Hivi ndivyo mabilionea na mamilionea wanavyotumia fedha zao

Fedha sarafu ya dola

Chanzo cha picha, AFP/Getty

Maelezo ya picha, Fedha sarafu ya dola
    • Author, Asha Juma
    • Nafasi, BBC Swahili

Pesa ni kitu cha ajabu sana, mtu anazitafuta kwa udi na uvumba na anapozipata anazitumia kwa matumizi yake aliyojipangia au alichokipatia kipaumbele.

Lakini kama wanadamu tunatofautiana katika matumizi.

Jarida la Business Insider liliwahi kuangazia vile bilionea wa kawaida anavyoweza kutumia dola milioni 80 kwa mwaka, huku Wamarekani wengi wakiwa na kipato cha nchini ya dola 60,000.

Na miongoni mwa mabilionea wakubwa duniani, Jeff Bezos akiwa mmoja wao, akiweza kutumia dola 88,000 kiwango hicho kikiwa sawa na matumizi ya wastani ya Marekani yaani dola 1.

Kuna baadhi ya mabilionea ambao wamekuwa wakijulikana kwa kuwa makini na utumiaji wa pesa zao lakini kuna wale kama Warren Buffett na Mark Zuckerberg ambao wanajulikana kwa kununua vitu vya kifahari.

Aliyekuwa mke wa bilionea Jeff Bezos

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Aliyekuwa mke wa bilionea Jeff Bezos

Hebu tuangazie jinsi mabilionea na mamilionea wanavyotumia pesa zao.

Usafiri

Kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine huenda kusiwe jambo la kawaida kwako lakini kuna baadhi ambao, hili limekuwa kama uraibu kwao.

Na ili kujiweka katika daraja lao mara nyingi mabilionea na mamilionea hujirahisishia kwa kujitafutia usafiri wao binafsi.

Kuna wale ambao hujinunulia ndege zao binafsi kurahisisha maisha yao wakati wanataka kusafiri kutoka eneo moja hadi jingine.

Kulingana na utafiti uliofanywa na jarida la business insider, asilimia 60 ya mamilionea duniani walisema kwamba kwanza kabisa wanapopata pesa wanachokipa kipaumbele ni kusafiri.

Pengine huenda ugunduzi huu usiwe wa kushangaza hasa kwa wale ambao hupendelea kusoma vitabu au kuangalia filamu zenye wahusika matajiri kwasababu ni jambo ambalo mara kwa mara hujitokeza.

Mfano, kuna kipindi Jeff Bezos, alisemekana kumiliki ndege yake binafsi yenye thamani ya dola milioni 65 aina ya Gulfstream G650ER.

Mfanyabiashara Mark Cuban pia ana miliki ndege yake binafsi aina ya Gulfstream V aliyoinunua dola milioni 40.

Ndege ya kibinafsi
Maelezo ya picha, Ndege ya kibinafsi

Na si hayo tu, mabilionea na mamilionea pia nao huwa na usafiri wa gari lakini tofauti ni kwamba wanayoyatumia wao yanakuwa ni kifahari zaidi.

Bill Gates ni mpendaji sana wa magari ya kifahari, baada ya kuanzisha kampuni ya Microsoft, gari yake ya kifahari aliyonunua wakati huo ilikuwa ni Porsche 911. Baadaye alinunua gari aina ya Porsche 959.

Elon Musk pia naye amedhihirisha kuwa mpenzi wa magari. Mwaka 2013, alinunua gari aina ya Lotus Esprit yenye uwezo wa kutembea ndani ya maji kama nyambizi iliyotumika kwenye filamu ya James Bond ambalo thamani yake ilikuwa ni dola 920,000. Mbali na kuwa ana miliki gari aina ya Teslas, Ford Modeli ya T na Jaguar E-Type Series 1 Roadster.

Ni wazi kwamba kundi la watu walio katoka daraja hili la maisha wanapenda sana magari ingawa kulingana na utafiti uliofanywa na jarida la business insider idadi hiyo iliendelea kupungua.

Mmoja wa mamilionea alisema ''Nimenunua magari aina ya Ferrari, Porsche na old Corvette, filosofia yangu ni kufurahia magari yangu kwasababu nikistaafu sitakuwa nafanya haya kwa kuwa yanaongeza matumizi kwa mwezi.''

Mwengine alisema anapenda magari ya Ujerumani na yeye ana mawili.

