Pakistan:Fahamu biashara ambayo inachukuliwa kuwa mwiko nchini Pakistan

Nchini Pakistan, moja wapo ya maeneo hayo ni duka linalouza nguo za ndani za wanawake, ambako kuna mchanganyiko wa desturi zinazochulia hilo kuwa mwiko na pia wanawake wenyewe hawako tayari kuchukua nyadhifa za juu katika makampuni hayo kuhakikisha wanajihisi vizuri.
Miezi 15 iliyopita Mark Moore alijipata amezuiwa na wanaume wawili katika lango la kuingia kwenye duka lililokuwa limezungushiwa vioo vilivyopakwa rangi nyeusi mjini Islamabad nchini Pakistan.
Nini? Wakauliza, alifikiria kwamba ataruhusiwa kuingia katika duka la kuuza nguo za ndani za wanawake? Hapana.
Lakini Bwana Moore aliruhusiwa kuingia baada ya rafiki yake kudanganya kuwa ni mwanadiplomasia na amefika dukani kumnunulia mke wake nguo ya ndani.
Lakini ukweli ni kwamba mfanyabiashra huyo wa Leicester alikuwa akifanya utafiti ambao ulimpa matumaini kwamba ungemsaidia kukamilisha dhamira yake ya kuanzisha biashara ya kuuza nguo za ndani za ubora wa juu, kwa guarama nafuu na zenye kufanya wanunuaji kujisikia vizuri yaani wanawake wa Pakistan.
Tatizo ni kwamba, walinzi walikuwa ni miongoni tu mwa vikwazo atakavyokumbana navyo katika utekelezaji wa biashara hiyo.
Cha msingi kabisa, hili linaashiria kuwa wanaume na wanawake wana mawazo tofauti linapokuja suala la nguo za ndani. Na kwa wanaume, suala hili ni kama lina uhusiano na "hisia za mapenzi na kumfanya mtu kuvutia", Moore anaelezea.

"Wanazungumza na kufanya mazungumzo ya lesi na kitambaa angavu.. wakati ambapo kwa wanawake ni kitu ambacho wakivaa watajihisi vizuri na pia kuwa na bidhaa ambayo wanaweza kuitegemea."
Kwa wanawake wengi Pakistan, hawawezi kumudu kununua nguo za ndani kutoka nje ya nchi. Hili ni jambo ambalo kwao linaweza kuwa ndoto tu.
Wanakuwa hawana chaguo zaidi ya kuvaa zile ambazo vitambaa vyao sio vizuri, zinachubua ngozi na kadhalika.
"Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, sijawahi kupata chupi au sidiria zaizi yangu yenye umbo ninalotaka," Hira Inam, 27, amezungumza na BBC akiwa nje ya soko la Anarkali mjini Lahore. "Mara nyingi kitambaa chake huwa sio kizuri. Zinawasha sana na mara ninapopata josho, napata harara kuzunguka chuchu."
Maneno yake yaliungwa mkono na wengine waliokuwepo sokoni.
"Nimetumia muda mwingi, pesa na nguvu kubwa kutafuta sidiria inayonitosha vizuri," mwanamke mwingine amesema, ingawa hakutaka kutajwa jina lake. "Lakini sijawahi kupata. Chuma kilichopo kwenye chuchu ndio cha kwanza kuanza kutoka. Na inaweza kudhuru ngozi yako ikiwa mtu hayuko makini."
Kwa hiyo hitaji la kupata nguo za ndani zenye ubora, za gharama ya chini bila shaka liko wazi laki bado biasha ya nguo za ndani ya Bwana Moore anazozitengeneza katika kiwanda chake kilichopo Pakistan hazina soko la haraka.
Kwanini?
Kwa kuanzia, sio watu wengi wanajua kuhusu hili. Kutangaza biashara yako kwa wanawake nchini Pakistan kidogo ni changamoto. Hasa nguo za ndani, suala hilo ni mwiko kulizungumzia hadharani.
Kwa wanawake wanaoishi maeneo ya mbali, majarida ndio muafaka kutoa matangazo yanayokubalikwa kwa wanunuzi.
Lakini baada ya kuingia enzi ya kidijitali, majarida hayo yamekosa soko. Wakati huo huo kampeni katika mitandao ya kijamii - pengine ndio njia ambayo huenda ikawa nzuri zaidi - lakini pia kuna uwezekano mkubwa matangazo hayo yakachukuliwa kuwa "matusi".
Na sio kwamba wanawake wanaweza kuvutiwa kununua bidhaa hizo kwa kuangalia kupitia dirishani kama Bwana Moore alivyogundua miezi kadhaa iliyopita.
Maduka mengi ya kuuza nguo za ndani hayana majina kuyatambulisha na pia yamewekwa vioo vya rangi nyeusi.

