Viumbe hivi vya angani hatuvijui! Marekani yasema

Maelezo ya video, Viumbe wa ajabu waliothibitishwa na Marekani kuwepo angani

Serikali ya Marekani imesema kuwa haina ufafanuzi kuhusu uwepo wa viumbe vya ajabu angani vilivyoonekana na rubani wa jeshi.

Taarifa za ripoti ya Pentagon iliyotolewa Ijumaa inasema ripoti 144 ziliyotolewa kuhusu matukio ya namna hii tangu mwaka 2004, lakini hayajaweza kupata ufafanuzi.

Aidha ufafanuzi hauondoi uwezekano wa kuwa vitu vya ziada vipo katika uso wa dunia.

Congress wanataka ripoti hiyo baada ya jeshi la Marekani kueleza mara kadhaa mifano ya viumbe vinavyoonekana vikitembea angani.

Vilevile Pentagon ilianzisha kikosi kazi cha anga mwezi Agosti kuangalia ripoti hizo.

Kazi ya kikosi kazi hicho ilikuwa "kugundua, kuchambua na kuorodhesha" matukio ya namna hiyo, na vilevile "kupata ufahamu" juu ya "asili na chimbuko" la viumbe hao wa ajabu , Pentagon ilisema.

Je ripoti ilibaini chochote kipya?

Ripoti mpya iliyotoka Ijumaa inasema kuwa katika ripoti 144 ,kesi za viumbe wasiofahamika zimekuja miaka miwili iliyopita baada ya jeshi la maji la Marekani kutoa ripoti.

Katika kesi 143 zilizoripotiwa, zilikuwa hazina taarifa za uhakika au takwimu ambazo zinaweza kutoa ufafanuzi kuhusu matukio hayo kwa uhakika".

Ni suala muhimu , ila hakukuwa na ishara za wazi zinazoelezea uwepo wa viumbe hivyo vya ajabu duniani " kutoka kwa watu wa anga lakini haimaanishi kuwa havipo.

UAP "inawezekana hawakuwa na ufafanuzi mmoja", taarifa ilisema.

Baadhi ya sababu zinaweza kuwa za teknolojia kutoka katika mataifa mengine kama vile China au Urusi, nyingine zinaweza kuwa sababu za kiasili kama vile saruji kufika katika mfumo wa rada, wakati ripoti ikipendekeza kuwa inawezekana kuwa na mpango ambao ulikuwa unaendelezwa na operesheni za Marekani.

Kesi nyingine ambayo walipaswa kuzibaini kwa kiwango cha juu ni jinsi viumbe hivyo vilivyo , maana walitambuliwa kuwa wapo kama puto linalodhoofika, taarifa ilisema.

Taarifa iliongeza kusema kuwa UAP imeweka suala la usalama wa safari za anga na kuhoji juu ya usalama wa taifa la Marekani".

Kikosi kazi sasa kinaangalia namna ya kuongeza taarifa na kutafuta taarifa zaidi na kuongezea kwenye suala la ufadhili kwa ajili ya utafiti zaidi .

Kuna ushaidi gani?

Idara ya usalama ya Marekani imetoa video ya UAPs mwezi Aprili 2020.

Ilisema kuwa ilipigwa picha na wanajeshi wa majini wa Marekani.

Taarifa ya habari ya CBS News-katika mfululizo wa dakika 60 mwezi uliopita, nahodha alijadili suala la kuona viumbe visivyofahamka katika bahari ya Pacific ambapo vilionekana katika kioo wakati meli ikitembea.

Nahodha mmoja alieleza kuwa kiumbe hicho kuwa cheupe, na kina umbo la mviringo.

"Na hivyo ndivyo kinavyofanana tofauti yake ni kuwa kilikuwa na kasi zaidi na ngumu kugundua jinsi kilivyo, shuhuda Alex Dietrich ambaye ni nahodha aliiambia BBC