Mzozo wa makombora wa Cuba: Mwanamke aliyezuia vita vya nyuklia baina ya Muungano wa Usovieti na Marekani

Hii ilikuwa ni mwezi Oktoba 1962. Dunia ilikuwa inakaribia kuingia katika vita vya nyuklia. Tarehe 14 Oktoba, ndege ya upelelezi ya Marekani iligundua kuwa Muungano wa Usovieti (sasa Urusi) ulikuwa umepeleka makombora ya masafa marefu ya nyuklia nchini Cuba.

Mahali ambapo makombora ya nyuklia yalikopelekwa ilikuwa ni umbali wa kilomita 150 kutoka kwenye mwambao wa Florida nchini Marekani.

Chini ya pembe ya Marekani , Muungano wa Usovieti ulikuwa umekusanya rundo la makombora na kutoka eneo hilo maeneo mengi ya Marekani yangeweza kushambuliwa. Tukio hili linakumbukwa katika historia kama moja ya matukio ya kutisha zaidi ya Vita baridi, 'Mzozo wa makombora wa Cuba''

Jibu la Marekani katika hali ya wasiwasi kama hiyo ilitokana na ripopti za ujasusi kutoka wa shirika. Ingawa upelelezi haukugundulika kwa miongo, lakini mtu huyu alikuwa na mchango muhimu katika kuzuwia vita vya nyuklia . Jina lake alikuwa ni Juanita Moody.

Alikuwa ni mtaalamu wa utunzi wa alama za siri (cryptographer) ambaye kazi yake ni kusoma alama au jumbe za siri zilizotukmwa katika lugha iliyofichwa. Bi Juanita Moody alikuwa akifanya kazi katika Shirika la usalama la Marekani (NSA), kitengo kinachoihusu Cuba.

Historia ya Vita baridi

Ripoti zilizondaliwa na Bi Moody bado ni za siri, lakini hivi karibuni baada ya uchunguzi wa mwandishi wa vitabu na mwandishi wa habari David Wallman, kuandika kuhusu taarifa ya mchango muhimu wa Juanita Moody katika matukio ya 1962 uliweza kujulikana.

Katika makala iliyochapishwa kwenye gazeti la Smithsonian Magazine, David Wallman alisema kuwa hilo lilikuwa ni kosa la kihistoria kupuuza jukumu la Juanita Moody katika historia ya Vita baridi .

Katika mazungumzo na BBC idhaa ya Mundo, David Wallman alisema kuwa umuhimu wa mchango wa Bi Juanita Moody hauwezi kupuuzwa. Alitengeneza njia yake ya kukabiliana na tatizo na kuonesha uwezo wake katika hilo. Katika ulimwengu wa wanajeshi wanaume , alikuwa ni mwanamke ambaye alionesha kuwa na uwezo wa kufanya jambo lake mwenyewe.

Katika hali kama hiyo swali linaibuka, jukumu la Juanita Moody katika Mzozo wa makombora wa Cuba lilikuwa ni lipi?, na kwanini taarifa yake haijafichuliwa?

Juanita Moody alikuwa na umri wa miaka 38 mwaka 1962.

Alizaliwa katika mwaka 1924 katika mji mdogo uliopo North Carolina. Katika mwaka 1943, wakati Vita vya pili vya Dunia vilipokuwa vikiendelea, alikuwa amejiunga na Chuo. Aliamua kuwa angejiunga na jeshi la majini.

Mojawapo ya mahojiano na mwanahistoria wa NSA yalitolewa kwa umma katika mwaka wa 2016 ambapo alisema "Nilihisi kwamba wakati nchi yangu iko vitani na ninasoma hapa katika eneo hili zuri katika chuo chini ya anga la bluu. Haiwezi kuwa sawa."

Juanita Moody alitumwa katika Arlington Hall, Virginia, ambako kulikuwa kitengo cha ishara za ujasusi za NSA.

Pale alipata mafunzo kuhusu utambuzi wa taarifa za ishara zilizofichwa zinazotumiwa kuficha taarifa. Alipewa kazi katika kikundi ambacho kilikuwa kikifuatilia mifumo ya mawasiliano ya Wanazi.

Alifanya kazi na wenzake katika kutengeneza mashine kutokana na kazi ya mwanamahesabu Alan Turing kuhusu alama za siri na kuthibitisha kipaji chake.

"Alitumia teknolojia mpya kusaidia ujasusi kufanya kazi kwa kiwango cha juu ," anasema David Wallman.

