kwa ajili ya kubaini hatari.

Vitisho kwa usalama wa taifa la Uingereza

Richard Moore anaorodhesha mataifa ya China, Russia, Iran na ugaidi wa kimataifa miongoni mwa vipaumbele vinne vya ujasusi wa ulimwengu wa kimagharibi . "Wapinzani wetu wanatumia bila kuchoka utajiri kupata intelijensia bandia , kompyuta zinazonasa ujasusi kwa njia ya nadharia na vitendo pamoja na teknolojia ya kibaiolojia, ambayo inawanufaisha," alisema.

Mashirika matatu ya ujasusi ya Uingereza, MI6, MI5 na GCHQ, yana jukumu la kukusanya ujasusi kutoka kwa watu wanaolengwa nje ya nchi hiyo kwa ajili ya usalama wa taifa.

Mkuu wa MI6, shirika ambalo hufanya kazi zake nyingi kwa kutumia mbinu za zamani za ujasusi, alitaja baadhi kazi ambazo MI6 inapaswa kufanya. Kwa mfano, wakati wa vita ya pili ya dunia, kubuni pesa za kidigitali -cryptocurrencies kulijumuisha juhudi za MI6 , teknlojia mbayo baadaye ilikuja kufahamika kama Wireless na secure speech.

Akili bandia na teknolojia ya kidigitali vimeleta mageuzi katika upatikanaji wa ujasusi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Akili bandia na teknolojia ya kidigitali vimeleta mageuzi katika upatikanaji wa ujasusi

Anasema MI6 kwa sasa ni mojawapo ya wajumbe waasisi wa kikosi cha Uingereza cha kupambana na uhalifu wa kimtandao , ambacho lengo lake ni kuzuia ugaidi, wahalifu na vitisho vingine na kusaidia jeshi katika operesheni zake.

Hotuba ya mkuu wa MI6 huenda ikawa kuchelewa kukiri kwa shirika hilo kwamba iwapo MI6 haiendelea kuwa macho, itabaki nyuma ya mahasimu wake katika enzi hii ya teknolojia.

"Hatuwezi kuepuka teknolojia ya dunia, kwahiyo tunapaswa kuitumia yake ," alisema.