Viumbe hawa sita wanaishi vipi kwa mamia ya miaka kuliko binadamu?

F

Chanzo cha picha, AFP

Maisha ya wanadamu duniani yanaweza kuzingatiwa kuwa mafupi ikiwa tunayalinganisha na urefu wa maisha ambao wanyama wengine wanao.

Wakati wanadamu wana wastani wa kuishi kwa miaka 72 kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), kuna viumbe kadhaa kwenye sayari ambao hawafi na wengine wanaweza kuishi hadi maelfu ya miaka.

Wanasayansi wanajaribu kujua kwanini wanyama wengine wanaishi kwa muda mrefu, wakijaribu kufichua mafumbo yao na wanatumai kuweza kutumia maarifa haya kuzidisha maisha ya mwanadamu.

Hawa hapa baadhi ya wanyama wanaoishi kwa muda mrefu zaidi:

1.Turritopsis dohrnii

TL

Chanzo cha picha, Getty Images

Samaki kwa jina Jellyfish Turritopsis dohrnii hana ubongo na moyo na anadhaniwa kuwa kiumbe pekee asiyeweza kufa duniani; ainaishi katika maji ya kitropiki.

Kama wanasayansi walivyothibitisha, jellyfish hawafi kwa uzee kwani huishi hadi umri fulani kisha wanaanza kuwa wadogo na kurudi kwenye hatua yao ya asili.

Na kutoka hatua hiyo ya kuwa mchanga , anaanza tena kukua. Kwa bahati nzuri, hakuna kikomo kwa idadi ya nyakati ambazo wanaweza kufanya hivyo! Kwa hivyo, kiumbe huki kinaweza kuishi idadi isiyo na kipimo .

2.Papa wa Greenland(Greenland shark)

TL

Chanzo cha picha, AFP

Papa wa Greenland anaishi katika kina cha chini zaidi cha Bahari ya Aktiki na anatoka familia ya inayojulikana kisayansi kama somnios.

Papa huyu hukua hadi sentimita 0.5 hadi 1 kwa mwaka na anaweza kukua hadi urefu wa futi 24 na anaweza kuishi majini na ni papa pekee anayeweza kuvumilia joto la Aktiki mwaka mzima na joto la digrii 7 hadi -2.

Hili ni la kushangaza sana kwani papa wengi ni huwa hawastahimili katika mazingira ya joto linalozidi 40c. Mnyama huyu huishi hadi miaka 100-200, ambayo ndiyo kiashiria kikubwa kwa papa.

Kiumbe huyu hachagui chakula, hula hata viumbe hai. Umri wa juu wa papa wa Greenland unaweza kuthibitishwa ni miaka 392.

3.Nyangumi wa Bowhead (Bowhead Whale)

Sifa ya kuwa mamalia anayeishi kwa muda mrefu zaidi kwenye sayari zinaenda kwa nyangumi kwa jina hili Bowhead, anayejulikana pia kama nyangumi wa Arctic. Wengi wao wanaaminika kuwa na zaidi ya miaka 200, wakati wa zamani zaidi anayejulikana ana umri wa miaka 211.

Nyangumi hawa wana jeni katika mwili wao, ambayo huitwa ERCC1 ambayo inaendelea kutengeneza DNA iliyoharibika mwilini.

Kwa hivyo, samaki hawa hawana magonjwa mabaya kama saratani, magonjwa ya moyo na mishipa .

4. Samaki wa Koi

F

Chanzo cha picha, AFP

Samaki aina ya Koi ni samaki wadogo wa kufugwa kwa ajili ya mapambo. Samaki wa zamani zaidi wa spishi ya koi alikufa akiwa na miaka 226 huko Japani mnamo 1977, kwa wastani, samaki hawa wanaishi miaka 40-50.

Nchi ya jamii hii ndogo ya samaki hawa kwa kawaida ni China, lakini samaki huyu alipata umaarufu zaidi nchini Japani, ambapo amekua sana.

Wajapani walimpa jina Hanako kwa mtu mmoja maarufu sana . Mara ya kwanza, samaki wa koi waliliwa, baadaye walianza kuhifadhiwa nyumbani kama samaki wa mapambo.

5.Kobe wakubwa wa Galapagos

G

Chanzo cha picha, AFP

Kobe wakubwa wa Galapagos wanajulikana kwa visiwa maarufu vya Galapagos na wamekuwa wakizingatiwa kama moja ya viumbe hai zaidi Duniani na kwa hivyo, kwa kuwa wao ndio viumbe wenye uti wa mgongo walio na maisha marefu zaidi, wastani wa miaka 200.

Mnamo 2006, kobe wa kiume aliyeitwa Adwaita alikufa akiwa na umri wa miaka 255 huko Alipore Zoological Gardens ya Kolkata. Aliishi kwa lishe ya matawi ya ngano, karoti, saladi, gramu iliyolowekwa (chickpea), mkate, nyasi na chumvi.

inasemekana kwamba kobe huyu wa kiume mwenye uzito wa hadi kilo 250 ya spishi za Algebra alipewa zawadi kwa Lord Clive, mwanzilishi wa Dola ya Uingereza nchini India. Uhai wa wastani wa kobe hawa ni zaidi ya miaka 150-250.

6. Samaki wa Rougheye

YT

Chanzo cha picha, YOUTUBE

Rougheye rockfish ni moja wapo ya samaki wakubwa wanaoishi. Wanaishi kwa takriban miaka 205. Samaki hawa hupatikana katika Bahari la Pasifiki kutoka California hadi Japani.

wanaweza kukua hadi inchi 38 kwa urefu. Pamoja na hayo, hatari ya kutoweka pia imeongezeka kwa spishi hii, na kusababisha kampeni nyingi ili kuwahamasiaha watu kuhusu umuhimu wa kuitunza spishi hii