Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je Ubora alioanza nao Pogba utaibeba Man United?
Mabao matatu aliyoweza kufunga Bruno Fernandes yamemfanya kuwa mchezaji wa bora wa mechi ya ligi kuu Uingereza ambayo Manchester United waliweza kufunga 5-1 dhidi ya Leeds katika dimba la Old trafford, lakini Paul Pogba alionekana kuwa ni mwenye msaada kwenye mechi hiyo.
Kwa kipindi sasa hakukuwa na mjadala kuhusu ubora wa Fernandes ndani ya Old Trafford tangu ajiunge akitokea Sporting Lisbon Januari, 2020, huku kwa Pogba pengine ndio matumaini yapo tofauti zaidi.
Siku ya Jumamosi jina la Graeme Souness lilionekana kuvuma zaidi ikiwa ni moja ya ujumbe kwa nyota huyo wa zamani wa Liverpool na Scottland ambaye ametumiwa kama mfano baada ya msaada aliokuwa akiutoa Pogba kwenye mechi hiyo.
Katika utafutaji wa magoli matano, Jina la Pogba limeingia kwenye orodha ya wanaume saba ambao walionekana kuwa na msaada mkubwa katika mechi ndani ya ligi kuu ya Uingereza na hii inamfanya kuwa mchezaji wa kwanza akitokea Manchester United , msaada wa Harry kane uliopelekea magoli 5-2 dhidi ya Southampton septemba 2020.
"Watu wanaongelea ubora wa Paul," Amesema Fernandes, "lakini ubora wake haujadiliwi. Tunafahamu fika anachokifanya na umuhimu wake.
"Paul ni mchezaji mwenye umuhimu mkubwa kwetu. Ili tupate ushindi kama wa leo tulimhitaji sana."
Lakini jambo hili linapitia tafsiri tofauti
Ni jambo la kushangaza kwamba katika mchezo mmoja Pogba ameweza kuweka tofauti ya kimahesabu ya kuisaidia timu ukilinganisha na mechi tatu za msimu wa uliopita.
Pasi ya kwanza ya wazi aliyopewa Fernandes ilikuwa ngumu kutafsiriwa na Pascal Struijik na kumfikia Mason Greenwood, pasi fupi kwa Fernandes kwa mminyio wa chini alioutoa kwa mguu wake wa kushoto kueleke kwa Fred katika nafasi ya kukamilisha mzunguko wao.
Mchanganuo wa mchezo mmoja unamuweka Pogba juu kwenye orodha ya wachezaji wenye ushawishi mkubwa ulimwenguni.
Tatizo ni kwamba licha ya kufikia viwango hivyo bado raia huyo wa ufaransa ameonekana kuwa hawezi kuwa na mchango zaidi kwenye mechi.
Ndio maana kumeonekana kuwepo kwa mazungumzo mengi katika majira ya joto kama wangemuuza mchezaji huyo ambaye aliingia Manchester United kwa dau la £89m akitokea Juventus mwaka 2016 - kwa mara ya pili - huku mkatana wake ukisalia mpaka kipindi kijacho cha joto.
Kwasasa Lionel Messi ameshakamilisha usajili wake .
Paris St-Germain ikiwa ndi klabu pekee yenye hadhi kutokana na uwezo wake wa kifedha na kimatamanio wa kukamilisha usajili katika dirisha hili la sasa.
Lakini ujio wa Messi nchini Ufaransa unamaana kuwa hawatomtaka mchezaji mwingine yoyote na hii inamfanya Pogba kusalia kwenye timu yake ya sasa.
Mazungumzo yanaweza kuendelea juu ya hatma ya mchezaji huyo huko mbeleni, na chaguzi zilizokubalika kwa muda mrefu zimesalia mbili .
Ama Pogba ataondoka msimu ujao wa joto kama mchezaji huru-wakala wake Mino Raiola alitumia mbinu hiyo hiyo kwa mchezaji Gianluigi Donnarumma msimu uliopita aliondoka AC Milan kwenda PSG - au atasaini nyongeza ya faida na kukaa na Manchester United.
Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameonekana kuchoshwa na mazungumzo yanayomhusu mchezaji huyo licha ya kwamba alifuatwa mara mbili, katika mkutano wake na waandishi wa habari alijaribu kukimbia maswali na kubainisha kuwa kwa sasa anaangalia kwa undani namna kikosi chake kinavyocheza.
"Paulo ana maono na ameonyesha viwangoo bora zaidi," alisema. "Nimevutiwa sana na viwango vyake sanjari na utayari wake pia. Anaonekana yuko tayari kusonga nasi.
"Miezi 18 iliyopita imekuwa ya kushangaza - mwingiliano pekee umekuwa kupitia vyombo vya habari na kutazama mechi kwenye runinga ili kurudisha umoja wetu kwa mashabiki. Hii ndio Manchester United halisi. Hivi ndivyo nilivyoiwezesha timu kupitia Edinson [Cavani ] na akasema huwezi kuondoka baada ya msimu mmoja bila mashabiki. Kujibu swali lako 'ndio'. "
Swali ni Je? Mashabiki wanaorudi wanaweza kuwa wanafanya kumshawishi Pogba kusalia klabuni hapo.
Inaweza isiwe sibabu mojawapo, Fedha iliyowekwa huenda ndio inaweza kumaliza mazungumzo ya mchezaji huyo mwenye miaka 28 na kuamua kitakachotokea hapo baadae.