Kuna baadhi ya maeneo ya kufanya manunuzi ambapo maduka ya nguo za ndani za kike ni maarufu sana lakini ni kidogo tu wanaofika.
Bwana Moore alisema kuwa ushauri aliopewa ni kushirikiana na makampuni makubwa na hilo lina maanisha kwamba kuelezea dhana ya kuwa bidhaa hizo ni salama, gharama ya chini wala sio kusema zinapendeza hasa katika maeneo yenye wanaume.
"Changamoto yangu kubwa sasa hivi ni kufahamisha wengi kwamba chupi na sidiria sio bidhaa za kusimumua," Moore ameogeza.
"Ni bidhaa ambayo ni rahisi kutumiwa na yenye kumfanya mtu kuhisi vizuri na kufanya manunuzi na mauzo yake kuwa jambo la kawaida."
Kampuni nyingi alizotembelea Bwana Moore alibaini kwamba wabunifu wengi wanaidhinisha utengenezaji wa nguo hizo ni wanaume.
"Lazima tutoe mawazo yetu kwa wanaume hawa," anaelezea Qamar Zaman, meneja anayesimamia uendeshaji wa shughuli wa kampuni ya Faisalabad.
"Wanawake mara nyingi ni wsaidizi na wao huitwa tu kutoa maoni yao. Lakini ni mazungumzo ambayo yanachukuliwa kutokuwa ya kawaida na wanawake huwa hawako huru kutoa mawazo yao kwa uwazi hasa wakiwa kwenye mikutano yenye waume."
Majaribio yao ya wanawake kuchukua majukumu ongozi zaidi viwandani bado hayajafanikiwa.
"Tulitangaza kazi kwa wanawake kuchukua nafasi za juu lakini tukasikia watu wakisema kwamba kwanza watazungumza na familia zao kabla ya kurejesha majibu," Bwana Moore anaelezea.
"Kuna wawili waliorejea kwetu na kutueleza kwamba familia zao zimekataa kuwaruhusu kufanyakazi katika kiwanda cha kutengeneza nguo za ndanipeople."

Mmoja wa wafanyakazi Sumaira amesema kuwa mume wake aliandamana naye wakati anaenda kusailiwa.
"Na baada ya kupata kazi, mume wangu aliniomba nisiwaeleze wanafamilia wengine pale ninapofanya kazi. Kwasababu itakuwa mambo makubwa bure."
Mfanyakazi nwingine anasema kuwa alizungumza na baba yake kabla ya kwenda kusailiwa kwa moja ya nafasi zilizokuwa zimetangazwa.
"Na moja kwa moja baba yangu alikataa kunisikiliza," alisema. "Nilimuomba anipe ruhusa niende kujionea mwenyewe na ikiwa sitafurahishwa na mazingira ya kufanya kazi, basi sitakubali kazi hiyo."
Anwar Hussain ameelezea BBC kuwa mwanzoni alikabiliwa na changamoto nyingi kutoka kwa familia na rafiki zake.

"Rafiki zangu walinifanyia mzaha pale ninapofanya kazi. Na familia yangu ikakataa kunirusu nijiunge na kazi hiyo. Na hatimaye nilipojiunga nayo, mwanzoni nilikuwa na haya sana kupitisha sidiria ninayoshona kwa mwanamke mwenzangu. Lakini sasa hivi, nimeanza kuwa sawa kwasababu mwisho wa siku ni kazi."
Hata hivyo sasa hivi kuna jingine lenye kutiwa wenyeji wasiwasi. Ikiwa kampuni hiyo haitafanikiwa kibiashara, Bwana Moore huenda akaamua kulifunga duka lake na kuacha wafanyakazi wengi bila ajira.












