Zifahamu haki walizonazo wanaohukumiwa kifo duniani

Chanzo cha picha, F. Carter Smith
Mfungwa anayesubiri kunyongwa John Ramirez hataki kufa peke yake, anataka kufarijiwa na mkono wa mchungaji wakati anakufa.
Lakini ombi hilo lilikataliwa na Idara ya haki za wahalifu ya Texas na sasa muda wake wa mwisho wa maisha yale utakuwa katika mikono tofauti- Mahakama ya juu zaidi ya Marekani.
John Ramirez mweney umri wa miaka 37-ambaye ni mwanajeshi wa zamani wa kikosi cha majini, alihukumiwa kifo kwa wizi wa uporaji na kumuumiza mfanyakazi wa duka mwaka 2004, alisema "sala, wimbo na kuguswa'' ni sehemu muhimu katika imani yake ya Ukristo.
Alihisi kwamba ibada yake ya mwisho inayosomwa na Mchungaji wa kanisa la Kibabtisti ni haki yake, lakini maafisa wa Texas hawakujali madai yake. Walisema kuwa alikuwa anapoteza muda kwa lengo la kuchelewesha kuuawa kwake na kuendesha mchakato kwa "mchezo game kurejesha suala hilo ili kuchelewesha hukumu ".

Chanzo cha picha, Getty Images
Aliwashitaki, akidai ukiukaji wa sheria iliyorekebishwa ya uhuru wa dini, na majaji walikubali kusikiliza malalamiko yake, wakaahirisha tarehe aliyopangiwa kuuawa Ramirez ambayo ilikuwa ni tarehe 8 Septemba hadi baada ya kusikilizwa kwa kesi yake Jumanne.
Utekelezwaji wa hukumu ya kifo ya Bw Ramirez ni ya tatu kuahirishwa na Mahakama ya juu katika kipindi cha miaka mitatu kuhusiana na kama kweli, washauri wa kidini wanaruhusiwa kuwepo wakati wafungwa waliohukumiwa kifo wanapouliwa.
Mwaka 2019 kulikuwa na ukosoaji wa umma baada ya mfungwa Muislamu kuomba awe kuwa na imam wakati anauliwa akakataliwa lakini ombi sawa na hilo lilipotoka kwa Mbudha mwezi mmoja tu baadaye lilikubaliwa.
Lakini makabiliano kuhusu kuwa na kiongozi wa kidini -na haki nyingine- katika wakati wa kifo si kwa Marekani pekee.

Chanzo cha picha, Reuters
Kote duniani, nchi ambako hukumu ya kifo inaruhusiwa, mazungumzo magumu yamekuwa yakifanyika kuhusu ni nini kinachochukuliwa kama jambo linalokubalia-na mamlaka mara nyingi hawatekelezi mambo hayo kwa usahihi.
Nchini Japan, wafungwa wawili wanaosubiri kuuawa wiki iliyopita walichukua hatua ya kisheria baada ya kuambiwa kuwa watanyongwa simu moja.
Huku, wafungwa hufahamishwa saa kadhaa kabla ya kunyongwa, lakini sasa makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwafahamisha wafungwa kuhusu kifo chao kabala ya saa chache ni "unyama wa hali ya juu " na huathiri afya yao ya akili.
Wanaume hao waliwasilisha kesi yao katika mahakama ya wilaya katika jiji la Osaka Alhamisi iliyopita, katika kile kinachoaminiwa kuwa ni kesi ya kwanza ya aina hiyo, wakidai kuwa kufahamishwa haraka kuhusu mauaji yao haiwaandai kiakili na kutafakari kuhusu mwisho wa maisha yao.
Ni mauji ya siri yanayosababisha upinzani wa kimataifa dhidi ya Iran.
Katika kesi za mauji ya Iran ambapo hukumu hutolewa kwa qisas (kunyongwa), ambapo wanafamilia wa muathiriwa huhamasishwa kutekeleza wenyewe mauaji ya mtu wao.
Wanaweza pia kumpa nafuu mkosaji anapokuwa katika chumba cha kuuawa - n ani hili, lililopelekea hadithi ya mama muombolezaji ambaye, alipomtizama mwanaume aliyemuua mtoto wake wa kike akiwa amesimama naye na Kamba shingoni mwake, aliamua kumsamehena kuondoa kama shingoni mwake.
Mwanamke huyo na mama wa muuaji wa muuaji hatimaye walikumbatiana mbele ya umati wa watu waliokuwa wamekusanyika kushuhudia kunyongwa kwa mhalifu.
Kulingana na sheria ya Iran, jopo la mawakili wawakilishi mshukiwa linapaswa kuundwandani ya saa 48, lakini wanakampeni wanasema hii haifanyiki kila mara, hususan kwa kesi zinazohusiana na siasa na usalama.
Wakati huo huo, katika Singapore hofu zinatolewa juu ya mauaji ya mwanume mwenye mwenye kipimo cha akili- IQ cha 69, kiwango ambacho kinatambuliwa kama kiashirio cha ulemavu wa akili.
Nagaenthran Dharmalingam alikamatwa katika mwaka 2009 kwa kuleta gramu 42.7 (1.5 ounces) za mihadarati aina ya heroin nchini Singapore na alikuwa anasubiri kunyongwa Jumatano asubuhi, lakini hii imeibua hali ya kutonyamaza katika kisiwa hicho ambako uungaji mkono wa adhabu ya kifo bado ni wa kiwango cha juu.
PICHA:

Chanzo cha picha, EPA
Mawakili wa Dharmalingam na makundi ya kutetea haki za wanapambana kunusuru maisha yake, wakisema Singapore inakiukasheria ya kimataifa kwa kumuua mtu mwenye ulemavu wa akili. Wamewasilisha maombi yote ya kisheria na maombi kwa rais kwa ajili ya kumuombea msahamaha lakini hayakufanikiwa.
Lakini serikali ya Singapore imeendelea kushikilia msimamo wake, ikisema kuwa mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 33 "alielewa wazi matendo aliyo yafanya na hakupoteza maana ya hukumu ya usahihi na makosa ya kile alichokuwa akikifanya ".
Hasira pia imeibuka kuhusiana na mchato wa hukumu ya kifo nchini Misri.
Ingawa sheria yan chi ya Mtoto inasema kuwa watoto wote waliokiuka sheria yan chi hawata''hukumiwa kiofo, kufungwa maisha, au kutumikishwa kazi za lazima ", ripoti ya Reprieve (kikundi cha kimataifa cha kampeni kinachoongozwa na mawakili wa kimataifa) inasema kwamba walau watoto 17 wamehukumiwa kifo tangu mwaka 2011.
Waendesha mashitaka wanasema, Reprieve, wanatumia mianya iliyopo kuwaweka watoto mbele ya mahakama za watu wazima kwa ajili ya kesi, kwasababu sheria huwaruhusu wenye zaidi ya miaka 15 wakati mshitakiwa mwenza anapokuwa mtu mzima, kushitakiwa pamoja naye.
Wakati Mahakama ya juu zaidi ya Marekani wiki hii itakapotoa uamuzi kuhsuu kesi ya Ramirez, itaombwa kuzungumzia juu ya jinsi ya kumuua mtu katika njia ambayo haikiuki hali zake za kidini.
Lakini hali ya wasi wasi baina ya misingi ya utu na heshima ya binadamu na utekelezwaji wa hukumu ya kifo ni kinyume na hayo-na ndio inayotekelezwa kote duniani.
Bilas haka utageuka kuwa mjadala mkubwa kuhusu haki za wanaume na wanawake wanaokabiliwa na hukumu ya kifo.















