Vita vya Ethiopia mwaka mmoja baadaye: Jinsi ya kumaliza mahangaiko

th

Chanzo cha picha, EPA

    • Author, Catherine Byaruhanga & Yemane Nagish
    • Nafasi, Africa correspondent, BBC News

Vikosi vya waasi wa Tigray kwa sasa vina uwezo mkubwa katika vita vilivyozuka mwaka mmoja uliopita kaskazini mwa Ethiopia.

Waziri Mkuu Abiy Ahmed, ambaye alitofautiana na chama tawala cha Tigray kuhusu mageuzi yake ya kisiasa, ametangaza hali ya hatari nchini kote - ni hofu na mashaka ambayo sasa yanatawala.

Wakati waasi wakisonga mbele kuelekea mji mkuu, serikali imewataka wakazi wa Addis Ababa kuhamasishwa na kulinda vitongoji vyao.

Mzozo wa Kaskazini mwa Ethiopia

Matukio hatua kwa hatua kukua kwa vita vya Tigray

Mgogoro wa kaskazini mwa Ethiopia

Wapiganaji kutoka Tigray, wakiongozwa na Tigray People's Liberation Front (TPLF), waliteka miji ya Dessie na Kombolcha mwishoni mwa wiki.

Wako katika eneo la Amhara, ambalo ni jirani na Tigray, na liko umbali wa kilomita 400 (maili 250) kutoka mji mkuu.

Vita vya Dessie viliaminika kuwa vikali zaidi katika vita hivyo kwani jiji hilo linaonekana kama lango la kuingia Addis Ababa, kusini, na mpaka na Djibouti, upande wa mashariki

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Mwanamume mmoja ambaye alifanya kazi katika hospitali kuu ya Dessie kabla ya kuchukuliwa na waasia alisema kuwa jiji lilikuwa limebadilika sana katika miezi michache iliyopita huku mapigano yakiendelea katika eneo hilo.

Akiomba asitajwe jina, aliiambia BBC kwamba Dessie ulijulikana kama "mji mkuu wa upendo" kwa sababu ya mchanganyiko wake wa makabila mbalimbali na kitamaduni - kitovu kinachostawi kiuchumi.

[Bofya kwenda chini ]

Wanajeshi wa Ethiopia na vikosi washirika waimarisha operesheni za anga na ardhini dhidi ya vikosi vya Tigraya huko Amhara, katika eneo la kaskazini, ripoti zinasema.

Rais wa Marekani Joe Biden alitia saini amri ya utendaji ya kuanzisha awamu mpya ya vikwazo vinavyoipa serikali ya Marekani mamlaka ya kuwawajibisha wale walio katika “serikali ya Ethiopia, serikali ya Eritrea, TPLF, na serikali ya eneo la Amhara ambao wanawajibika, au kushiriki." katika, kurefusha mzozo, kuzuia ufikiaji wa misaada ya kibinadamu, au kuzuia usitishaji wa mapigano”.

Maelfu ya watu wameripotiwa kuuawa katika mapigano kaskazini mwa Ethiopia, huku mapigano kati ya wanajeshi na waasi wa Tigray yakiendelea.

Mzozo huo umekuwa ukiendelea kwa miezi 10, na kuwaingiza mamia kwa maelfu ya watu

katika hali ya njaa.

Waziri Mkuu Abiy Ahmed
Maelezo ya picha Waziri Mkuu Abiy Ahmed Haki miliki ya picha na Getty Images

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anatoa wito kwa raia kujiunga na jeshi katika

mapambano yake dhidi ya waasi katika eneo la Tigray. Aliwataka “Waethiopia wote wenye uwezo" "kuonyesha uzalendo wao” kwa kujiunga na vita.

Serikali kuu inakusanya makurutu zaidi na vikosi kutoka mikoa mingine - karibu mikoa yote sasa inahusika katika mzozo. Mkoa wa Amhara ‘unafanya kampeni ya kujinusuru’ huku TDF ikiripotiwa kusonga mbele katika miji zaidi ya Amhara.

Wanajeshi wa kike wa Ethiopia waliotekwa wamelala kwenye nyasi katika Kituo cha Marekebisho cha Mekelle huko Mekele, mji mkuu wa mkoa wa Tigray, Ethiopia.
Maelezo ya picha Wanajeshi wa kike wa Ethiopia waliotekwa wamelala kwenye nyasi katika Kituo cha Marekebisho cha Mekelle huko Mekele, mji mkuu wa mkoa wa Tigray, Ethiopia. Haki miliki ya picha na Getty Images

Mzozo huo unaenea haraka katika mikoa mingine miwili, ambayo ni Amhara na Afar. Ripoti kwamba mapigano yanafanyika kwa ajili ya udhibiti wa barabara kuu ya Djibouti-Addis Ababa- ambayo ni njia muhimu sana kuelekea kwa serikali ya Ethiopia.

