Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Waliopata dozi mbili za chanjo huweza kuwaambukiza wengine
Watu waliopata awamu mbili za chanjo hupata maambukizi ya Covid na kuwaambukiza wale wanaoishi nao, watahadharisha wataalam ambao wametafiti hali ya maambukizi kwenye kaya za Uingereza.
Watu ambao wamepata dozi mbili za chanjo wanaweza kuambukiza sawa na wale ambao hawajachanjwa.
Hata kama hawana dalili au dalili chache, nafasi ya wao kusambaza virusi kwa wenzao walio nyumbani ambao hawajachanjwa ni karibu wawili kati ya watano, au 38%.
Hii inashuka hadi mmoja kati ya wanne, au 25%, ikiwa wenzao wa nyumbani pia wamechanjwa kikamilifu.
Watu ambao hawajachanjwa hawawezi kuwategemea wale walio karibu nao kuchanjwa ili kuondoa hatari yao ya kuambukizwa, wanaonya.
Chanjo hufanya kazi nzuri ya kuzuia ugonjwa na vifo vya Covid, lakini sio nzuri katika kukomesha maambukizi, haswa tangu kuibuka kwa kirusi aina ya Delta ambacho kikubwa nchini Uingereza.
Na baada ya muda, ulinzi unaotolewa na chanjo hupungua na unahitaji kuimarishwa kwa dozi zaidi.
• Watu waliopata chanjo dozi mbili wako kwenye hatari kiasi, lakini wako hatarini kuambukizwa kirusi cha Delta ikilinganishwa na watu ambao hawajachanjwa.
• Pia wanaonekana kuwa na uwezo wa kuambukiza vile vile
• Watu waliopewa chanjo huyakabili maambukizi kwa haraka zaidi, lakini kilele chao cha virusi - wakati watu wanaambukiza zaidi - ni sawa na kile kinachoonekana kwa watu ambao hawajachanjwa.
• Hii inaweza kueleza kwa nini wanaweza kusambaza virusi kwa urahisi katika mazingira ya kaya.
Prof Ajit Lalvani, wa Chuo cha Imperial London, Uingereza, ambaye aliongoza utafiti huo, alisema: "Maambukizi yanayoendelea tunayoona kati ya watu waliochanjwa yanafanya kuwepo kwa umuhimu kwa watu ambao hawajachanjwa kupata chanjo ili kujikinga na maambukizi na Covid-19 kali. hasa kwa vile watu wengi zaidi watakuwa wakitumia muda mwingi wakiwa ndani hasa wakati wa miezi ya baridi kali.
"Tuligundua kuwa uwezekano wa kuambukizwa uliongezeka ndani ya miezi michache baada ya dozi ya pili ya chanjo - kwa hivyo wale wanaostahili kupata chanjo za nyongeza wanapaswa kuzipata mara moja."
Mwandishi mwenza Dk Anika Singanayagam, pia kutoka Imperial, alisema: "Matokeo yetu yanatoa ufahamu muhimu juu ya athari ya chanjo kwa aina mpya za virusi, na haswa, kwa nini kirusi cha Delta kinaendelea kusababisha idadi kubwa ya maambukizi ya Covid ulimwenguni kote, hata katika nchi zilizo na viwango vya juu vya chanjo.
"Kuendelea na kuchua hatua za afya ya umma na kijamii kupunguza maambukizi - kama vile kuvaa barakoa, kuzingatia umbali wa mtu na mtu na upimaji - kubaki kuwa muhimu, hata kwa watu waliochanjwa."