Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Milipuko Uganda: Watu 6 wafariki katika milipuko Kampala
Polisi nchini uganda wamethibitisha kwamba takriban watu sita wamefariki katika milipuko iliyotokea mjini Kampala mapema leo.
Shirika la habari la Reuters linanukuu kituo cha televisheni cha ndani juu ya idadi ya vifo.
NTV Uganda imesema Meya wa Kampala Salim Uhuru ndiye chanzo cha habari za vifo vya watu wawili vilivyoripotiwa hapo awali
Ripota wa NTV alisema aliona sehemu za mwili zikiwa zimetapakaa katika eneo moja la mlipuko huo:
Majengo ya ofisi yalitikisika wakati milipuko hiyo ilipoanza, baadhi ya mashahidi wameiambia BBC.
Gazeti la Daily Monitor limesambaza video ya magari yakiungua nje ya jengo la bima baada ya mlipuko huo:
Haijulikani ni watu wangapi wamejeruhiwa.
Mwezi uliopita, milipuko miwili tofauti nchini humo iliua watu wawili. Mmoja ulimuua mhudumu katika baa na mwingine, mshambuliaji wa kujitoa mhanga ambaye alikuwa ameingiza vilipuzi kwenye basi.
Mamlaka nchini humo zimeshutumu milipuko hiyo ya Oktoba dhidi ya kundi la waasi wa Kiislamu lenye makao yake makuu nchini Uganda, DR Congo, Allied Democratic Forces.
Takriban watu 50 wamekamatwa, na wengine kushtakiwa mahakamani, tangu matukio hayo ya hivi majuzi.