Msemaji wa JWTZ Getachew Reda anasema vikosi vya Tigray viliteka udhibiti wa Alamata, mji mkuu kusini mwa Tigray.

Wafanyakazi watatu wa shirika la kimataifa la kutoa msaada la Madaktari wasio na Mipaka (Medecins Sans Frontieres, au MSF) waliuawa katika jimbo la Tigray.

Haki miliki ya picha na Getty images

Shambulizi la anga lapiga soko lenye shughuli nyingi katika kijiji cha Tigray cha

Togoga (Km 25 kutoka mji mkuu) na kuua takriban watu 60. Jeshi la serikali lilikanusha shutuma hizo likisema lilikuwa likilenga tu waasi.

Haki miliki ya picha na BBC

Viongozi wa zamani wa eneo la Tigray wanadai kuwa vikosi vya TDF vimedhibiti tena mji mkuu wa eneo hilo, Mekelle. Siku hiyo hiyo, serikali Kuu ilitangaza ‘kusitisha mapigano kwa sababu za kibinadamu’ na kusema kuwa iliondoa vikosi vyake.

Mwanamke anafua na kutundika vitambaa katika kambi ya wakimbizi wa ndani katika shule ya Kisanet Complete Primary na Junior mnamo Juni 18, 2021 huko Mekele, Ethiopia.
Maelezo ya picha Mwanamke anafua na kutundika vitambaa katika kambi ya wakimbizi wa ndani katika shule ya Kisanet Complete Primary na Junior mnamo Juni 18, 2021 huko Mekele, Ethiopia. Haki miliki ya picha na Getty images

Ripoti za mapigano makali huku Kikosi cha Tigray kilipoanzisha mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa serikali kuu. Jeshi la Ulinzi la Tigray (TDF) limesema limekamata miji kadhaa, silaha na kuharibu magari. Inasemekana yalifanyika uchaguzi wa kitaifa ulipokuwa ukiendelea tarehe 21 Juni, 2021.

Umoja wa Mataifa unasema watu 350,000 katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia

wanaathiriwa na baa la njaa huku zaidi wakiwa hatarini.

Katibu w masuala ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken
Maelezo ya picha Katibu w masuala ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony J. Blinken anatangaza vizuizi vya viza kwa maafisa wowote wa sasa au wa zamani wa Ethiopia na Eritrea, kwa wanamgambo wa kabila la Amhara na wanachama wa TPF wanaohusika na kudhoofisha utatuzi wa mgogoro wa Tigray.

Baraza la Seneti la Marekani limepitisha azimio kwa kauli moja la kutaka vikosi vya Eritrea kuondoka nchini Ethiopia.

Serikali ya Ethiopia yalitangaza TPLF kama kundi la “kigaidi”.

Eritrea yathibitisha kuwa wanajeshi wake walikuwa wakipigana huko Tigray nchini Ethiopia kupitia kwa balozi wake kwenye Umoja wa Mataifa kama ilivyoelekezwa kwa Baraza la Usalama. Kwa miezi pande zote mbili zilikataa kuwa wanajeshi wa Eritrea walihusika.

Vikosi vya jeshi la Ethiopia vinashika doria katika mitaa ya mji wa Mekelle wa eneo la Tigray, kaskazini mwa Ethiopia mnamo Machi 07, 2021 baada ya jiji hilo kutekwa katika operesheni dhidi ya Kikosi cha Ukombozi cha Tigray (JWTZ)
Maelezo ya picha Vikosi vya jeshi la Ethiopia vinashika doria katika mitaa ya mji wa Mekelle wa eneo la Tigray, kaskazini mwa Ethiopia mnamo Machi 07, 2021 baada ya jiji hilo kutekwa katika operesheni dhidi ya Kikosi cha Ukombozi cha Tigray (JWTZ) Haki miliki ya picha na Getty images

Waziri Mkuu Abiy Ahmed kwa mara ya kwanza anasema Eritrea ilikuwa imekubali kuondoa majeshi kutoka eneo la Tigray.

Waziri wa Mambo ya Nje Tony Blinken analaani “mauaji ya kikabila” yanaofanywa katika eneo la Tigray Magharibi nchini Ethiopia.

Haki miliki ya picha na Getty images

Uchunguzi wa Amnesty International unaonyesha kuwa wanajeshi wa Eritrea waliwaua mamia ya raia wa Axum, jambo ambalo linasema linaweza kuwa uhalifu dhidi ya binadamu-Eritrea inakanusha.

