Mabadiliko yatabia nchi: Mambo 4 unayoweza kufanya kupunguza gesi ya kaboni

Kukabiliana na mabadiliko yatabia nchi kunawahitaji viongozi wa dunia kuchukua hatua kwa viwango vya kimataifa.

Lakini sisi wenyeye pia huchangia gesi zinazoharibu. Hivi ni baadhi ya vitu unaweza kufanya kupunguza athari zako wewe binafsi.

1. Kuziba nyumba yako

Kuanzia kutumia pampu za umeme hadi kuzima vifaa vya joto, kuna mabadiliko kadhaa nyumbani yanayoweza kuisaidia dunia

"Kwa kuacha kutumia mifumo ya joto inayotumia gesi na mafuta kwenda ile inayotumia umeme inaweza kuwa na mabadiliko makubwa," kulingana na Dr Neil Jenning msomi kutoka Imperial College London.

"

"Kila siku, kuzima taa na vifaa vya nyumbani wakati havitumiki inaweza kutusaidia kuokoa pesa huku pia tukipunguza athari zetu kwa mabadiliko ya tabia nchi."

Serikali ya Uingereza itatoa misaada ya pauni 5,000 kufadhili ununuzi wa pampu zinazotumia umeme kutoka Aprili 2022.

Tunaweza kubadilisha nyumba zetu kwa kuweka vizuizi vya joto kwenye ukuta, kwenye dari na madirisha.

Pia kuna njia moja inayotajwa kuwa nafuu na bora zaidi inayojulikana kama Draught-Proofing inayohusu kuziba mianya isiyohitajika inayoruhusu hewa baridi kuingia na hewa yenye joto kutoka kwa mfano sehemu zilizo kando ya madirisha na milango.

Inakadiriwa kuwa kwa kufanya hivyo kunaweza kuokoa paundi 25 kwa mwaka katika matumizi ya nyumbani.

2. Kuzuia utupaji wa chakula na kupunguza nyama nyekundu

Mifugo huchangia asilmia 14 ya gesi chafu, huku ng'ombe wakiwa ndio wachangiaji wakubwa.

Njia rahisi na bora zaidi ya kupungzua athari yako ni kupunguza nyama unayokula, hasa nyama nyekundu kwa mfano ya ng'ombe.

Dr Jonathan Foley ambaye anachunguza suluhu kwa mabadiliko ya hali ya hewa anasema unaweza kuokoa pesa na kupunguza utupaji wa chakula kwa kupika chakula kidogo na kuhifadhi mabaki kwa matumizi ya baadaye nyumbani.

Dunia hutupa kati ya asilimia 25 na 30 ya chakula chake.

3. Punguza utumiaji wa magari na pia ndege

Sekta ya usafiri inachangia karibu robo ya gesi ya kaboni duniani.

Kuacha kuendesha gari kunaweza kuwa kitu bora tunaweza kufanya kupunguza gesi itokanayo na usafiri kwa mujibu wa Dr Jennings.

Hata hivyo kuacha gari haitawezekana kwa kila mtu, hasa ikiwa unaishi eneo lisilo na mifumo mizuri ya usafiri au kufanya kazi awamu ya usiku maeneo yasiyo na mifumo mizuri ya usafiri.

Hatua ndogo bado zina matokeo kama vile kutembea au kwa kuendesha baskeli kwenda dukani au kutumia gari moja na marafiki au na majirani.

Magaria yanayotumia umeme yamekuwa mengi lakini bado ni ghali. Na yatakuwa safi iwapo umeme unatumiwa kwa magari hayo unatokana kwa nishati safi kama vile yenye itokanayo na upepo na jua.

Kwa bahati mbaya usafiri wa ndege ndio mchangiaji mkubwa zaidi wa hewa ya kaboni na vitu tunaweza kufanya sisi binafsi.

Usafiri wa ndani ya nchi huwa na kiwango cha juu zaidi cha gesi kwa kila mtu kwa kilomita moja.

4. Fikiri kabla ununue

Unagharamu lita 3,781 za maji kutengeneza suruali moja aina na jeans kuanzia uzalishaji wa pamba, kutengeneza, usafirishaji na kuosha.

Unaweza kupunguza athari zako kwa kushona nguo badala ya kununua nyingine, kuchangia badala ya kutupa na kuchagua nguo za ubora wa juu ambazo zitadumu.

Kampuni zinazo azima nguo zinaendelea kuongezeka ambazo husaidia kupunguza utupaji. Pia unaweza kujaribu nguo za mitumba au zilizotumika.

Kwa kuchagua vifaa bora vya kutumika nyumbani pia utapunguza athari zako kwa gesi chafu. Dr Jennings anasema kwa kuhakikisha umenunua vifaa visivyotumia kiwango kikubwa cha umeme kama vile mashine za kuoshea wakati tunahitaji zingine.