"The accident": kitu cha ajabu kilichogundulika katika galaksi yetu kinacho washangaza wanaanga na wataalamu wa nyota

Sio nyota au sayari kabisa, lakini kuna kitu katikati, na kinaweza kuwa zaidi ya kile ambacho awali kilidhaniwa kuwepo kwenye galaksi yetu.

Hii inathibitishwa na utafiti mpya uliochapishwa na jarida la kisayansi la Astrophysical Journal, ambalo linazingatia vitu mbilikimo vya kahawia ambavyo vimepewa jina la "The Accident", kwasababu viligunduliwa kwa bahati sana.

Hivi vinavyotambulika kama vimbilikimo vya rangi ya kahawia ni vitu vidogo sana kuwa nyota na ni vikubwa mno kuzingatiwa kama sayari.

Wakati mwingine huitwa "nyota zilizoshindwa."

"Kitu hiki huchukuliwa kwamba kilikaidi matarajio yetu yote," anasema Davy Kirkpatrick, mwandishi mwenza wa utafiti huo na mtaalamu wa nyota katika Taasisi ya Teknolojia ya California (Caltech).

Utafiti huo unabainisha kuwa kile kimbilikimo kinachotambulika kama 'The Accident' kinaweza kuwa kati ya miaka bilioni 10 na bilioni 13, na kukifanya kiwe na umri wa mara mbili ya vitu kama mbilikimo hivyo vya kahawia vya zamani ambavyo viligunduliwa hapo awali.

Hii inaonyesha kwamba viliundwa wakati galaksi yetu ilikuwa ndogo zaidi na ilikuwa na muundo tofauti wa kemikali.

"Ikiwa kitu hicho ndivyo kilivyo, kuna uwezekano mkubwa vimbilikimo hivyo vya kahawia vya zamani vinavyojificha katika galaksi," anaongeza Kirkpatrick.

Kitu kingine tofauti mbilikimo cha kahawia

Kitu cha kwenye anga kwa jina 'The Accident', kinachojulikana kama WISEA J153429.75-104303.3, kiligunduliwa na mwanasayansi Dan Caselden kwa bahati tu, kwasababu haionekani kama kitu kingine kile mbilikimo kinachopatikana kwenye kwenye galaksi hadi sasa, kulingana na taarifa ya NASA .

Wakati kitu hiki cha kahawia kinaendelea kuzeeka, hupoa na mwangaza wao hubadilika kwa urefu tofauti wa mawimbi, sawa na namna vyuma vya moto hubadilisha rangi wakati vinapoa.

Kitu hicho kiliwashangaza wanasayansi kwasababu mwangaza wake sio kawaida kama unaoonekana katika vitu vingine vya kahawia vilivyozeeka.

Pia wakati mwingine huwa na mwanga dhaifu kwa urefu wa mawimbi muhimu, ikidokeza kuwa ni baridi sana, lakini wakati huo huo inaonyesha mwangaza mahali pengine, ikionyesha kuwa maeneo hayo ni ya joto zaidi.

Haishangazi kitu kama hicho kifupi, cha zamani na rangi ya kahawia lakini ni jambo la kushangaza kupata moja nyuma ya nyumba yetu," anasema Federico Marocco, mwenzake wa Davy Kirkpatrick huko Caltech na mwandishi mwenza wa utafiti huo.

"Tulitarajia kwamba vitu kama hivi tena vya umri huu vipo, na pia tulitarajia vitakuwa nadra sana," anaendelea mtaalam wa falsafa, ambaye amekuwa akisimamia uchunguzi huo kwa kutumia darubini za Keck na Hubble.

Kwa kutumia darubini za ardhini, watafiti walijaribu kutazama 'The Accident'.

Lakini kitu hiki cha kahawia kilionekana dhaifu sana hivi kwamba hakigunduliki, ikithibitisha kuwa ni baridi sana na hivyo basi, ni ya zamani sana.

Watafiti wanakadiria kasi ambayo inazunguka ni uthibitisho mwingine kwamba imechukua galaksi kwa muda mrefu, kwani imevuta vitu vikubwa ambavyo vinaisababisha kuharakisha na mvuto wake.

Kitu hicho kimebainika karibu umbali wa miaka-nuru milioni 50 kutoka Duniani . 'The accident' pia inasafiri kwa kasi ya kilomita 800,000 kwa saa . Kasi hii ni kubwa zaidi ya vimbilikimo vingine vilivyopo katika umbali huo kutoka duniani kama vile 'The Accident'.

Uchunguzi unaonesha kuwa sifa nyingine za The Accident, ni kwamba ina viwango vya chini vya methane, ikilinganishwa na mbilikimo wengine wa kahawia waliopatikana, jambo ambalo linathibitisha zaidi madai kwamba iliundwa miaka milioni bilioni 100 iliyopita wakati mfumo wa mamilioni ya nyota wenye mchanganyiko na vumbi unaoshikiliwa na nguvu ya dunia au galaxy ulipotengenezwa kwa hydrogen na helium, na ukosefu wa kaboni inayohitajika kutengeneza methane.