Wanajeshi wa Jeshi la Ethiopia wakiwa wamesimama huku watoto wakiwa nyuma yao kwenye kambi ya Wakimbizi ya Mai Aini, nchini Ethiopia, Januari 30, 2021.
Maelezo ya picha Wanajeshi wa Jeshi la Ethiopia wakiwa wamesimama huku watoto wakiwa nyuma yao kwenye kambi ya Wakimbizi ya Mai Aini, nchini Ethiopia, Januari 30, 2021. Haki miliki ya picha na Getty Images

Jeshi la Ethiopia latangaza kuuawa na kukamatwa kwa maafisa kadhaa wa JWTZ katika operesheni ya jeshi inayoendelea katika eneo la kaskazini la Tigray.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed awapa wanajeshi wa Tigray saa 72 kujisalimisha. Siku sita baadaye majeshi ya serikali kuu ya Ethiopia na washirika wake walichukua udhibiti wa Mekelle.

Mapigano yalianza kati ya serikali ya Ethiopia na vikosi vya jimbo la Tigray.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed aliamuru mashambulizi ya kijeshi kujibu shambulio dhidi ya kambi ya kijeshi inayohifadhi wanajeshi wa serikali huko.

Lakini katika kipindi cha miezi michache iliyopita, maelfu ya watu wamemiminika, wakikimbia harakati za waasi.

"Kuenda na kurudi kazini, watoto wadogo walikuwa wakivuta suruali yangu miguuni na kuniomba pesa za kununua mkate."

Yeye na wenzake zaidi ya 10 waliitelekeza hospitali walipowaona wanajeshi wa serikali wakiondoka mjini.

th

Sasa yuko Addis Ababa ambako Tewodrose Hailemariam, mwanachama mkuu wa Vuguvugu la Kitaifa la Amhara (NaMA), anahamasisha watu kutuma wapiganaji kukomesha hatua za TPLF na pia kusambaza misaada kwa wale waliokimbia makazi yao.

Anasema chama chake kinaamini misukumo ya kweli ya TPLF ni kurejea madarakani.

TPLF iliongoza nchi kwa miaka 27 hadi 2018 - ikitengwa na serikali ya Waziri Mkuu Abiy.

"Kuna mawili - ama TPLF itashindwa na serikali kuu ya Ethiopia iokolewe. Au hali mbaya zaidi ni kwamba TPLF inatawala na kudhibiti Addis Ababa na kisha kutakuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe katika taifa zima," Bw Tewodrose aliambia BBC.

Watigraya 'wanakamatwa'

Kwa watu wa Tigraya katika mji mkuu, kuanguka kwa Dessie kumezusha mvutano wa kikabila katika jiji hilo.

Wakili wa Tigraya anayeishi Addis Ababa alisema sio tena "mji nilikozaliwa na nilikokulia". Polisi wamekuwa wakiwakusanya watu wa Tigraya katika uvamizi wa nyumba, mikahawa na baa - na hata wakati wa ukaguzi wa utambulisho katika teksi na mabasi, alisema.

th

Katika visa vingine wiki hii, BBC iliambiwa kuhusu kundi ambalo lilichukuliwa walipokuwa wakipata chakula cha jioni kwenye mkahawa.

"Ikiwa wewe ni Mtigraya huna jinsi ya kujitetea. Unakamatwa. Kukamatwa ni kwa jina la kabila," mkazi mmoja alisema.

Msemaji wa polisi wa Addis Ababa alisema watu walikamatwa tu baada ya kupata ushahidi wa shughuli haramu. Alithibitisha kuwa wengi wa waliokamatwa walikuwa watu wa Tigraya lakini alisema kuwa watu wa makabila mengine pia walizuiliwa.

Waasi hao wanasema lengo lao ni kulazimisha serikali kukomesha vizuizi katika eneo la kaskazini la Tigray, ambapo misaada inahitajika na huduma za umeme na benki zimekatwa.

th

Tangu Mei, Umoja wa Mataifa umeonya kwamba watu 400,000 wako kwenye hatari ya njaa huko.

Baada ya TPLF kulisukuma jeshi nje ya mji mkuu wa Tigray, Mekelle, mwezi Juni, mashirika ya misaada yanasema yamekabiliwa na vizuizi kwenye barabara zinazoelekea katika eneo hilo, wakati vikwazo vya mafuta na fedha vimefanya kuwa vigumu kuleta misaada ya dharura kwa zaidi ya WATU milioni tano wanaohitaji misaada .

Baada ya awali kuweka mfumo wa mazungumzo na utawala wa Bw Abiy, vikosi vya Tigray, vilivyotiwa moyo na mafanikio yao ya kijeshi katika mikoa ya Amhara na Afar katika kipindi cha miezi michache iliyopita, sasa wanasema hawatazungumza.

Tsadkan Gebretensae, jenerali wa zamani wa jeshi na kamanda mkuu wa vikosi vya Tigray, amesema vita vinakaribia kumalizika na hatua inayofuata itakuwa mazungumzo ya kitaifa baada ya Abiy.

