Khadija: Mfahamu mwanamke huyu aliyemsaidia pakubwa mtume Muhammad kueneza Uislamu

Mwanamke katika ibada

Kuna msemo unaoelezea kwamba nyuma ya kila mwanamume aliyefanikiwa kuna mwanamke pia aliyefanikiwa.

Ni msemo uliomkumba mtume Muhammad. Mtume huyo aliyesifika kwa kueneza Uislamu alifunga ndoa na wanawake zaidi ya mmoja , lakini katika kipindi muhimu cha miaka 25 ya maisha yake , alimuamini sana mwanamke mmoja.

Jina la mwanamke huyo ni Khadija.

Utambulisho wa Khadija kuwa mwanamke wa kwanza aliyekubali kuwa Muislamu umekumbatiwa na wengi, na hadithi ya Khadija inawashangaza wanawake wengi wasio Waislamu.

Alikuwa mwamake aliyefanikiwa kwa kiasi kikubwa kibiashara, kiumri alikuwa mkubwa zaidi ya Mtume huku akiwa na mchango mkubwa katika Maisha ya mtume Muhammad

Je Khadija ni nani?

Alizaliwa mjini Mecca katikati ya karne ya sita katika familia tajiri ambapo alihusika sana katika kufanikisha biashara za babake.

Hata baada ya kifo cha babake , Khadija aliendeleza biashara na kutoa mchango mkubwa katika ufanisi wake.

Alitumia mali yake kwa maendeleo ya umma. Alitumia utajiri wake katika kuwasaidia wajane, wasiojiweza na wagonjwa mjini Mecca.

Uhusiano kati ya Khadija na mtume Muhammad ulionekana muhimu katika kuenea kwa Uislamu.

Mtume Muhammed hakumsaidi Khadija kibiashara tu , bali pia alimsaidia kuipanua na kuendeleza zaidi biashara yake mbali na mapenzi waliokuwa nayo kati yao .

Mbali na kumsukuma kuendelea na juhudi zake za kusambaza Uislamu bi Khadija pia alimsaidia mtume kifedha.

Profesa wa chuo kikuu cha Havard nchini Marekani Laila Ahmed aliambia BBC kwamba Khadija alichangia pakubwa katika harakati za Muhammad kuwa mtume.

Wakati Uislamu ulipokuwa mashakani katika siku zake za kwanza , ukarimu wa Khadija ulisaidia sana katika kuivutia imani na mioyo ya wengi.

Mwanamke huyo alikuwa na uwezo mkubwa na mwenye mawazo huru na njia aliyochagua ilibadilisha historia ya Uislamu.

Waumini wa dini ya Kiislamu
Maelezo ya picha, Waumini wa dini ya Kiislamu

Laila anasema, "Khadija alikuwa na mali nyingi . Alimpenda mtume Muhammad kwasababu alikuwa mtu mwaminifu .

Wakati Khadija alipokuwa na umri wa miaka 40 mtume Muhammad alikuwa na umri wa miaka 25. Kila wakati mtume Muhammad alihisi kukata tamaa , Khadija alimpatia nguvu za kuendelea.

Wakati ambapo watu walikuwa hawaamini 'uwepo wa Mungu mmoja' katika mashariki ya kati, Mtume Muhammad alisimama kidete na kusisitiza kwamba Mungu{ Allah} ni mmoja.

Mwaka 619 AD , Khadija alipatwa na maradhi na kufariki. Hii leo licha ya kwamba kuna mjadala kuhusu hadhi ya mwanamke katika Uislamu , ni Mwanamke aliyehusika pakubwa katika kuenea kwa dini ya Kiislamu