Ayesha Khan: Nyota aliyekimbia nchi yake kwa sababu ya muziki

Chanzo cha picha, Courtesy Ayesha Khan
Ayesha Khan akiwa amekaa kwenye zulia la rangi ya kahawia akiimba kwa sauti nzuri. Ghafla anaangukwa na kilio lakini sipati maneno ambayo yanaweza kumfariji.
Kwa wiki kadhaa, Ayesha amekuwa akiishi katika chumba kimoja katika gorofa jipya, katika taifa la kigeni.
Baada ya Taliban kuchukua madaraka, alilazimishwa kuondoka nyumbani kwake Kabul, hivyo ilimbidi akimbie taifa lake, lakini katika yote ameondoka huku hajatimiza ndoto zake.
"Sijaondoka nchini kwangu kwasababu mimi ni msichana wa kiislamu ambaye sivai hijab au kufunika kichwa changu chote," aliiambia BBC.
"Ilinibidi kuondoka katika nchi yangu kwa kuwa mimi ni mwanamke na muimbaji."
Taliban wanapiga marufuku maonesho ya muziki na aina yoyote ya muziki ambayo si ya kidini ya kiislamu.
Lakini kwa kesi ya Ayesha, hatari iliyokuepo kwake ilichanganywa na uelewa wa kundi hilo na nafasi ya mwanamke katika jamii.
"Taliban wametulazimisha kuacha kazi zetu ," anasema Ayesha. "Ni ngumu sana kuwa mwanamke wa Afghanistan siku hizi lakini kuwa mwimbaji ni jambo ambalo halivumiliki kwa Wataliban."
'Nyota wa Afghan'
Ayesha alipata umaarufu baada ya kuanza kuonekana katika kipindi kimoja maarufu cha TV mwaka 2018.
Alisomea muziki Kabul kwa kipindi cha miaka miwili na anakipaji cha sanaa ya maonesho.

Ayesha anasema asingeweza kuacha muziki. "Nilifanya kazi sana, usiku na mchana kwasababu ninapenda muziki. Siwezi kuacha," alisema.
"Kwangu mimi , muziki ni namna ya kujieleza wewe ni nani pamoja na utamaduni wako. Kwa kuwa ni mwanamke inaniwia vigumu sana kuongea kuhusu jinsi ninavyojisikia, lakini tunaweza kufanya hivyo kupitia muziki kwasababu kila mtu anapenda muziki."
Maamuzi yake ya kuondoka Afghanistan hayakuwa rahisi hata kidogo. Ayesha aliondoka kwake bila kitu bali akiwa na mkoba ambao ulikuwa na nguo , na safari haikuwa rahisi haswa katika kuvuka mipaka.
Ndoto yake ya kuwa mwanamuziki ilikuwa tayari inakinzana na mahusiano yake na familia yake.
"Nilikuwa mwanafunzi wa sheria . Baba yangu alinipeleka shule nzuri sana na chuo , lakini alitaka kunifanya niwe wakili kazi ambayo sikuvutiwa nayo ," alisema.
Ayesha hapendi kuongelea kuhusu familia yake kwa undani lakini anasema alipata wakati mgumu na changamoto nyingikuchagua muziki kuwa kazi ".
Shuleni, alisimamia katika kipaji chake kwa kuimba mashairi yanayomsifu Mtume Muhammad.
Walimu wake walipenda kipaji chake lakini kilikuwa akithaminiwi nyumbani .
"Familia yangu wana misimamo mikali ya kidini, hawapendi muziki."

Chanzo cha picha, Courtesy Ayesha Khan
Miaka michache iliyopita, wakati alipochaguliwa kushiriki katika kipindi cha Afghan Star, Ayesha aliondoka nyumbani na kwenda kuishi hosteli.
Alifahamu kuwa familia yake haitaridhia kwa yeye kushiriki katika kipindi hicho.
"Mashindano ya Afghan Star yalikuwa maarufu sana nchini kwangu " alisema. "Nilijua kuwa familia yangu isingeweza kuniruhusu kushiriki kama ningeomba ruhusa."
Hali ikawa mbaya zaidi wakati Taliban walipochukua madaraka, Ayesha anasema anapata wakati mgumu kulala. Anahofia marafiki zake ambao wanapata changamoto nyingi sana na vitisho kutoka katika kundi hilo.
"Hawawezi kwenda kokote hata kuzunguka mtaani kwao tu. Wana simanzi na mioyo yao imekatishwa tamaa," alisema.
"Si maamuzi rahisi kufanya mahojiano katika hali ya sasa lakini nataka kuongea kwa ajili ya rafiki zangu wote ambao bado wanaishi Afghanistan chini ya vitisho," aliongeza kusema.
Nataka kutuma ujumbe kwa Taliban - kuwa Afghanistan "ni nchi ya Waafghanstani wote".
"Afghanistan si taifa la Taliban peke yake. Taliban wanapaswa kuwaruhusu wanawake kuishi kwa amani kwa kuheshimiwa na kutominywa kwa haki zao muhimu."

Ayesha ana ujumbe kwa dunia pia.
"Watu wa umri wangu wanajihisi kuwa hawalindwi hivyo nina ombi kwa dunia kutusaidia ili tuweze kupata uhuru wetu"
Wakati tunamaliza mahojiano, Ayesha analia tena. Na kuanza kuimba kwa lugha ya Urdu.
Wakati nasikiliza nadhani Ayesha ana nia thabiti ya kuongea kwa ajili ya kizazi chenye vipaji nchini Afghans ambao wamekataa kukubali mfumo huu wa giza.














