Vita vya Afghanistan: Matano ya kujifunza tangu shambulio la 9/11

US troops in Afghanistan in 2003

Chanzo cha picha, Frank Gardner

Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Marekani waliondoa wanamgambo wa al-Qaeda na Taliban haraka sana kutoka Afghanistan mwaka 2003, lakini kwanini vita hivyo vimechukua muda mrefu?

Nini cha kujifunza, kama kipo, katika kipindi cha miaka 20 ya kupambana na ugaidi ulimwenguni kote? Kipi kimefaulu au kutofautu? Na leo hii, wakati Afghanistan inadhibitiwa tena na kundi ambalo wakati fulani lilikuwa na ushirikiano na lile la al-Qaeda, je tuna busara zaidi kuliko tulivyokuwa asubuhi ile ya Septemba 11, 2001?

Kwa Marekani mshtuko uliokumba Marekani kutokana na shambulizi mbaya zaidi la kigaidi kufanyika nchini humo, ulimwengu ulionekana na wengine kwa ukosoaji mkali. Kulikuwa na watu wazuri dhidi ya watu wazuri. "Kila taifa, kila mkoa," rais George W. Bush alisema, siku tisa baada ya mashambulizi ya 9/11, "sasa ana uamuzi wa kufanya. Au wewe uko pamoja nasi ama wewe uko pamoja na magaidi. "

Na kile kilichojulikana kama "Vita dhidi ya ugaidi". Tangu wakati huo kimesababisha uvamizi wa Afghanistan, kisha Iraq, kuchipuka kwa Isis na kuenea kwa maelfu ya waasi wanaoungwa mkono na Iran kote Mashariki ya Kati, vifo vya maefu ya wanajeshi, wanawake na raia wengi wa kawaida.

Ugaidi haujatokomezwa - kila nchi kuu ya Ulaya imekumbwa na mashambulio katika miaka ya hivi karibuni - lakini kumekuwa na mafanikio pia.

Hadi hii leo, hakujawahi kutokea shambulio linalokaribia kiwango cha shambulizi la 9/11.

Kambi za Al-Qaeda huko Afghanistan ziliharibiwa, viongozi wake waliwasaka Pakistan.

Ukhalifa wa Isis waliojitangazia uliotisha sehemu nyingi za Syria na Iraq umesambaratishwa.

Orodha inayofuata haina shaka yoyote ni yenye guzua gumzo.

Imezingatia uchunguzi wangu mwenyewe wa kufuatilia suala hili kote Mashariki ya Kati, Afghanistan, Washington na Guantanamo Bay.

1. Kushirikishana taarifa muhimu za kijasusi

Dalili zilikuwepo lakini hakuna mtu aliyeunganisha alichokiona kwa wakati.

Katika miezi iliyotangulia hadi 9/11, mashirika mawili ya kijasusi ya Marekani, FBI na CIA, yote mawili yalikuwa yakijua kuwa aina fulani ya njama ilikuwa ikiendelea.

Lakini huo ndio ulikuwa uhasama kati ya ujasusi wa ndani na nje ya nchi kwamba walibana taarifa za kile walichojua kwao wenyewe.

Tangu wakati huo, Ripoti ya Tume ya 9/11 imetatiza sana katika suala la kupitia makosa yaliyofanywa na maboresho makubwa ambayo yamefanywa vilevile.

Kutembelea Kituo cha Kitaifa cha Kukabiliana na Ugaidi (NCTC) huko Virginia mnamo mwaka 2006, nilionyeshwa jinsi mashirika 17 ya Marekani sasa yanavyochangia kila siku kulingana na taarifa walizonazo za ujasusi.

Uingereza ilianzisha kituo chake: Kituo cha Pamoja cha Uchambuzi wa suala la Ugaidi (JTAC) ambapo wataalamu kadhaa kutoka MI5, MI6, sekta ya Ulinzi, Uchukuzi, Afya na maeneo mengine wote wanakaa pamoja ndani ya jengo moja huko London, wakitoa tathmini yao endelevu juu ya vitisho vya ugaidi vinavyoendelea dhidi ya raia wa Uingereza nyumbani na nje ya nchi.

The city of Manchester mourned bombing victims in 2017

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mji wa Manchester uliomboleza waathirika wa shambulizi la bomu mwaka 2017

2. Tambua lengo lako na usikubali chochote kukutatiza kifikra

Kati ya sababu nyingi ambazo Afghanistan imerudi kwa utawala wa Taliban, moja ni dhahiri: uvamizi ulioongozwa na Marekani dhidi ya Iraq mnamo mwaka 2003. Uamuzi huu mbaya ulikuwa usumbufu mkubwa kwa kile kilichokuwa kikiendelea huko Afghanistan.

Vikosi Maalum vya Marekani na Uingereza, ambavyo vilikuwa vimefanikiwa kuwinda shughuli za al-Qaeda na kufanya kazi na washirika wa Afghanistan kuwazuia waasi wa Taliban kwa kujilinda dhidi yao, waliondolewa na kupelekwa Iraq badala yake.

Hii iliruhusu Taliban na wengine kujipanga tena na kurudi wakiwa na nguvu.

Mnamo mwezi Novemba mwaka 2003, wakati nilitembelea kituo cha watoto wachanga cha Marekani katika mkoa wa Paktika wa Afghanistan, Wamarekani walikuwa tayari wakielezea kazi yao huko kama "Iliyosahaulika."

