'Sikujua kwamba baba yangu alikuwa mwandishi wa vitabu vya ngono'

Sara Faith Alterman wakati wote alihisi kuwa na uhusiano wa karibu sana na baba yake. Na ndipo aligundua anaficha siri.
Sara ambaye alikulia karibu na Boston, Massachusetts, miaka ya 1980s, alihisi kuwa na uhusiano wa kipekee na baba yake, Ira.
"Mimi na baba yangu tulikuwa na mienendo sawa sana," anasema. "Pia tulifanana sana, jambao ambalo ni la kuchekesha kwa sasa ni kwamba msichana mdogo kama mimi angeweza kuwa na muonekano sawa na mtu wa Kiyahudi wa maiaka 40. Tulikuwa na sura sawa za uso na nywele sawa kwa hivyo nilikuwa nataka kumuiga."
Ira pia alikuwa mtu ambaye wakati wote alimwendea akiwa na tatizo ambalo lilihitaji kutatuliwa.
Aliwaridhisha Sara na ndugu yake upendo wake wa lugha na kucheza na maneno - alifanya kazi kama mwandishi wa gazeti kabla kujiunga na masuala ya mauzo, na safari za familia zlitumika kucheza, au kubuni maneno mapya au yale ambayo yanaendana.
"Niilitaka kuwa kama yeye kwa njia nyingi sana," anasema. "Kwa hivyo nilijifunza mengi kupitia michezo hiyo tuliyocheza ndani ya gari. Nilifurahia sana kugeuza maneno na kubuni mapya- nilihisi kuwa ustadi wa baba wa ajabu ambao marafiki wangu hawakuwa nao."

Wazazi wa Sara walikuwa na shauku juu ya mafumbo na kuandaa uwindaji wa utapeli.
Kile ambacho hawakupenda ni kitu chochote walichohisi kinaweza kutishia nidhamu ya watoto wao - kwa hivyo mada zote za watu wazima zilikuwa mwiko kabisa, haswa ngono.
"Wazazi wangu walifany kana kwamba vitu hivyo havikuwepo," anasema. "Sidhani nimewahi kumsikia baba yangu akitumia neno 'ngono'hadi nilipokuwa na miaka 30."
Hali ilikuwa mbaya zaidi ikiwa wanatazama kipindi cha televisheni au filamu iliyokuwa na maudhui ya mapenzi.
"Baba yangu angelisema, "Euch!" na kunyanyuka haraka na kugeuza kituo cha runinga haraka iwezekanavyo au kutoa tepu kwenye mashine ya VCR ya kuonesha kanda ya video, anasema Sara.
"Wakati mwingine, ikiwa hakuweza kugundua kitasa kwenye Runinga haraka, angechomoa tu.
"Nadhani hakutaka kujibu maswali kuhusiana na hilo. Pia nafikiria hakuwa huru kukaa ndani chumba kimoja na watoto wakati kuna kitu kilichokuwa na maudhui ya kingono kilichokuwa kinafanyika."
Lakini wakati mmoja akiwa na miaka minane, Sara alipata ugunduzi ambao ulipinga kila kitu alichofikiria anajua juu yake.

