Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 11.06.2021: Sancho ,Hakimi, Sterling, Benitez, Ronaldo, De Gea, White, Xhaka, Lingard

sancho

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United wanatarajia kutangaza kumsaini winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho baada ya Euro 2020 na tayari wamekubaliana masharti ya kibinafsi na mchezaji huyo wa miaka 21.

Chelsea inataka kumsaini beki wa kulia wa Inter milan na Morocco Achraf Hakimi . Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa akinyatiwa na klabu ya PSG.. (Times, subscription required).

Iwapo Chelsea itamsaini Hakimi basi wanaweza kusikiza ofa za kumuuza winga wa England Hudson Odoi 20 au Tino Livramento, huku Aston Villa ikiwa na hamu ya kumsajili beki huyo wa kulia. (Guardian)

Hudson Odoi

Paris St-Germain inachunguza hali ya mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 24, ambaye kandarasi yake katika klabu hiyo ya Barcelona imesalia mwaka mmoja. (Marca)

Barcelona inafikiria kumsajili winga wa England na Manchester City Raheem Sterling ambaye anaonekana kama chaguo la kuchukua nafasi yake Dembele iwapo hataongeza kandarasi yake.

Raheem sterling

Chanzo cha picha, Getty Images

Meneja wa zamani wa Liverpool na Newcastle Rafael Benitez anawania umeneja wa Everton baada ya kazi hiyo kuachwa wazi. (Mail)

Mmiliki wa klabu ya Inter Miami Jorge Mas amethibitisha kwamba yeye na mmiliki mwenza wa klabu hiyo David Beckham wamekuwa na mazungumzo na mshambuliaji Muargentina Lionel Messi, 33, kuhusu kujiunga na timu hiyo kama sehemu ya mazungumzo ya mkataba na Barcelona wa miaka 10 wa mchezaji huyo nyota. (Miami Herald)

Mshambuliaji wa Brazil Neymar, 29, ameweka sharti aliposaini mkataba mpya na PSG kwamba hawatamuuza mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, msimu huu. (AS - in Spanish)

Neymar

Chanzo cha picha, Reuters

Tottenham wanafanya mazungumzo na winga wa Borussia Monchengladbach Mfaransa Marcus Thuram - mwana wa kiume wa mshindi wa Kombe la Dunia Lillian - kabla ya uwezekano wa uhamisho msimu wa majira ya joto. (RMC Sport - in French)

Mkurugenzi ajaye wa michezo Fabio Paratici atamuambia Harry Winks kwamba Tottenham itasikiliza ofa kwa ajili ya kiungo huyo wa kati Muingereza mwenye umri wa miaka , 25, msimu huu. (Football Insider)

Mlinda lango wa Muhispania David de Gea, 30, anatarajia kubakia katika Manchester United hata baada ya msimu huu. (Sun)

Arsenal wamejiunga na Liverpool, Tottenham na Manchester United katika azma yao ya kusaini mkataba na mlinzi wa Brighton na England- Ben White, 23. (Mirror)

Roma wanakaribia kukamilisha taratibu za kusaini kandarasi na kiungo wa kati Mswizi Granit Xhaka, 28, kutoka klabu ya Arsenal. (Corriere dello Sport - in Italian)

Kiungo wa safu ya kati wa timu ya Ujerumani ya RB Leipzig Muaustria Marcel Sabitzer, 27, ambaye awali alihusishwa na taarifa za kuhamia klabu ya Tottenham, anataka kuondoka katika klabu hiyo ya Bundesliga na anaweza kuondoka kwa mauzo ya pauni milioni 15 msimu huu. (Athletic, subscription required)

Burnley wamekubali mkataba mpya na meneja Sean Dyche, 49, ambaye anatarajiwa kusaidiwa katika kipindi cha dirisha la uhamisho la msimu wa majira ya joto. (90min)

Meneja wa zamani wa Chelsea Frank Lampard amerejea kazini lakini mara hii katika klabu ya Crystal Palace baada ya mazungumzo na meneja wa zamani wa Wolves Nuno Espirito Santo kugonga mwamba. (Mirror)

West Ham wameongeza bidii katika kusaini mkataba wa kudumu na Jesse Lingard kutoka Manchester United baada ya kiungo huyo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 28 kukosa katika orodha ya wachezaji wa kikosi kitakachocheza katika European Championship. (Sun)