Ni rahisi sana kusahau kuwa msingi wa ujumbe wa Afghanistan ulikuwa wazi na ulitekelezwa vizuri.

Baada ya watawala wa Taliban kukataa kuwakabidhi wahalifu, Marekani iliungana na Muungano wa Kaskazini (Waafghani wanaopinga Taliban) kufanikiwa kuwafukuza Taliban na al-Qaeda vilevile.

Lakini katika miaka iliyofuata, nguvu ya ujumbe huo ikapungua, na kuzungukwa kwa njia nyingi.

3. Mchague mshirika wako kwa makini

Ushirikiano wa Uingereza na mshirika wake wa karibu, Marekani, katika uvamizi wa Iraq wa mwaka 2003, ilimaanisha kuwa Uingereza ilikuwa mshirika mdogo katika karibu maamuzi yote muhimu yaliyofuata wakati wa uvamizi.

Maombi ya haraka ya kutolivunja jeshi la Iraq au kupiga marufuku washiriki wote wa chama cha Baath kutoka kwa majukumu ya serikali kulipuuzwa au kupinduliwa.

Matokeo yake ni muungano mbaya kati ya wanajeshi wapya wa Iraq wasiokuwa na ajira maafisa wa ujasusi kupambana na wanajihadi washupavu.

Na hili likachangia kuundwa kwa kundi la Isis.

Hofu ya pamoja iliyofuata 9/11 ilimaanisha kuwa ujasusi wa Marekani na Uingereza uliishia kushirikiana na serikali kadhaa na rekodi mbaya za uvunjaji wa haki za binadamu.

Kwa mfano, baada ya utawala wa Kanali Gaddafi nchini Libya kupinduliwa mnamo mwaka 2011, waandishi wa habari walipata barua kutoka kwa afisa mwandamizi wa MI6 kwenda kwa mwenzake wa Libya iliyojadili juu ya kurudishwa kwa muasi wa Kiislam ili akamatwe na kutendewa vibaya.

Leo hii, vurugu zinazosababishwa na kundi la jihadi zimeibuka tena katika maeneo yasiyotawaliwa vizuri au yasiyosimamiwa barani Afrika, na kuwa kusababisha tatizo la nani haswa nchi za Magharibi anapaswa kushirikiana naye.

4. Kuheshimu haki za binadamu au upoteze maadili yako

Mara kwa mara watu katika Mashariki ya Kati wameniambia: "Huenda hatukupenda sera za kigeni za Marekani lakini kila wakati tuliheshimu sheria yake. Hadi Guantanamo Bay."

Kukusanya washukiwa "kwenye uwanja wa vita" - ikiwa ni pamoja na visa vichache vya raia wasio na hatia ambao walikuwa wameuzwa kujipatia faida - na kisha kuwafunga macho na kuziba masikio ili kuwasafirisha nusu ya ulimwengu hadi kituo cha mahabusu cha Marekani huko Cuba kulisababisha uharibifu mkubwa kwa Marekani na sifa ya Magharibi.

Kuzuiliwa bila kufunguliwa kesi ilikuwa kitu ambacho kilitokea katika nchi za kidemokrasia nyumbani.

Waarabu hawakutarajia hilo kutoka kwa Marekani.

Mbaya zaidi ilikuwa kuwafuata, kwa kile kilichosemekana kuwa "kuhojiwa kwa njia ya kisasa", kuwatesa na kuwanyanyasaji kwa kutumia maji na mbinu nyinginezo katika maeneo ya shirika la CIA ambapo watuhumiwa wa ugaidi walipotea tu wasijulikane walipo.

Urais wa Obama ulisimamisha hili lakini tayari uharibifu ulikuwa umefanyika.

Camp X-Ray

Chanzo cha picha, Getty Images

5. Kuwa na mkakati wako wa kujiondoa

Uingiliaji wa nchi za magharibi uliotangulia shambulizi la 9/11 ulikuwa wa haraka na rahisi kwa kulinganisha.

Sierre Leone, Kosovo, hata kampeni ya Dhoruba ya Jangwani mwaka 1991 - yote hayo yalikuwa na mwisho.

Lakini uvamizi ulioongozwa na Marekani nchini Afghanistan na kisha Iraq umesababisha kile kilichoitwa "vita vya milele"

Hakuna mtu aliyehusika miaka ya nyuma ya 2001 au 2003 alidhani kwamba bado watakuwepo miongo miwili baadaye.

Kwa ufupi, Magharibi haikuelewa ilikuwa inajiingiza wapi na hakukuwa na mpango halisi wa kutoka.

Hakuna shaka kwamba ikiwa Magharibi haingewahamisha Wataliban na Al-Qaida huko Afghanistan mnamo 2001 basi mashambulio mengine kutoka hapo yangetokea.

Ujumbe wa kupambana na ugaidi katika nchi hiyo sio kwamba haukufaulu lakini ule wa kujenga taifa haukukamilika.

Na leo, picha moja ya kudumu ambayo watu wengi wataondoka nayo ni ile ya Waafghan waliokata tamaa kukimbia pamoja na usafirishaji wa USAF C17, wakijaribu kutoroka nchi yao ambayo kwa sasa Magharibi imeachana nayo kabisa.