Mali:Ufaransa yasitisha uhusiano wa kijeshi na Mali kuhusiana na mapinduzi

Ufaransa imesitisha operesheni za pamoja za kijeshi na Mali juu ya mapinduzi ya wiki iliyopita katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Ilisema ushirikiano wowote utasitishwa hadi itakapopata hakikisho kuhusu kurudi kwa utawala wa kiraia nchini Mali.

Vikosi vya Ufaransa vimekuwa vikisaidia wanajeshi kutoka Mali, Chad, Mauritania, Niger, na Burkina Faso kupambana na wanamgambo katika eneo la Sahel.

Mnamo Mei 25, mwanajeshi mwenye nguvu za kijeshi wa Mali, Col Assimi Goïta, alimwondoa mamlakani rais wa kiraia wa nchi hiyo

Wiki hii kundi la Afrika Magharibi la Ecowas na Umoja wa Afrika (AU) ziliibvua Mali unachama wa makudi hayo

Siku ya Alhamisi wizara ya majeshi ya Ufaransa ilisema kwamba Ecowas na AU wameweka "mfumo wa mabadiliko ya kisiasa nchini Mali".

Iliongeza: "Wakati inasubiri hakikisho la kurejea kwa utawala wa kiraia , Ufaransa imeamua kusimamisha, kama hatua ya muda, operesheni za kijeshi za pamoja na vikosi vya Mali."

Vikosi vya Ufaransa vitaendelea kufanya kazi huko kwa njia huru

Ni nini kinachofanyika Mali?

Kiongozi wa mapinduzi Kanali Assimi Goïta aliteuliwa kama rais wa mpito na korti ya katiba Ijumaa iliyopita - siku mbili baada ya kujitangaza kuwa kiongozi wa mpito.

Alitetea kuondolewa kwa Rais Bah Ndaw na Waziri Mkuu Moctar Ouane kama hatua iliyohitajika kwa sababu walishindwa katika majukumu yao na walikuwa wakitafuta kuhujumu mabadiliko ya nchi.

Askari waliwakamata na kuwaweka kizuizini wanaume hao wawili baada ya mabadiliko ya baraza la mawaziri ambayo Kanali Goita alisema hakushauriwa juu yake.

Pia aliongoza mapinduzi Agosti iliyopita, ambayo ilimfanya Rais mteule Ibrahim Boubacar Keita kulazimishwa kuondoka ofisini.

Kanali Goita ameahidi kuwa waziri mkuu mpya atateuliwa ndani ya siku chache, na kwamba uchaguzi bado utaendelea mwakani kama ilivyopangwa.

Kwanini hali nchini Mali huwa tete?

Mali ni koloni kubwa ya zamani ya Ufaransa, ambayo haina bahari, na maeneo makubwa yanakumbw ana umaksini na hayana maendeleo.

Mapinduzi ya serikali mnamo 2012 yalisababisha wapiganaji wa Kiisilamu kutumia machafuko hayo kuteka kaskazini mwa nchi.

Wanajeshi wa Ufaransa walisaidia kupata maeneo hayo tena, lakini mashambulio yameendelea kwani waasi wamejitahidi kwa kutokuwa na utulivu wa kisiasa katika maeneo hayo ya kaskazini mwa nchi .

Hii yote imesababisha imani ya umma kupungua juu ya uwezo wa viongozi wa jeshi kukabiliana na uasi wa Kiislam ambao umeshamiri katika nchi jirani za Burkina Faso na Niger.

Mali imejipataje katika mgogoro wa sasa?

Rais na waziri mkuu walizuiliwa na wanajeshi saa kadhaa baada ya kutangazwa kwa mabadiliko ya baraza la mawaziri ambalo lilisababisha maafisa wakuu wawili wa jeshi ambao walishiriki katika mapinduzi ya mwaka jana kubadilishwa.

Rais Bah Ndaw na Waziri Mkuu Moctar Ouane walisafirishwa na wanajeshi kwenda kwenye kambi ya jeshi ya Kati karibu na mji mkuu, Bamako.

Katika mabadiliko ya baraza la mawaziri, waziri wa zamani wa ulinzi Kanali Sadio Camara na waziri wa zamani wa usalama Kanali Modibo Koné waliachwa nje .

Hakuna maelezo yaliyotolewa kwa kutengwa kwao.

Nafasi zao zilipaswa kuchukuliwa na Jenerali Souleymane Dacouré na Meja Jenerali Mamadou Lamine Diallo mtawalia. Baadaye waliachiwa huru na kanali Goita akajitangaza kuwa rais wa mpito .Umoja wa mataifa ,Muungano wa Afrika na ule wa Ecowas zimeendelea kulaani kupinduliwa kwa serikali ya kiraia na kutaka utawala utakaoheshimu katiba ya nchi kurejeshwa

Kwanini kujiondoa kwa Ufaransa kunaihatarisha Mali?

Kutokuwepo kwa serikali thabiti nchini Mali kunaweza kukafuua fursa nyingine kwa makundi yaliyojihami .

Mataifa kadhaa ya eneo la Sahel - sehemu ya mataifa kadhaa ya afrika ya kati na magharibi yaliyo jangwani yapo mashakani kwa sababu ya tishio la usalama kutoka kwa makundi mbali mbali yaliyojihami .

Hali hiyo imesababisha maeneo hayo kuwa katika hatari ya kukosa kabisa uthabiti na amani na maelfu ya watu katika nchi kama vile Nigeria , Mali,Chad ,Burkina Faso na Niger wameachwa bila makao .

Ufaransa ambayo imekuwa mstari wa mbele kuzisaidia nchi hizo kukabiliana na makundi mbali mbali ya wapiganaji pia imeonekana kushindwa katika kuleta utulivu katika eneo hilo .

Hali huenda ikawa mbaya zaidi kwa sababu ya kifo cha aliyekuwa rais wa Chad Idriss Deby ambaye alikuwa mojawapo ya viongozi wanaotegemewa kupambana na kundi la Boko Haram ambalo limekuwa likizihangaisha nchi za Nigeria , Chad ,Niger na Burkina faso .