Afghanistan: Nyota wa muziki wa pop alitorokaje Kabul
Aryana Sayeed anafahamika kama Madona wa Afghanistan. Yeye pia ni mwanaharakati mkubwa wa kutetea haki za wanawake nchi humo na amekuwa akipigania haki ya Waafghanistana kuvaa wanavyotaka. Hapa anasimulia kutoroka kwake kwa kutisha kutoka uwanja wa ndege wa Kabul.