Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Fahamu kwanini NASA inachunguza tena Venus, sayari ambayo ni "kama kuzimu" licha ya kufanana Dunia
Shirika la anga la Marekani, NASA, limetangaza safari mbili kuzuru sayari ya Venus.
Lengo kuu ni kuelewa jinsi sayari hii ilivyobadilika kuwa ''ulimwengu wa kuzimu" licha ya kuwa na sifa za kufanana na Dunia
Wanasayansi wanaamini Venus, zamani huenda ilikuwa na bahari na hali ya hewa sawa na Dunia.
Tafiti hizo mbili zilichaguliwa katika mashindano awamu ya tisa ya kipindi cha uvumbuzi cha Nasa, ambacho kilizinduliwa mwaka 2019.
Miradi yote miwili katika sayari ya Venus itapokea ufadhili wa awali wa dola milioni 500 kuanzia uundaji wa chombo hadi wakati zitakaposafiri kati ya mwaka 2028 na 2030.
Chombo cha mwisho cha Marekani kutua Venus kilikua Magellan, ambacho kilizunguka sayari hiyo hiyo mwaka 1990. Chombo zingine ni za kutoka Ulaya na Japan pia zimezuru sayari hiyo kutoka wakati huo.
"Lengo la utafiti huu ni kubaini jinsi Venus ilivyobadilika kuwa ulimwengu sawa na jehanamu, ikiwa na joto ambalo linaweza kuyeyusha chuma," Nelson alisema.
Venus ni sayari ambayo ina joto kuliko sayari yetu , ijapokuwa ni ya pili kutoka ubali wa Jua, baada ya Mercury. Viwango vya joto katika sayari ya Venus ni karibu nyuzi joto 500 .
Uchunguzi huo utajumuisha nini
Katika uchunguzi huo unaofahamika kama D avinci + , kifupi wa uchunguzi mazingira ya gesi, Kemia na mandharu ya Venus.
Davinci + itachukua vipimo vya mazingira ya sayari hiyo ili kuelewa jinsi ilivyoundwa na ilivyokubadilika, na itajaribu kubaini ikiwa sayari ya Venus iliwahi kuwa na bahari.
Mpango huo pia unatarajiwa kutuma picha zake za kwanza za hali ya juu kupitia mfumo wa kijiolijia wa unaofahamika kama "tesserae." Wanasayansi wanaamini kwamba picha hizo zitafanana vitu vilivyopo katika sayari ya Dunia.
Baadhi ya vifaa vya kufanyia uchunguzi vitatolewa na kituo cha angani cha Ujerumani, Shirika la Anga la Italia na Kituo cha Kitaifa cha Ufaransa kinachotoa elimu ya masuala ya anga za mbali.
"Malengo makubwa"
"Inashangaza jinsi tulivyo na Helena mdogo kuhusu sayari ya Venus. Lakini matokeo ya pamoja ya mpango huu utatufahamisha mengi kuhusu sayari hii, kuanzia mawingu yake hadi milima yake ya volkano hadi chini yake," alisema Tom Wagner kutoka kitengo cha sayansa ya masala ya sayari.
Thomas Zurbuchen, Msimamizi Mshirika wa Sayansi katika shirika la NASA, alisema: " Tutatumia teknolojia ya hali ya juu iliyoundwa na NASA na kufanyiwa maboresho katika miaka kadhaa ya shughuli zake za uchunguzi wa anga za mbali. Tunakaribisha mwongo mpya wa Venus ili kuelewa sinsi sayari hii inayofanana na Dunia ilivyobadilika kuwa hatari zaidi kwa maisha. "
"Malengo yetu ni makubwa. Sio tu suala la kuelewa jinsi sayari zinavyozunguka katika mifumo yetu ya solar, lakini pia tunaongeza juhudi za katika tafiti zetu ili kubaini mamba yanayoibuka katika utafiti wa NASA ."
Paul Rincon, mwandishi wa BBC wa kitengo cha sayansi, anasema sayari ya Mars imetawala bajeti ya NASA katika miongo ya hivi karibuni "mambo sasa yanabadilika."
"Kwa muda mrefu baadhi ya watu walidhani Venus ni sayari 'iliyokufa', lakini saya wanasayansi wanaanini huenda ikatoa nafasi ya kuendelezwa kwa shughuli za kijiolojia,"aliongeza.
"Na huenda ilikuwa na bahari kwa zaidi ya mabilioni ya miaka.
Uvumbuzi huu wa kimapinduzi unaonesha kwamba huenda kulikuwa na uhai katika sayari ya Venus
"Kwa wanasayansi waliojitolea kuchunguza sayari ya Venus, mpango huo ni wa kutia moyo sana."
Vidokezo 10 muhimu kuhusu sayari ya Venus
- Ukubwa wake unatoshana na dunia na imepewa jana la "sayari pacha," wa dunia lakini pacha hao hawafanani kabisa.
- Hewa take ni nzito na chafu , iliyojaa gesi chafu ya kaboni iliyozingirwa na wingu la rangi ya manjano ambayo ni ya asidi inayozuia joto, na kuongeza athari ya hewa chafu.
- Ni sayari iliyo na joto kali zaidi katika mfumo wa jua, ijapokuwa sayari ya Mercury iko karibu na jua. Venus iko umbali wa kilomita milioni 108 kutoka kwa jua.
- Kiwango chake cha toto ni karibu nyuzi joto 500, ambayo inaweza kuyeyusha chuma.
- Siku moja katika sayari ya Venus ni sawa na siku 243 duniani.
- Sayari hiyo inazunguka mwelekeo tofauti, kumaanisha jua katika sayari ya Venus Jua linachomoza magharibi na kutua mashariki (Kulingana na mfumo wa mitambo yetu maalum).
- Haina miezi wala pete.
- Mvuke unaotokana na joto lake ni mara 90 zaidi ya mvuke unaosikika Duniani, sawa na shinikizo linalopatikana katika kina cha kilomita 1.5 ya bahari ya duniani.
- Ni sayari ya kwanza iliyofikiwa na chombo cha Nasa cha anga za mbali, Mariner 2, mwaka 1962.
- Muungano wa zamani wa Sovieti ndio nchi pekee uliyofanikiwa kutua chombo chake katika sayari ya Venus (Venera 7, mwaka 1970). Chombo hicho kilidumu kwa muda muchache sana kutokana na mazingira magumu katika eneo hilo.
Chanzo: NASA