Juanita Moody alishikilia nyadhifa za juu tangu kuundwa kwa NSA mwaka 1952, ambapo kazi yake ilikuwa ni ya kutambua taarifa mbali mbali zilizopo haraka iwezekanavyo na kuziwasilisha kwa wale waliokuwa wamewezeshwa kuchukua maamuzi .

David Wallman ameandika , "Juanita Moody alikuwa mtaalamu katika matumizi ya data kubwa kabla ya dhana ya tathimini ya data kuwepo."

Mzozo wa Cuba wa makombora

Mnamo mwaka 1961, Cuba ilikubali ofa ya kiongozi wa Usovieti Nikita Khrushchev ya usaidizi baada ya jaribio la baadhi ya Wacuba waliopewa mafunzo na CIA- kuipindua serikali ya Fidel Castro kutofanikiwa.

Muungano huu wa Cuba na Muungano wa Usovieti uliigeuza nchi hii ya kisiwa kuwa kitovu cha Vita baridi. Wakati huo macho ya Wamarekani yaliigeukia Cuba. Na Juanita Moody alifanywa kuwa kiongozi wa kikosi cha maafisa kilichobuniwa kukusanya taarifa kuihusu Cuba.

Kazi ya maafisa hao ilikua kunasa jumbe za redio za mawasiliano , data za minara ya mawasiliano, safari za meli na taarifa zoozte ambazo zingeweza kunaswa.

Kando na kazi hii, NSA ilijenga vituo vya ujasusi katika Florida na kusambaza ndege za upelelezi. Chini ya operesheni hii, Meli za kikosi cha wanamaji zilitumwa zikiwa na mifumo upelelezi ambayo haikuweza kugundulikwa kwa urahisi.

Kwa raslimali hizi, kikundi cha Bi Moody kiligundua kwamba Cuba ilikuwa imeboresha mifumo yake ya mawasiliano ya usalama . Pia waligundua kuwa shughuli za majini baina ya ngome za kikosi cha majini za Muungano wa Usovieti na Cuba zilikuwa zimeongezeka.

Ripoti za Juanita Moody

Meli za aina hiyo zilikua zinafika Cuba ambayo nyaraka hzikuwa zimekamilika. Uzito wa bidhaa zilizokuwa zinapakiwa kwenye meli hizo haukuwiana na uzito uliorekodiwa bandarini.

Ilionekana kwamba vitu vilikuwa vikipakuliwa kutoka kwenye meli usiku.

Timu ya Bi Woody iliweza kusikia mazungumzo kuhusu kuishambulia ndege kwa kutumia vifaru vya kijeshi, mnara na silaha, na kwamba Wasovieti walikuwa wamefika Cuba.

Taarifa ya David Wallman ilimnukuu Juanita Moody kisema, "Hali katika Cuba inakuwa ya wasi wasi."

Juanita Moody aliagizwa kuwasilisha taarifa alizokusanya kwa mfumo wa ripoti .Naibu Waziri wa ulinzi Edward Lansdale alimwambia, "tunataka kujua kile unachokijua kuhusu Cuba. Kama una hofu zozote, basi ...Tunataka kujua kila kitu unachokifikiria kuhusu Cuba." Ni wakati wa kufikiria ."

Juanita Moody alifahamu kila kitu na alijibu bila uoga , "Hakuna wasi wasi."

Katika mwezi wa Februari 1962, alijaribu kumshawisi naibu mkurugenzi wa NSA, Luis Tordella, kutuma ripoti kwa Ikulu ya White House, Wizara ya mambo ya na jeshi. Luis Tordella alikataa kushirikisha ripoti hiyo mashirika mengine.

Kufungwa kwa njia ya meli za kijeshi za Cuba

Lakini anaonesha katika ripoti yake kwa rais President John F. Kennedy kwamba mwishowe, Moody alifanikiwa kumshawishi Luis Tordella kutuma ripoti yake kwa mashirika mengine, ikiwa ni pamoja na CIA.

Kufikia majira ya vuli ya mwaka 1962, ilikuwa wazi kuwa Cuba ilikuwa imeweka mifumo ya ulinzi dhidi ya mashambulio ya anga, na Urusi ilikuwa imeanza kusogea karibu na Cuba katika maeneo ambako meli za Marekani zilikuwa zimetia nanga. .

