Fahamu miji 10 safi zaidi Afrika

Usafi ni mojawapo ya sababu muhimu wakati wasafari wanapofikiria kuzuru eneo lolote lile .

Kulingana na Mtandao wa Nile Post nchini Uganda ,Bara Afrika ndilo bara bora zaidi katika suala la kuimarisha na maendeleo.

Miji mingi barani humo imechukua hatua muhimu katika kuweka mazingira bora na safi kwa raia wake.

Hapa chini ni orodha ya ya miji kumi safi zaidi barani Afrika kwa mujibu wa Nile Post.

1- Kigali, Rwanda

Kigali ni jiji kubwa na lenye watu wengi nchini Rwanda.

Ukisoma historia ya hivi karibuni ya Rwanda, utashtuka kuhusu mabadiliko ambayo nchi hii na mji wake mkuu wa Kigali umepitia ndani ya kipindi cha muda mfupi.

Kulingana na mtandao huo, Kigali ndio mji msafi zaidi barani Afrika kwasababu zifuatazo. Wakazi wote wana shauku ya kuweka mji wao safi. Tembea kwenye barabara za Kigali kwa saa kadhaa na ufuatilie kila kona, na hautapata takataka hata moja, kulingana na mtandao wa Nilepost.

2- Port Louis, Mauritius

Port Louis, mji mkuu wa Mauritius ni jiji la kushangaza ambalo Wamauritias wanajivunia.

Baraza la mji la Port Louis linaweka jiji safi kila wakati.

Kwa ubora wa hewa inayotokana na mazingira, mji huo unashindana tu na miji ya Scandinavia kwasababu ubora wa mji wa Port Louis ni wa hali ya juu sana ikilinganishwa na miji mingine mingi ulimwenguni.

Port Louis ni mji wa pili kwa usafi zaidi barani Afrika.

3- Cape Town, Afrika Kusini

Cape Town, jiji zuri la Afrika Kusini, limeshinda tuzo nyingi za kimataifa za usafiri kwa hali yake ya kuvutia na watu.

Cape Town ina Idara ya Usimamizi wa Taka taka ambayo ina lengo la kuhakikisha usafi wa jumla katika barabara na maeneo ya umma.

Ndio maana fukwe za mji wa Cape Town ni miongoni mwa fukwe safi zaidi ulimwenguni.

Ikiwa ungependa kupata ubora kabisa wa Afrika, lazima utembelee Cape Town.

Cape Town ni mji wa tatu safi zaidi barani Afrika.

4- Tunis, Tunisia

Tunis ni mojawapo ya miji safi kabisa Afrika Kaskazini na Afrika kwa ujumla.

Halmashauri ya mji inawajibika kusafisha mitaa na haiishii hapo tu!

Wakazi wa Tunis daima wanahimizwa kutegemea zaidi vyanzo vya nishati mbadala, pamoja na nishati ya jua, nishati ya upepo, nishati ya mimea, na nyinginezo.

Watu pia wanaendesha shughuli zao kwa kutumia usafiri wa baiskeli na magari ya umeme ambayo husaidia Tunis kukaribia kuwa mji usiochafua mazingira!

5- Windhoek, Namibia

Ikipata shuuku kutoka kwa Ujerumani katika usanifu wake na majina yaayopewa barabara, Windhoek ndio mahali pekee barani Afrika ambapo watu wanaweza kuzungumza Kijerumani!

Licha ya bia na soseji zote za Wajerumani katika kila kona ya mji huo, manispaa ya Windhoek daima inashirikisha jamii za wenyeji katika usimamizi wa taka ngumu, ili kuweka mazingira yake nadhifu.

Mji huo inasemekana kuwa safi, salama kiasi, na ni rahisi kuzunguka.

6- Dar es Salaam, Tanzania

Dar es Salaam ni jmji mkubwa zaidi nchini Tanzania, na pia ni moja ya miji safi kabisa katika bara la Afrika.

Mji huo uko kando ya bahari ya Hindi ambayo inachangia uwe mji mzuri sana na wa kuvutia!

Hupendi kuondoka katika mji huu baada ya kuutembelea.

Hivi sasa, nusu ya mji na maeneo yaliyo karibu yamefunikwa na miti na vichaka ambavyo vinachukua hewa ya dioksidi kaboni na kutoa kiasi kikubwa cha oksijeni angani.

Umuhimu mkubwa pia hupewa kusafisha hifadhi ya maji.

7- Gaborone, Botswana

Taifa lenye demokrasia zaidi barani Afrika pia ni nyumbani kwa mojawapo ya miji safi kabisa barani Afrika.

Mtandao wa Nile Post imesema kwamba Gaborone imebarikiwa na uchumi mzuri ambao unalinganishwa na manispaa yenye busara ambayo inawaelimisha wakaazi kila mara njia za kuchakata upya, mbolea, na kutumia tena.

Ukisafiri kwenda Gaborone, utashangaa kuona mbuga zake kubwa za kijani kibichi na barabara pana ambazo ni safi sana.

8-Algiers, Algeria

Mji mkuu wa Algeria umepewa jina la utani "Paris ya Afrika Kaskazini" kwasababu ya majengo yake ya kupendeza ya mtindo wa Ulaya ambayo yamechanganywa na usanifu wa Arabia.

Manispaa ya Algiers kila wakati inakuja na maoni tofauti ya kupunguza matumizi ya magari ya kibinafsi kuweka hali ya hewa kuwa ya kupendeza.

9- Nairobi, Kenya

Kwasababu ya vilima vyake, mabonde, na mbuga kubwa za kijani kibichi, Nairobi ni maarufu kama " Mji wa Kijani katikati ya Jua".

Raia wengi wa Nairobi hutembea, hutumia usafiri wa umma, au hutumia baiskeli hatua inayopunguza kiwango cha hewa chafu ya Kaboni kwa kiasi

Watu huko Nairobi pia wanapenda sana kuchakata taka.

10- Libreville, Gabon

Mji mkubwa zaidi la Gabon uko pwani ya bahari ya Atlantiki.

Ukumbi wa jiji la Libreville umekuwa na maoni kadhaa ya ubunifu ili kuhakikisha hewa safi ya mji, kama kuongeza malipo ya maegesho ya gari mengi na kuitumia kama njia ya watu kulazimika kutegemea zaidi usafiri wa umma.