"Hatujawahi kuwa nia ya kutatua utata wa kisiasa wa nchi kwa masharti yetu tu. Tutaunda jukwaa la kuwaleta wadau wote pamoja na kujadili mustakabali wa nchi," aliambia Televisheni ya Tigrai.

Mshtuko wa wazazi

Mgogoro wa kibinadamu huko Tigray bado ni mbaya - kama inavyoonekana kwenye video kutoka Hospitali ya Rufaa ya Ayder ya Mekelle ambapo kilio cha Eden Gebretsadiq mwenye umri wa mwaka mmoja, kilichounganishwa na bomba la kulisha, kinasikika kupitia korido.

th

Chanzo cha picha, AYDER REFERRAL HOSPITAL MEDIC

"Mwanzoni sikujua kuwa ulisababishwa na uhaba wa chakula. Sasa wameniambia ana utapiamlo," mama yake mzazi, Hiwote Berhe, alisema huku akijaribu kumliwaza.

"Mume wangu alikuwa ameajiriwa - huku mimi nikitunza watoto nyumbani. Tulikuwa tukiwalea watoto wetu vizuri. Walikuwa wakipata chakula bora na walikuwa wamevalia vizuri kila wakati."

Katika kitanda kingine yuko Mebrhit Giday, viungo vyake vinaonekana vyembamba sana huku babake, Gidey Meresa, akimketisha kwa upole ili kula ndizi.

Anasema walisafiri zaidi ya kilomita 100 kufika hospitalini kutoka katika mji wao wa mashambani wa Kola Tembien, ambao ulishuhudia mapigano makali wakati wanajeshi wa serikali walipokuwa Tigray.

Wakazi wengi walilazimika kukimbilia milimani. Waliporudi baada ya jeshi na washirika wake kufukuzwa, walikuta nyumba zao zimeteketezwa na ng'ombe na punda wao wameibiwa.

"Hayo yote yalifanyika - na tulikubali. Lakini binti yangu aliugua sana - alikuwa na afya nzuri hapo awali," anasema. Madaktari wamemwambia mtoto huyo wa miaka 11 ana matatizo ya moyo, pengine yanasababishwa na ukosefu wa lishe.

Hizi ni sauti adimu kutoka Tigray - zilizotolewa kinyemela na maafisa wa matibabu kwa BBC.

Kuzimwa kwa huduma za mawasiliano ya simu na intaneti kunamaanisha kuwa mtandao hauna kasi na ni vigumu sana kuongea na watu huko. BBC, kama vyombo vingi vya habari, imezuiwa kufikia eneo hilo.

Kufeli kwa Vitisho

Katika ziara ya hivi majuzi nchini Ethiopia, Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu Peter Maurer hakuweza kwenda katika maeneo yenye migogoro.

"Kwa sasa hatuoni mwanga mwishoni mwa handaki," aliambia BBC.

"Kadiri tunavyopata suluhu ya kisiasa mapema inayotutoa kwenye mzozo, ndivyo inavyokuwa bora - kwa sababu tusijidanganye, hata kama mzozo huo utakoma kesho, bado tutakuwa na mamia ya maelfu ya watu waliokimbia makazi yao na mahitaji makubwa."

th

Chanzo cha picha, Reuters

Marekani, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika zote zimekuwa zikihimiza mazungumzo.

Vitisho vya kuwekewa vikwazo na hata tangazo la Marekani kwamba itaiondoa Ethiopia katika makubaliano muhimu ya kibiashara yameshindwa kubadili mkondo wa mzozo huo.

William Davison, mchambuzi mkuu katika Kundi la Kimataifa la Migogoro, anafikiri itakuwa kwa manufaa ya serikali kutoa makubaliano - kumaliza vikwazo vya upatikanaji wa misaada na kurejesha huduma muhimu kwa Tigray.

"Wadau nuhimu wa kimataifa wanapaswa pia kutoa wito kwa uongozi wa Tigray kuonyesha kujizuia kwa kiwango cha juu, kwani sio tu kwamba wanahitaji kumpa Waziri Mkuu Abiy Ahmed nafasi ya mwisho kubadili mwelekeo, lakini jaribio la haraka la kwenda hadi Addis pengine litasababisha kuongezeka kwa ghasia na uvunjifu wa amani. kwa kila mtu," aliiambia BBC.

Hata hivyo Bw Abiy, ambaye alishinda Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka wa 2019 kwa kumaliza vita na nchi jirani ya Eritrea, haonekani kuwa katika hali ya kutaka maelewano.

Wakati Ethiopia ikiadhimisha mwaka mmoja wa vita, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 45 aliendelea kuwahimiza wananchi wake kuelekea mstari wa mbele au kuunga mkono juhudi za vita.

"Tutamzika adui huyu kwa damu na mifupa yetu na kufanya utukufu wa Ethiopia kuwa juu tena."