Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Familia yawashitaki maafisa wa New York juu ya picha za video za mauaji ya msichana wao
Mama wa msichana mwenye umri wa miaka 17 ambaye aliuawa mwaka 2019 amewasilisha mashitaka mahakamani akiwashutumu maafisa kwa kutoa video za ngono na mauaji yake kwa vyombo vya habari.
Taarifa za kifo cha Bianca Devins zilisambazwa sana na vyombo vya habari wakati picha zilizotumwa na mtu aliyemuua zilisambazwa kwa haraka kwenye mitandao ya kijamii.
Sasa waraka wa mashitaka wa familia yake unadai kwamba picha zilizorekodiwa na mtu aliyemuua zilitolewa kwa watengenezaji wa makala.
Familia hiyo inamshitaki kaunti ya Oneida katika jimbo la New York na maafisa ikiwa ni pamoja Mwanasheria wa Wilaya Scott McNamara.
Mashitaka hayo yanadai "wakitoa taarifa kwa uzembe bila kujali " zinazomuhusu muathiriwa "wakitanga ushahidi kwa uzembe " kwa waandaaji wa vipindi wakitaka kuficha kesi.
Mashitaka hayo yanadai Kimberly Devins, mama yake Bianca, alishitushwa sana kubaini kuwa video iliyochukuliwa na Brandon Clark imesambazwa.
Sasa anahofia video inayowaonesha wakifanya ngono pia itasambazwa sana kwneye mtandao , sawa na picha alizosambaza za mauaji ya binti yake.
Anawshitaki pia maafisa kwa kuvunja sheria za ponografia za nchi, kwasababu ushahidi ulijumuisha picha za video ya Bianca akifanya ngono na Brandon Clark kabla ya kumuua.
BBC iliwasiliana Ofisi ya Mwanasheria wilaya na pamoja na kiongozi wa Kaunti ya Bw McNamara, lakini wote hawajajibu.
Tarifa ya mauaji ilisambaa sana
Bianca Devins aliuawa julai 2019 na Clark, 21, ambaye alimdunga kisu katika gari lakewakati walipokuwa wakielekea nyumbani kutoka katika tamasha la Queens, katkka mji wa New York .
Alirekodi shambulio kwenye mtandao-akituma picha za kuogofya za mwili wa Bianca kwenye kumbi za mitandao ya kijamii kama Snapchat na Instagram, pamoja na mitandao mingine ya mawasiliano inayotumiwa na marafiki wa Bianca.
Alijaribu kujiua pia baada ya kumuua, lakini alinusurika. Alishitakiwa na akahukumiwa kifungo cha miaka 25 jela mwezi Machi mwaka huu.
Picha za Clark zilizotumwa za mwili wa Bianca Devins zilisambaa haraka sana kwenye mitandao ya kijamii baada ya mauaji yake.
Baada ya kukamatwa, ilijitokeza kuwa Clark pia alikuwa amerekodi video ya mauaji.
Mashitaka hayo yanasema kwamba kuna picha zilizomuonesha akifanya ngono na msichana huyo mwenye umri wa miaka 17 kabla ya kumdunga kisu hadi kumuua baada ya kumshutumu kwa kutokuwa mwaminifu kimapenzi katika kile kilichoonekana kama "hasira ya wivu".
Picha alizozihofia kwa muda mrefu Kimberly Devins zitaoneshwa kwa umma, na kulingana mashitaka yake anataka hakikisho kutoka kwa waendesha mashitaka wa Kaunti ya Oneida County kwamba picha hizo zitalindwa.
Kulingana na mashitaka hayo, anadai baadaye aliambiwa kuwa na waandaji wawili wa makala kwamba wamepewa video za ngono na mauaji na ofisi ya mwanasheria wa wilaya , pamoja na picha za utupu kutoka kwa simu ya binti yake.
Mauaji yake yalioenezwa kwa umma yalipelekea ongezeko kubwa la ukuaji wa mtandao wake pamoja na muuaji aliyemuua huku watu wasiojulikana wakiingia na kutuma tena picha ili kuvutia mazungumzo kuzihusu.
Kimberley Devins amesema bado anapokea matusi ya mtandaoni na picha za ponografia za mwili wa binti yake kutoka kwenye mtandao.