Mpigapicha wa wanyamapori wa mwaka: Picha ya mlipuko wa ngono wa samaki yashinda tuzo

Chanzo cha picha, LAURENT BALLESTA / WPY
Ni kama mlipuko chini ya maji. Lakini ni Kundi la samaki wa kiume likikimbia kumwaga mbegu za kiume kwenye mayai ambayo yameachiliwa tu mara moja na samaki wa kike.
Picha hii iliyopigwa na mpigapicha Fakarava Atoll katika bahari ya Pacific, ilimpatia Laurent Ballesta hadhi ya kuwa mpigapicha wa mwaka wa wanyamapori (WPY)
Rais wa jopo la majaji, Roz Kidman Cox, aliitaja picha hiyo kama picha iliyopigwa kwa ufundi wa hali ya juu .
"Kwa upande mmoja ni mazingira, ilichukuliwa wakati wa mbaramwezi, lakini pia wakati sahihi, kujua ni wakati gani wa kupiga picha.
"Picha hii ilinivutia kwasababu ya umbo la wimbi la yai :Linaonekana kama alama ya kuuliza. Ni swali kuhusu hali ya baadaye ya mayai haya kwasababu ni mmoja kati ya milioni atanusurika na kuweza kuwa samaki mzima, labda ni ishara zaidi ya hali ya baadaye ya asili, Ni swali muhimu kuhusu hali ya baadaye ya asili. "
Katika sherehe hizo mshindi wa tuzo hili kubwa, ambaye ni Mfaransa alishinda tuzo ya picha za chini ya maji .

Chanzo cha picha, VIDYUN R HEBBAR / WPY
Mvulana mwenye umri wa miaka 10, Vidyun R Hebbar kutoka India alichaguliwa kama mpigapicha mwenye umri mdogo zaidi wa mwaka kwa picha hii ya ya buibui anayezunguka kwenye mtandao wake.
Picha hiyo inaitwa Dome Home.
Shindano hilo lililoanza mwaka 1964, huandaliwa na Makumbusho asili ya kihistoria yaliyopo mjini London.
Mashindano hayo huwavutia maelfu ya wapiga picha wanaotuma maombi ya kushiriki kila mwaka. Wafuatao ni washindi walioshinda katika vitengo binafsi.
Ndovu katikachumba cha Adam Oswell, Australia

Chanzo cha picha, ADAM OSWELL / WPY
Adam Oswell alipokea tuzo la uandishi wa habari wa picha kwa picha hii ya wageni wanaotembelea hifadhi ya wanyama katika Thailand wakimtazama ndofu mchanga ndani ya maji . Utalii wa ndovu umeongezeka kote nchini Urusi.
Mguso wa uponyaji, kutoka kwa kituo cha ukarabati cha kijamii , iliyochukuliwa na Brent Stirton, Afrika Kusini

Chanzo cha picha, BRENT STIRTON / WPY
Brent Stirton alishinda katika kitengo cha uandishi wa habari wa picha. Ni msururu wa picha zinazotiririka katika kituo cha ukarati na utunzaji wa sokwe waliookolewa kutokana na walaji wa wanyama pori Afrika.
Ana kwa ana na Stefano Unterthiner, Italia

Chanzo cha picha, STEFANO UNTERTHINER / WPY
Tuzo ya WPY kila mara imekuwa limekuwa na picha bora za barafu na kitengo cha picha hizi mshindi alikuwa ni Stefano Unterthiner ambaye alishuhudia nguruwe kutoka Svalbard, na Norway.
Tafakari ya Majed Ali, Kuwait

Chanzo cha picha, MAJED ALI / WPY
Majed Ali alitembea saa nne kukutana na Kibande, sokwe wa mlimani mwenye karibu umri wa miaka 40 -katika msitu mkubwa wa Bwindi kusini magharibi mwa Uganda. Kitengo cha picha za wanyama Picha hii inayoonesha Kibande alijipoza katika jua ilishinda.
Barabara ya kuelekea uharibifu ya Javier Lafuente, Uhispania

Chanzo cha picha, JAVIER LAFUENTE / WPY
Picha ya Javier Lafuente inanyesha barabara zinazopinda katika ardhi tambarare la eneo lenye unyevu ambalo ni makao ya zaidi ya mamia ya spishi za ndege .Barabara hiyo ilijengwa katika miaka ya 1980 ili kutoa njia ya kufikia ufukweli imegawanya maeneo mawili ya ardhi yenye unyevunyevu, Picha hii ilishinda kitengo cha picha za ardhi ya unyevu : Kitengo cha picha pana Broader.
Weaving Gil Wizen's Cradle, Israel / Canada

Chanzo cha picha, GIL WIZEN / WPY
Gil Wizen ni mtaalamu wa picha na daktari wa magonjwa buibui aina ya dolomede anavuta Hariri ilikutengeneza mfuko wa mayai yake . Aina hii ya buibui ni maarifu katika maeneo yenye ardhi zenye unyevunyevu mashariki mwa Marekani . Picha hii ilishinda katika Tabia : kitengo cha viumbe wasiokuwa na uti wa mgongo
Maonyesho ya picha ya mwaka ya wanamapori yalifunguliwa Ijumaa, Oktoba 15 katika Makumbusho asilia ya kihistoria mjini London. Halafu yataendelea katika maeneo mengine ya Uongereza na baadaye yatafanyika kimataifa katika mataifa Australia, Ubelgiji, Canada, Denmark, Germany, Marekani nan chi nyingine.