Mwezi Agosti, kufuatia ripoti ya Juanita Moody, CIA ilimwambia Rais Kennedy kwamba maelfu ya wanajeshi wa Muugano wa Usovieti na idadi kubwa ya vifaa vya kijeshi vilikuwa vimefika Cuba

Hadi wakati huo, Marekani ilizuwia ndege zake kupita juu ya anga la Cuba. Tarehe 14 Oktoba , ndege ya Marekani ilichukua kwa ndege picha 928 za Cuba, ambazo zilionesha Wamarekani kwamba Muungano wa Usovieti ulikuwa umepeleka makombora nchini Cuba.

Kwa kuzingatia ripoti hiyo, Rais Kennedy alianza kuzuwia ndege za Cuba. Lengo la kuzizuwia lilikuwa ni kuzuwia makombora kufika Cuba na kutoa fursa ya mazungumzo na Muungano wa Usovieti.

'Hakujali kuhusu siasa '

Mara tu baada ya kufanyika kwa mazungumzo ya kupeleka makombora ya Usovieti nchini Cuba, kazi ya Juanita Moody iliyofuatia ilikuwa ni kutafuta taarifa kuhusu shughuli za ujasusi za usovieti nchini Cuba haraka iwezekanavyo.

David Wallman anaeleza kuwa Bi Moody alipewa kinasa sauti cha chini ya maji, ndege za upelelezi, vifaa vya kumsaidia kusikia na aina mbali mbali ya zana ambazo ziliweza kufichwa ili kumsaidia katika kazi yake ya upelelezi .

Tarehe 24 Agosti, siku mbili baada ya kuzuiwa kwa ndege za Cuba, kikosi cha Moody kilibaini kwamba moja ya meli za kijeshi za Usovieti iliyokuwa inaelekea Cuba ilikuwa imebadili mwelekeo wake na ilionekana kuelekea nyuma kuelekea Muungano wa Usovieti.

David Wallman anasema kwamba tukio hilo lilionekana kama ishara kwamba muungano wa Usovieti haikutaka kukabiliana na Marekani.

Juanita Moody alihisi kuwa hilo lingepaswa kuripotiwa kwa Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Adlai Stevenson haraka iwezekanavyo. Alikuwa anakaribia kulihutubia Baraza la uslama la Umoja wa Mataifa kuhusu mzozo wa Cuba wakati ule.

Maafisa wa wizara ya mambo ya nje walikataa ombi la Moody, lakini Moody hakujali kuamka usiku kumpigia Balozi Adlai Stevenson katika hoteli yake New York.

Moody anasema, Nilimuita usiku. Nilifanya kile nilichofikiria ni sahihi. Sikujali kuhusu siasa."

Suluhu ya amani

David Wallman anaelezea kuwa taarifa za kijasusi zilizokusanywa na moody zilionekana kama dalili za mapema za kuondoka nje ya Mzozo wa Cuba wa makombora. Ilikadiriwa kuwa suluhu la amani la mzozo linaweza kupatikana.

Tarehe 28 Oktoba, Rais kennedy alituma jumbe mbili kwa Muungano wa Usovieti. Nikita Khrushchev alikubali kuondoa makombora yake nchini Cuba lakini kwa masharti mawili . Kwanza ni kuhakikisha Marekani hawatashambulia Cuba na pili kwamba itaondoa makombora yake nchini Uturuki..

Jukumu la Juanita Moody lilithaminiwa kwa kiwango cha juu na maafisa wa ngazi ya juu wa idara ya ujasusi ya Marekani . Kamanda wa kitengo cha kijeshi cha Marekani cha Atlantic Robert Dennison aliandika barua ya kumshukuru kwa kazi ya NSA nchini Cuba.

David alielezea bayana kwamba Bi Moody amekuwa sehemu ya taasisi zote za serikali akishiriki kikamilifu katika kutafuta suluhu la mzozo wa Cuba, lakini ni katika ripoti yake tu ambapo ukubwa wa mzozo wa Cuba unaweza kuelezewa.

Kutokana na ripoti yake, ndge ya Marekani ilifufua safari zake kupitia anga la Cuba , ambapo baadaye makombora ya nyuklia ya Usovieti yaliyopelekwa huko yaliweza kuonekana.

David anasema, "Vipi kama Juanita Moody angekuwa sio makini kwa kile alichokifanya, kama asingesisitizia kuhusu umuhimu wa kushirikisha taarifa zake na mashirika mengine.

Yeyoye anaweza kubashiri? Aliamua. Jinsi ilivyotolewa, kwa njia ilivyopatikana na jinsi ilivyotolewa kwa kasi, ilisaidia kupata suluhu la amani kwa mzozo wa Cuba ."