Najua pengine unajiuliza magari mengi ni ya nini lakini kilichobainika ni kwamba magari yanawapa furaha moyoni.

Kuna wale ambao wana magari ya kawaida pengine moja na gari jingine la kifahari na pia huwa wanajiwekea malengo kama vile kununua gari la kifahari aina fulani na kuwa nalo kwa kipindi fulani pengine miaka mitano na baada ya hapo mtu anauza alilo nalo na kununua jingine la kisasa zaidi.

Jahazi la kifahari linalotumiwa na mamilionea
Maelezo ya picha, Jahazi la kifahari linalotumiwa na mamilionea

Lakini sio mabilione au mamilionea wote wanaosafiri kwa ndege au magari, kuna wale wanaosafiri kwa kutumia bahari na hutumia usafiri wao binafsi.

Bilionea Shahid Khan ana miliki mashua aina ya 312- Kismet, ambayo pia bilionea Beyoncé na Jay-Z wamewahi kuipanda.

Bilionea wa Urusi Roman Abramovich inasemekana kuwa ndio mwenye kumiliki usafiri wa majini ambao ni wa pili kwa ukubwa duniani, Eclipse, wenye uwanja unaoweza kutua helikopta mbili. Thamani yake ni dola bilioni 1.9.

Kwa Afrika mashariki, mwanamuziki Diamond Platnumz ambaye ni miongoni mwa matajiri anayesemekana kuwa katika kiwango cha mamilionea amenunua gari ambalo ndani mandhari yake ni kama ndege.

Mabilionea na mamilionea hao walionesha kwamba wanapenda kujionea au kupitia tajriba mbalimbali kutokana na kusafiri wala sio kupewa zawadi.

Majumba ya kifahari

Kujinunulia majumba ya kifahari imekuwa kama mtindo kwa mabilionea. Lakini pia ni jambo ambalo limejidhihirisha wazi hata kwa matajiri wa eneo la Afrika au Afrika Mashariki.

Jumba la kifahari

Chanzo cha picha, YOUTUBE/ALEXEI NAVALNY

Maelezo ya picha, Jumba la kifahari

Michael Bloomberg kuna wakati aliripotiwa kumiliki kati ya nyumba 12 na 15 kote duniani kuanzia nyumba anayo miliki katika mji wa New York pamoja na eneo la kifahari huko Vail, Colorado, nyumba mbili mjini London, ikiwemo moja iliyopo Knightsbridge yenye thamani ya dola milioni 18.

Mbali na nyumba yake yenye thamani ya dola milioni 125 huko Seattle, Bill Gates alitumia dola milioni 27 kwa ununuzi wa nyumba huko Wellington, Florida, na dola milioni 18 kununua Rancho Paseana.

Baadhi ya nyumba anazomiliki Bezos huko Marekani ni pamoja na maeneo ya Medina, Washington; Beverly Hills, California; Van Horn, Texas; Washington, DC; na New York.

Chakula

Hili huenda likashangaza kwa watu wa kawaida lakini ndivyo ilivyojitokeza, mamilionea wanapenda kula chakula kizuri.

Chakula

Chanzo cha picha, Getty Images

Na chakula wanachopenda kula sio kwamba ni chakula tu lakini pia kula migahawani.

Na ilisemekana kwamba mara nyingi wakiwa nyumbani wanapenda kujaribu vyakula ambavyo hawajawahi kula hapo kabla.

Utaona ndani ya majokovu yao hakukosi nyama, jibini, vyakula vya baharini, mvinyo, matunda na mbogamboga pamoja na chokoleti nyingi tu.

Mvinyo

Kitu kingine ambacho kwako kinaweza kikakosa maana kabisa lakini kwa mamilionea ni cha msingi ni mvinyo.

Wata wanaokula chakula na mvinyo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wata wanaokula chakula na mvinyo

Baadhi yao wanasema kuwa ni vigumu kula pasipo na mvinyo.

Kuna waliothibitisha kwamba akiba za mvinyo wanazinunua hasa wanapokuwa wameenda kutembelea sehemu fulani mpya pia kuna wale wanaofurahishwa na ladha mbalimbali za mvinyo tena za bei ghali.

Nguo

Ni asilimia 7 pekee ya milionea waliosema kwamba wanapendelea kununua nguo wakidai kuwa ni kutokana na kazi zao au kujiweka nadhifu.

Watu wanaonunua nguo dukani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Watu wanaonunua nguo dukani