Siku moja akiwa katika chumba cha familia cha kusoma akiwa amechoshwa na kitabu alichokuwa akisoma, Sara alianza kuchakura rafu za vitabu.
Katika rafu ya juu zaidi pembeni aligundua kuna vitabu vingine vimefichwa kwenye mifuko ya kuvutia na kuwekwa pamoja, kuashiria wazi kwamba vimewekwa hivyo kwa lengo la kuhakikisha havionekani.
"Nikajiambia: 'Lazima nijue yaliyomo ndani ya vitabu hivyo,'" anasema Sara.
Vilikuwa tofauti na vitabu vingine ambavyo Sara aliwahi kuviona.
Kurasa za juu zilionyesha vielelezo vya "wanawake wa buxom na wanaume wenye sura ya kusisimua sana wameketi kwenye mapaja yao na kubusiana", anakumbuka - laiti angeliwaona kwenye televisheni ya familia, baba yake angelibadilisha kituo mara moja.
Vichwa vingi vilikuwa na neno "ngono" -na vilijumuisha Jinsi ya Kupata Wasichana na Mwongozo wa Ngono kwa Watu Zaidi ya miaka 30.
Kufikia hapo Sara alisikia wazazi wake wanakuja. Alifahamu fikra kwamba hakustahili kuangalia vitabu hivyo, kwa hivyo alivirejesha. Lakini aligundua kitu ambacho kilimchanganya zaidi.
"Niliona kurasa za kwanza za vitabu hivyo zimeandikwa 'na Ira Alterman' - ambalo ni jina la baba yangu, na hapo nikajiuliza, 'Jamani hii inamaaanisha nini? Baba yangu haandiki vitabu.'"
Kwanza aligundua kuwa baba yake alitajwa kama mwandishi katika vitabu hivyo vyote."Ilikuwa hali ya kutatanisha sana na sikuwa na wakati wowote wa kutathmini kwa sababu nilihitaji kuweka kando vitabu hivyo haraka sana," Sara anasema.

"Ilinichukuwa muda kuelewa kwamba, baba yangu ndiye aliyeandika vitabu hivi vyenye mada za ngono ambavyo sikuhitajika kuona,"anasema.
Baadaye aligundua kwamba kutoka miaka ya 1970, vitabu hivi vya Ira vimeuza mamilioni ya nakala kote duniani na vilikuwa vimetafsiriwa katika lugha nyingi.
Lakini hakuweza kumuuliza moja kwa moja kuhusiana na suala hili.
Alipoleta hati ya ruhusa nyumbani ili aweze kushiriki katika darasa la elimu ya ngono, ilikuwa ngumu sana - Ira hakuweza kumtazama machoni wakati akiisaini. Kwa hivyo kujadili masuala ya uandishi wake ni jambo ambalo halingeliweza kumuingia akilini.
Kutokana na hili uhusiano wake na baba yake uliathirika,
"Niliacha kumwamini kwa sababu nilihisi baba niliyemjua ni tofauti na yule niliyemgundua kupitia uandishi wake," anasema.

Hata hivyo, alipojiunga na shule ya upili, Sara alirejea katika rafu ya vitabu hivyo vilivyofichwa na kujisomea kujipatia maarifa ya jinsi ya kudumisha mapenzi na rafiki wa kiume.
Lakini katika miaka ya1990 ilikuwa vigumu kupata maelezo kuhusu kile kilichofanyika baadaye haikuwa wazi. Ijapokuwa ni jambo la kufedhehesha kusema lakini vitabu hivyo vilikuwa vizuri sana kuliko kitu kingine chochote.
Lakini kilichojitokeza katika vitabu hivyo vilivyoandikwa na Ira ni kwamba vilikuwa sehemu ya machapisho ya vitabu vingi - vyote vimeandikwa na waandishi wa kiume - waliomuangazia mhusika kwa jina Bridget.
"Bridget alikuwa mwanamke mnene," anasema Sara. Alikuwa mhusika aliyekejeliwa sana kuashiria jinsi wanawake wanene walivyodhalilishwa linapokuja suala la mapenzi.
Akitafakari hilo, Sara sasa anatambua kuwa hii ilifany kuwa wazo kwamba wanawake wanene zaidi hawakustahili kuwa vitu vya kutamani, ambavyo vilikuwa na athari mbaya kuhusu mwili wake mwenyewe.
"Jambo la kushangaza zaidi ni kujua kwamba baba yangu alifanya utani huu na alidhani kuwa wanawake wanene hawastahili ngono na mapenzi," anasema Sara.
Kwa hivyo kwa miongo miwili, ingawa walibaki karibu, vitabu vya Ira vilibaki kuwa mada ambayo Sara hakuweza kujadili naye.












