China yafoka kwa hamaki baada ya Marekani kukubali kuipa Tawain silaha nzito na hatari

Chanzo cha picha, AFP
Marekani imeidhinisha uuzaji wa mifumo ya silaha za howitzer kwa Taiwan katika mpango wenye thamani ya hadi $ 750m, Pentagon imetangaza na kusababisha China kulaani vikali hatua hiyo
Idhini ya Idara ya masuala ya kigeni ilitangazwa Jumatano kufuatia uuzaji wa silaha kwa kisiwa hicho mwaka jana kuwa ni pamoja na ndege zisizo na rubani(droni) na na makombora ya kujikinga ya pwani yaliyokusudiwa kuboresha uwezo wa Taiwan na kukatisha tamaa uvamizi unaowezekana kutoka China, ambayo inadai Taiwan inayosimamiwa kidemokrasia ni eneo lake, ambalo inaweza kulichukua kwa nguvu ikilazimu
Mauzo hayo yatajumuisha mifumo ya ufundi wa vifaa vya kufyatua makombora vya 40 155mm M109A6, vifaa vya mwongozo wa usahihi 1,698 kwa vitufe, vipuri, mafunzo, vituo vya ardhini na uboreshaji wa wa muundo mzima wa ulinzi wa Taiwan .
Marekani inatekeleza 'wajibu wake kisheria'
Utawala wa Rais Joe Biden umeidhinisha mauzo mengine ya kibiashara ya moja kwa moja kwa Taiwan tangu achukue madaraka mapema 2021, na imetaka kuimarisha uhusiano zaidi na kisiwa hicho, na kusababisha hasira kutoka Beijing.
Shirika la Ushirikiano wa Usalama na Ulinzi la Pentagon liliarifu Bunge kuhusu uwezekano wa uuzaji Jumatano.
Kama mataifa mengi, Amerika haina uhusiano wowote wa kidiplomasia na Taiwan lakini inahitajika na sheria ya 1979 kukipatia kisiwa hicho kinachojitawala njia ya kujilinda na ndio mshirika wake muhimu zaidi wa kimataifa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Licha ya idhini ya Idara ya mashauri ya kigeni arifa hiyo haionyeshi kuwa kandarasi imesainiwa au kwamba mazungumzo yamekamilika.
Ikiwa makubaliano kama hayo yamesimamishwa, Bunge pia linaweza kupitisha sheria inayozuia uuzaji, ingawa kumekuwa na nia adimu sana ya kisiasa ya kuzuia uuzaji wa silaha za Marekani kwa Taiwan katika miaka ya hivi karibuni kwani Warepublican na Wanademocrat wameweka kipaumbele kile wanachokiita kukabiliana na uchokozi wa Wachina.
China yaaapa kuchukua hatua 'kali'
Siku ya Alhamisi, wizara ya ulinzi ya Taiwan ilielezea "shukrani za dhati" kwa serikali ya Marekani , ikisema katika taarifa mauzo hayo yangesaidia vikosi vyake vya ardhini kuongeza "uwezo wao wa kukabiliana haraka na mashambulizi".

Chanzo cha picha, AFP
Wizara hiyo iliita msaada unaoendelea wa silaha za Marekani kama "msingi wa kudumisha utulivu wa kikanda".
Wakati huo huo, wizara ya mambo ya nje ya China ilisema "ilikuwa inapinga kabisa" mauzo hayo na imewasilisha " vikali maoni yake " kwa Washington, kulingana na taarifa ya msemaji wake kwenye tovuti ya wizara hiyo.
Msemaji huyo alisema mauzo hayo "yaliingilia" katika maswala ya ndani ya China na alionya kuwa Beijing itachukua hatua za kukabiliana na suala hilo iwapo litaendelea















