Cecafa: Wachezaji 5 wa kikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 kutoka Eritrea watoweka Uganda

Bendera ya ya Eritrea

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Eritrea ilipoteza mechi zake mbili za kwanza katika michuano ya Cecafa kwa Tanzania na Ethiopia

Wachezaji hao walitoweka kutoka katika hoteli yao mjini Jinja siku ya Jumanne alfajiri.

Walikuwa miongoni mwa kikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 wa kikosi cha michuano ya CECAFA , ilioanza siku ya Jumamosi na kuendelea hadi Novemba 9 karibu na eneo la Njeru.

Hii ni mara ya pili katika kipindi cha miaka miwili kwa raia hao wa Eritrea kutoweka kutoka katika michezo ya kombe la CECAFA nchini Uganda, baada ya wachezaji watano wa kiume kutoroka hoteli yao mwaka 2019.

Taarifa kutoka Cecafa ilisema kwamba suala hilo liliripotiwa kwa maafisa wa polisi na uchunguzi unaendelea.

Mkurugenzi mkuu wa CECAFA ameambia BBC kwamba hatua zimechukuliwa kuwazuia wachezaji kutoroka licha ya tukio hilo.

Auka Gecheo aliongezea kwamba Cecafa itashirikiana kwa karibu na Shirikisho la soka Uganda FA{ Fufa} ili kuwasaka wachezaji waliotoweka.

'Tayari tumeripoti kwa mamlaka na kutoa habari zote na pamoja na Fufa tutashirikiana na mamlaka', alisema Gecheo.

''Kulikuwa na mikakati mizuri ya usalama iliowekwa na Fufa ilituhakikishia kwamba timu zote zilikuwa katika hoteli nzuri. Sio tukio gen,i limefanyika awali . Mamlaka inajua kuhusu kilichotokeaa awali. Tutaendelea kufanya kazi kwa karibu na mamlaka huku tukihakikisha kwamba tunaafikia malengo yetu ya kuandaa mchuano ambayo itajumuisha wote katika eneo hili''.

Ndege za kimataifa

Tukio hili linajiri wakati ambapo kumekuwa na orodha ndefu ya wachezaji wa soka kutoka Eritrea wakitoroka wakati ambapo wako katika mechi za kimataifa ugenini.

Wachezaji saba walitoweka nchini Uganda mwaka 2019 wakati wa michuano ya CECAFA.

Wachezaji 10 wa Eritrea walikataa kurudi nyumbani kutoka mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia nchini Botswana 2015 , huku Uganda ikiwapatia uhifadhi wachezaji 15 na daktari wa timu 2013.

Mwaka 2009 , timu yote - isipokuwa mkufunzi na afisa - walikataa kurudi nyumbani baada ya michuano ya Cecafa nchini Kenya

Kundi la haki za kibinadamu la Amnesty International linasema maelfu ya raia wa Eritrea wanaendelea kutoroka taifa hilo la Afrika mashariki huku mamlaka ikikiuka uhuru wa kujieleza , ule wa kidini na ule wa kutembea.

Serikali ya Eritrea imekana madai hayo hapo nyuma na kusema kwamba idadi ya wale wanaoripotiwa kutoroka ni bandia. Wachezaji watano wa Eritrea kutoka kikosi cha wachezaji wanawake wasiozidi umri wa miaka 20 wametoweka wakati wa michuano soka nchini Uganda.